HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Mtu unasubiri placement za MDA&LGA ghafla unakutana na tangazo la kazi zilezile....nchi ngumu hii afu tutakuja kuambiwa kuna data base sijui hiyo database ni ya kufugia kuku??
 
WAKUU NITOENI USHAMBA..HIVI HIZI KAZI AMBAZO HAZITAJI TAASISI UNAYOENDA HUWA ZIKO VIPI?MFANO HAPO MHANDISI MAGARI LAKN HAWAJASEMA NI TAASISI GANI..
NA TGS E NI KIASI GANI?

NATANGULIZA SHUKRANI.View attachment 2685319
TGS E1 - E12 Tsh 1,000,000/= hadi 1,209,000/=. Kwa nyongeza ya tsh 19,000/= kwa mwaka.
Yaani TGS E inaanzia Tsh 1,000,000/= na ukomo wake ni Tsh 1,209,000/= kwa mwaka. Kwa ngazi hii mshahara hupanda kwa sh 19,000/= kwa mwaka kama nyongeza ya mwaka hadi ukomo wake ufike. Lakini kwa kawaida mtu hupanda daraja baada ya miaka mitatu au minne na kuhamia ngazi inayofuata, Kwa huyu itakuwa TGS F ambayo huanzia na 1,300,000/= hadi 1,564,00/= kwa nyongeza ya Tsh 24,000/= kwa mwaka!!
Kwa kawaida ngazi ya TGS E hupewa watu waliosoma kozi za miaka 4 huko chuo kama Wahandisi, wafamasia, wanasheria nk.​
 
Fani za science na Tehama ukiondoa afya ni TGS E
Siyo fani zote za sayansi ni TGS E. Inategemea hiyo fani ameisoma kwa miaka mingapi chuo. Kwa mfano afisa kilimo, afisa mifugo, afisa samaki nk hizi zote ni fani za sayansi lakini wamesoma chuo kwa miaka mitatu, kwa hiyo wanaangukia kwenye TGS D1 - TGS D12: 765,000/= hadi 930,000/= kwa mwezi, na nyongeza yao ya mwaka ni Tsh 15,000/=.
TGS E ni kwa fani ambazo husomewa miaka 4 chuo kikuu kama vile wahandisi, wafamasia, wanasheria nk.​
 
Naona post za jana zimenyofolewa zote sijui nini shida
Kwa uzoefu tunafahamu kuwa, wakiamua ku-withdraw tangazo la ajira ni lazima watoe taarifa kwenye tovuti yao na huwa wanafanya hivyo. Ukiona tangazo limenyofolewa na isitolewe taarifa yoyote maana yake ni kwamba, wanafanya marekebisho fulani tu kwenye tangazo na litabandikwa tena muda si mrefu. Ni makosa makubwa kubandika na kuondoa tangazo jumla bila taarifa yoyote kama bado halijapitwa na wakati.​
 
Mtu unasubiri placement za MDA&LGA ghafla unakutana na tangazo la kazi zilezile....nchi ngumu hii afu tutakuja kuambiwa kuna data base sijui hiyo database ni ya kufugia kuku??
Hapo ndipo utajua haujui😂😂😂
 
Kwa uzoefu tunafahamu kuwa, wakiamua ku-withdraw tangazo la ajira ni lazima watoe taarifa kwenye tovuti yao na huwa wanafanya hivyo. Ukiona tangazo limenyofolewa na isitolewe taarifa yoyote maana yake ni kwamba, wanafanya marekebisho fulani tu kwenye tangazo na litabandikwa tena muda si mrefu. Ni makosa makubwa kubandika na kuondoa tangazo jumla bila taarifa yoyote kama bado halijapitwa na wakati.​
Sawa wakala wa psrs
 
Sema usemavyo na kinadharia unaweza kuwa uko sahihi. Lakini katika uhalisia mambo mara nyingine hayaendi kama ilivyotarajiwa!! Tutazunguka sana lakini mchawi hapa ni pesa!! Mara nyingi huwa hazipatikani kwa wakati kama ilivyotarajiwa!! Mipango huwa inatangulia halafu pesa zinakuja nyuma kuja kuwezesha utekelezaji wa mipango. Haiwezekani usubiri pesa zipatikane ndio upange!! Bunge linapopitisha bajeti kwa ajil;i ya utekelezaji wa mipango tarajiwa ya mwaka haina maana kuwa hizo pesa zipo, lakini inatarajiwa kuwa zitapatikana kutokana na vyanzo mbalimbali hasa MAKUSANYO YA KODI, hii ni pamoja na mipango ya kuajiri katika sekta m,balimbali!!

Sekta fulani ikiomba kibali cha kuajiri, ni kwa sababu imeweka fungu la kuajiri katika bajeti yake kwa mwaka husika na bajeti hiyo imeshapitishwa tayari bungeni. Wizara yenye dhamana ya kutoa kibali cha kuajiri ikijiridhisha kuwa anayeomba kuajiri analo fungu la ajira kwenye bajeti yake, hutoa hicho kibali cha kuajiri. Sekta husika ikishapata kibali hicho huwasiliana na WAKALA mwenye jukumu la kutangaza, kufanyisha usaili na kupanga waajiriwa KWA NIABA YA SEKTA INAYOAJIRI. Wakala huyo ni PSRS.

Inaweza ikatokea kuwa pesa iliyotarajiwa kwa ajili ya waajiriwa wapya aidha haijapatikana bado au imepatikana kiasi fulani na si kiasi chote. Kama haijapatikana yote watachukuliwa baadhi tu ya waajiriwa na wengine wabaki nwanasubiri. Kama haijapatikana kabisa maana yake ni kwamba watasubirishwa hadi ipatikane!! Makusanyo ya kodi hayako constant!! na kuna watu hukwepa kulipa kodi na athari yake ni hiyo!! Bado watanzania walio wengi huwa hawaoni umuhimu wa kulipa kodi. Ni mara ngapi umenunua bidhaa na hukupewa risiti ya EFD na wewe hukuona sababu ya kuidai hiyo risiti? Usipodai risiti unamwezesha mfanyabiashara kuiibia serikali mapato yake, na moja ya madhara yake ni haya ya kuchelewesha placement!!

Hakuna wizara hata moja ambayo hufanikiwa kupewa pesa yote iliyokuwa imeidhinishiwa kwenye bajeti yake kwa sababu hiyo pesa haikupatikana yote na hiyo iliyopatikana huenda haikupatikana kwa wakati uliotarajiwa! Hii ina maana kuwa kuna mipango kadhaa ambayo huwa imeshindikana kutekelezeka na kusubirishwa kwa wakati ujao. Ingia kwenye tovuti ya wizara yoyote usome hotuba ya bajeti yake. Huwa wanatoa mrejesho wa bajeti iliyopita na kueleza ilitekelezeka kwa asilimia ngapi!!

Huu ndio ukweli ambao tunalazimika kuumeza hata kama ni mchungu!! Wazo linalotolewa kuwa watu waambiwe kuwa wamepangwa kwenye ajira sekta fulani halafu wakae wakisubiri kuitwa. Hilo ni sawa lakini linaweza kuibua makelele ya aina yake, na yanaweza kuwa makubwa zaidi!! Unaonaje mtu akakukaribisha mezani na una njaa, halafu ukakaa mezani kwa masaa sita kabla ya chakula kuletwa mezani!! Mbaya zaidi ukifia mezani wakati unasubiri chakula kitatokea kitu gani?

Nafahamu kuna watu hupenda kuambiwa maneno matamu hata kama hayo maneno hayana ukweli!! Wanasiasa hutumia ufahamu huo kudanganya watu ili tu watu wafurahi!! Tujifunze kuukabili ukweli ili tuwe katika nafasi ya kutafuta suluhisho!! Narudia tena, mchawi ni pesa na huwa haipatikani kwa wakati na kwa utimilifu kam,a ilivyotarajiwa. Tutafute suluhisho hapo ili pesa ipatikane yote na kwa wakati!! Suluhisho ni kukubali kuwa waadilifu na waaminifu kila mtu kwa nafasi yake!! Tuondokane na mawazo ya kutafuta kula rushwa, na kukwepa kulipa kodi!! Ukimwona mtu anakwepa kulipa kodi huyo ni sawa na jambazi!! TUKUBALI KUWA WAZALENDO.

Niombe radhi kwa wale watakaoona nimewakera kwa kuweka kipande kirefu kama sehemu ya mchango wangu kwenye kutoa elimu hii ya uraia!!

​
Anko kwan wewe unajishughulisha na nn?

Kwa madini haya wewe sio jobless kabisaaa😄😄😄.
 
Siyo fani zote za sayansi ni TGS E. Inategemea hiyo fani ameisoma kwa miaka mingapi chuo. Kwa mfano afisa kilimo, afisa mifugo, afisa samaki nk hizi zote ni fani za sayansi lakini wamesoma chuo kwa miaka mitatu, kwa hiyo wanaangukia kwenye TGS D1 - TGS D12: 765,000/= hadi 930,000/= kwa mwezi, na nyongeza yao ya mwaka ni Tsh 15,000/=.
TGS E ni kwa fani ambazo husomewa miaka 4 chuo kikuu kama vile wahandisi, wafamasia, wanasheria nk.​
Shukrani kwa kuzidi kutupatia nondo kiongozi. Hivi tofauti ya D1 na D12 ni nini? Yani naomba utufafanulie ili tuweze kuelewa zaidi.
 
Back
Top Bottom