HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Screenshot_20220701-143746_1.jpg
 
TGS D1 ni kianzia mshahara/salary entry point. Baada ya mwaka mmoja mwajiri wako anaweza kukupa nyongeza moja ya mshahara kutokana na utendaji wako wa kazi. In practice karibuni watumishi wote hupata nyongeza kama ikitolewa. Ila mwajiri anaweza akazuia nyongeza ya mwaka kama hajaridhishwa na utendaji wako wa kazi. Na akiam,ua hivyo lazima akupe hiyo taarifa kwa maandishi (hii hutokea nadra sana). Kwa hiyo ukipata hiyo nyongeza unakuwa TGS D2, na kwa ngazi hii nyongeza ya mwaka ni 15,000/= na mshahara wake ni 780,000/= Mwaka unaofuata ukipata nyongeza unakuwa kwenye TGS D3 mshahara wake ni 795,000/=. Itaenda hivyo mpaka unafika TGS D12 -930,000/= kwa mwezi.

In practice siyo rahisi mtu kufika TGS D12 labda kama serikali imeamua kusimamisha kupandisha vyeo. Vinginevyo baada ya miaka kama 4 hivi mtu akiwa ngazi ya TGS D4(at most), kutokana na utendaji mzuri wa kazi mwajiri hupandisha vyeo na mtu kuwa kwenye ngazi ya TGS E1 - 1,000,000/= kwa mwezi.

Kwa mfano mtu akiajiriwa kama Agricultural Officer II -TGS D1, baada ya miaka mnne anaweza kupandishwa cheo na daraja akawa Agricultural Officer I - TGS E1 - 1,000,000/=.
Shukran sana kiongozi, nimekuelewa vizuri sana. Unatupatia elimu ambayo itakuwa na manufaa huko mbeleni tukibahatika kuingia kwenye government. Now tunapambana na private huku.
 
Mpotezeeni huyo amekuja kupotosha uzi na kututoa kwenye mada
Asa kazi zenyewe hatujapata tuanze kujadili mishahara badala ya kupaza saut psrs wajirekebishe na kutoa placement kwa wakat nyie mnakubali kuyumbishwa
mtaani njaa kali kinoma chamuhimu
checkno kwanza,hata tupangiwe mbwinde,tunduru,gamboshi wengine tutaripoti tu kwa mshahara huo huo wa halmashauri ambao baadhi ya watu wana uponda hapa.
 
Kwa hiyo psrs wamegoma kuweka PDF kwa muda wote huu????
Hii week iishe tena bila kimulimuli???
Wametangaza kazi za LGA and MDA wanaona hata aibu kuandika tangazo la nafร si za kazi LGA and MDA wakaweka tu tangazo la kazi ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Msichojua ni kwamba kwenye huu uzi wapo mawakala wa psrs na Moja akicomment mwingine anakuja kusapoti na pia wana tabia ya kujidai kuuliza maswali yenye kulenga kuwatoa nje ya uzi
Ndio maana nasema tuungane tuongee 1 mbona malalamiko yatafika
Tukiongeza Kasi wote tukacomment na kutaja makandokando yao wataacha kututesa jobless.

Kwa wewe unayeogopa kujulikana fungua fake account (fekoro) andika email ya uongo tu inakubali then njoo mzigoni tupush ajenda ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ
 
Back
Top Bottom