HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hapa ndio mjue kuchelewa Placement sio swala la Psrs Bali ni serikali. Sasa hivi hakuna placement sababu mwaka mpya wa fedha. Placement ni beyond Psrs boundaries. Psrs wanapanga ila lini waajiriwa wapya waanze kazi hawawezi amua.
 
Kweli mkuu, PSRS ni waratibu TU na si vinginevyo. Muhitaji akiwa tayari wao pia wapo tayari muda wowote kumpatia watu. Mfano mzuri ni ule usaili wa bunge. Ndani ya muda mfupi plecement ikatoka.
 
Hivi wadau kwa wanaofahamu ikitokea usaili unahitaji let say watu 500 kwa mujibu wa tangazo la kazi linavyotaka kwa mantiki ya kwamba itabidi waite watu 1500 kwenye oral ili kufanya ratio ya nafasi moja kugombaniwa na watu watatu- 1/3 ambao ndio utaratibu wao

Swali langu ni kwamba kama watu 100 tu ndio waliopata alama 50 the rest labda 2000+ wakapata 40 kushuka huwa wanatumia mbinu gani kutimiza watu 400 waliobaki ili kutimiza akidi ya wasailiwa 500 Ili ratio yao ya 1/3 ikae sawa?
 
Hapo mchakato wa ajira utaendelea kwa hao wachache waliofaulu usaili, kisha tangazo la kazi litarudiwa Tena kwa umma wa watanzania ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi. Hakuna namna ya kudeal na waliopata chini ya 50 mkuu.
 
Yesuuu
 
Hapa ndio mjue kuchelewa Placement sio swala la Psrs Bali ni serikali. Sasa hivi hakuna placement sababu mwaka mpya wa fedha. Placement ni beyond Psrs boundaries. Psrs wanapanga ila lini waajiriwa wapya waanze kazi hawawezi amua.
Wakala mwingine wa psrs 😂😂😂 kwani wakitoa majina wakawaacha watu wasubirie kuanza kazi kama zile za February tra Kuna tatizo gani. Issue sio pesa wala nn ni uzembe wao Tu na kutafuta per Diem ili waonekane Wana kazi nying
Ukiangalia placement za LGA MDA zilivyotolewa nusunusu hadi watu wanapigiwa simu na halmashaur (kabla psrs hawajatoa majina kwenye website) wakaripoti sasa hapo utasema uzembe wa nani?
 
Sasa hivi watu wakienda vituoni watakufa njaa Account zimefungwa taasisi zinafunga mahesabu. Hakutakuwa na Hela za kujikimu mtaanza kulalamika Tena serikali haitujali
 
Umemuelewa uliyemjibu kweli ?

Ngoja nifanye uchambuzi kidogo:

Yeye: Majina ya waliopata ajira yawekwe hadharani (watu wajijue) hata kama hawataanza kazi sasa. Wasubiri taratibu wakijua kwamba wameshapata, waliokosa waendelee na maisha mengine.

Wewe: Akaunti kwa sasa zimefungwa, waliopata ajira wataendea kuteseka vituoni kwa kukosa pesa ya kujikimu.

Mchambuzi hadi napata kizunguzungu.
 
Hapa ndio mjue kuchelewa Placement sio swala la Psrs Bali ni serikali. Sasa hivi hakuna placement sababu mwaka mpya wa fedha. Placement ni beyond Psrs boundaries. Psrs wanapanga ila lini waajiriwa wapya waanze kazi hawawezi amua.
Tanzania tuna tatizo kubwa sana la kuwa na WATATUZI (Solvers/Fixers) wachache.

Watanzania wengi sana sio natural solvers.

Ngoja turudi kwenye hoja zako hapo juu.
Umesema kuchelewa kwa placement "sio kosa la PSRS bali ni kosa la serikali". Hii kitaalam inaitwa kurushiana mpira yaani "sio mimi, ni yule".

Hivi unafahamu kwamba mchakato wa ajira unapaswa kuwa well coordinated baina ya sehemu zote husika ? Yaani unakujaje hapa ku justify units kufanya kazi antagonistic ?

Kama hii ni sababu ambayo wewe unaikubali kwamba inatosha kuchelewesha placement, kesho na keshokutwa tukikupa nafasi kama mtumishi wa serikali, utaweza kweli kuleta suluhu za matatizo ya watu ?
Si utaendeleza hizi SIO MIMI, NI YULE wewe ?
 
