HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hivi nyongeza ya mishahara waajiriwa wapya wanahusika kwenye huo mgao??
Nyongeza ya mshahara hupewa mtumishi baada ya kutumikia ngazi yake kwa mwaka mmoja. Kwa maana hiyo haitawahusu waajiriwa wapya. Ila ongezeko la mishahara huwa linawahusu watumishi wote wakiwemo waajiriwa wapya. Ongezeko la mishahara hupandisha kianzia mshahara kwa kila ngazi. Kwa mfano kwa sasa TGS D1 ni sh 765,000/= kwa mwezi. nyongeza yake kwa mwaka ni 15,000/= kwa hiyo nyongeza itamsogeza mtu kuwa TGS D2 sh 780,000/= kwa mwezi. Waajiriwa wapya watabaki TGS D1 765,000/=.

Ila kama kukitokea ongezeko la mishahara, TGS D1 haitakuwa tena 765,000/= bali zaidi ya hapo kutegemea hilo ongezeko ni la asilimia ngapi. Ikitokea hivyo hata waajiriwa wapya watapata ongezeko hilo la mishahara. Sijajua kwa uhakika kinachozungumzwa ni nyongeza ya mishahara au ni ongezeko la mishahara. Hivi ni vitu viwili tofauti.
 
Habari zenu wakuu, kwa ambao walishapataga kazi kupitia utumishi hua inachukua muda gan mpka kupangiwa kituo chako cha kazi? After kuchukua barua na kuipeleka sehem husika inayoelekeza!
Kutokana na shuhuda za watu hapa, huchukua kati ya wiki mbili na miezi miwili mtu kuitwa kuanza kazi baada ya kuripoti. Ila habari nzuri ni kwamba baada ya kukabidhi barua na kuzaja fomu za taarifa binafsi, unahesabika kuwa umeshaanza kazi na watu wamekuwa wanapokea mishahara hata kabla hawajaanza kazi rasmi. Ila kitu kibaya ni kwamba kama sehemu ulikoajiriwa huna ndugu katika mji huo, na huna pesa za kula na malazi, na nauli ya kurudi nyumbani huna, waajiriwa wapya wanapata shida sana kipindi hiki cha kusubiria. Wengine hulala stendi usiku na mchana hutafuta vibarua ili maadamu wapate chochote cha kuwategemeza!
 
Jamvi la jana hatujapata shuhuda humu, leo tena ngoja tuone kama tutapata hata mmoja wa kumpa pongezi.

Hata hivyo Hongereni sana mnaoendelea kuingia kundini, mkawe watumishi wema

BALENSIAGA ona watu wamelamba Asali eGA, uliisema sana Asali ya eGA ngoja vijana wakaishuhudie huko
 
Habari, naomba kujua kama Kuna aliyebahatika mkeka wa Jana nafasi za database administrator na data analyst kama yupo humu au mnafahamiana, nahitaji anipatie abc za practical na oral inakuwa.
Naomba kuwasilisha.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom