HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hapana sio wanaangalia kwenye mfumo .pale mkishapita kwenda oral zile document zenu zote za ajira portal zinakuwa printed day before interview kwahiyo pale ukishapeleka vyeti huwa wanafananisha kama zile document ndo zenyewe na zile document then wanaangalia hiyo nafasi inahitaji hizo sifa ulizonazo ndo unaitwa uingie ndani pale hakuna cha mfumo pale
Inategemea na idadi ya interview zilizopo siku hiyo ila kama wanamuda wanapitia account ya kila mmoja wakikuta kama ukishawahi kuap load basi shughuri inaishia hapo.
Ila wapo wengine wanaojichoma wenyewe kwa kubeba mavyeti mengi nilishudia kama mara mbili mmoja ilikua interview ya diploma lakini jamaa alikua amemaliza degree akabeba vyeti vyote pale kwenye kukaguliwa wakamzuia na ilikua oral. Mwingine kwenye written ya diploma pia jamaa alikuja vyeti vya degree na CPA wakamzuia.
 
Haya yakizingatiwa angalau yatasaidia kuboresa mazoezi ya usaili yanayoendeshwa na Utumishi nchini:

1. Katika upande wa mwombaji Waboreshe utoaji wa taarifa kama kuitwa, matokeo, ratiba na mabadiliko yoyote kupitia sms kwa sababu taarifa wanazotoa kwenye website na mifumo inaweza kukwamishwa na mtu kutokuwa na intaneti. Pia kuwe na notifications kwe mfumo ua ajira, notifications zinaonesha kila kinachoendelea.

2. Mfumo uweze kuonesha ajira zinazosubiriwa, zilizopita, n.k. katika majedwali tofauti. Hii itasaidia mwombaji kufuatilia kwa umakini bila kukosea kama ameitwa au la ili asichanganye au kusahau ajira yoyote aliyoomba

3. Usajili ulipaswa kufanyika kila mkoa kulingana na wahusika walioomba kama wanapatikana. Na kama itakuwa ni ngumu, basi saili zifanyike katika kanda zote nchini. Hii itasaidia watu kumudu gharama za kusafiri na kufanya usahili.

4. Kuwe na machine ya utambuzi kwa namba za kutoka NIDA. Kutokana na changamoto mbalimbali za waombaji kutokuwa na vitambulisho au nyaraka za utambulisho, mwombaji anaweza kutumia namba ya NIDA kukamilisha utambulisho wake kwa sababu ni njia ya halali na ya kuaminika itakayo ondoa usumbufu katika zoezi la ukaguzi.

5. Waombaji wajulishwe matokeo ya kila hatua ya usahili hata usaili wa mahojiano kwa wakati. Kuna kipindi usahili unaweza kufanyika lakini matokeo yanatoka kesho yake. Napendekeza matokeo yatoke ndani ya siku moja kwa hatua zote za usahili. Hii itaepusha gharama za kuendelea kusubiri kutokana na wengi wao kusafiri kutoka mbali na makazi yao.
 
Inategemea na idadi ya interview zilizopo siku hiyo ila kama wanamuda wanapitia account ya kila mmoja wakikuta kama ukishawahi kuap load basi shughuri inaishia hapo.
Ila wapo wengine wanaojichoma wenyewe kwa kubeba mavyeti mengi nilishudia kama mara mbili mmoja ilikua interview ya diploma lakini jamaa alikua amemaliza degree akabeba vyeti vyote pale kwenye kukaguliwa wakamzuia na ilikua oral. Mwingine kwenye written ya diploma pia jamaa alikuja vyeti vya degree na CPA wakamzuia.
Unaendaje na cheti ambacho hujaombea kazi??kupita kwenye mfumo sio rahisi wale wanakuwaga na document zako pale mezani zote labda unikologe mwenyewe tu
 
Back
Top Bottom