Ukiwa mtumishi wa umma utaelewa ninachokisema. Wizara inapangiwa bajeti may be 700B lakini mwisho WA siku hadi mwaka unaisha wamepewa 400B. Hapo lazima mipango mingine ife.
Kuna mengi sana vijana hamyajui mnatakiwa mjifunze lakini nyinyi mnakuja kutoa lawama. Hao wenyewe ni waajiriwa tu. Swala la muhimu watoe MATOKEO ya Oral interview ila PLACEMENT ni swala la Fedha na bajeti.
 
Sema usemavyo na kinadharia unaweza kuwa uko sahihi. Lakini katika uhalisia mambo mara nyingine hayaendi kama ilivyotarajiwa!! Tutazunguka sana lakini mchawi hapa ni pesa!! Mara nyingi huwa hazipatikani kwa wakati kama ilivyotarajiwa!! Mipango huwa inatangulia halafu pesa zinakuja nyuma kuja kuwezesha utekelezaji wa mipango. Haiwezekani usubiri pesa zipatikane ndio upange!! Bunge linapopitisha bajeti kwa ajil;i ya utekelezaji wa mipango tarajiwa ya mwaka haina maana kuwa hizo pesa zipo, lakini inatarajiwa kuwa zitapatikana kutokana na vyanzo mbalimbali hasa MAKUSANYO YA KODI, hii ni pamoja na mipango ya kuajiri katika sekta m,balimbali!!

Sekta fulani ikiomba kibali cha kuajiri, ni kwa sababu imeweka fungu la kuajiri katika bajeti yake kwa mwaka husika na bajeti hiyo imeshapitishwa tayari bungeni. Wizara yenye dhamana ya kutoa kibali cha kuajiri ikijiridhisha kuwa anayeomba kuajiri analo fungu la ajira kwenye bajeti yake, hutoa hicho kibali cha kuajiri. Sekta husika ikishapata kibali hicho huwasiliana na WAKALA mwenye jukumu la kutangaza, kufanyisha usaili na kupanga waajiriwa KWA NIABA YA SEKTA INAYOAJIRI. Wakala huyo ni PSRS.

Inaweza ikatokea kuwa pesa iliyotarajiwa kwa ajili ya waajiriwa wapya aidha haijapatikana bado au imepatikana kiasi fulani na si kiasi chote. Kama haijapatikana yote watachukuliwa baadhi tu ya waajiriwa na wengine wabaki nwanasubiri. Kama haijapatikana kabisa maana yake ni kwamba watasubirishwa hadi ipatikane!! Makusanyo ya kodi hayako constant!! na kuna watu hukwepa kulipa kodi na athari yake ni hiyo!! Bado watanzania walio wengi huwa hawaoni umuhimu wa kulipa kodi. Ni mara ngapi umenunua bidhaa na hukupewa risiti ya EFD na wewe hukuona sababu ya kuidai hiyo risiti? Usipodai risiti unamwezesha mfanyabiashara kuiibia serikali mapato yake, na moja ya madhara yake ni haya ya kuchelewesha placement!!

Hakuna wizara hata moja ambayo hufanikiwa kupewa pesa yote iliyokuwa imeidhinishiwa kwenye bajeti yake kwa sababu hiyo pesa haikupatikana yote na hiyo iliyopatikana huenda haikupatikana kwa wakati uliotarajiwa! Hii ina maana kuwa kuna mipango kadhaa ambayo huwa imeshindikana kutekelezeka na kusubirishwa kwa wakati ujao. Ingia kwenye tovuti ya wizara yoyote usome hotuba ya bajeti yake. Huwa wanatoa mrejesho wa bajeti iliyopita na kueleza ilitekelezeka kwa asilimia ngapi!!

Huu ndio ukweli ambao tunalazimika kuumeza hata kama ni mchungu!! Wazo linalotolewa kuwa watu waambiwe kuwa wamepangwa kwenye ajira sekta fulani halafu wakae wakisubiri kuitwa. Hilo ni sawa lakini linaweza kuibua makelele ya aina yake, na yanaweza kuwa makubwa zaidi!! Unaonaje mtu akakukaribisha mezani na una njaa, halafu ukakaa mezani kwa masaa sita kabla ya chakula kuletwa mezani!! Mbaya zaidi ukifia mezani wakati unasubiri chakula kitatokea kitu gani?

Nafahamu kuna watu hupenda kuambiwa maneno matamu hata kama hayo maneno hayana ukweli!! Wanasiasa hutumia ufahamu huo kudanganya watu ili tu watu wafurahi!! Tujifunze kuukabili ukweli ili tuwe katika nafasi ya kutafuta suluhisho!! Narudia tena, mchawi ni pesa na huwa haipatikani kwa wakati na kwa utimilifu kam,a ilivyotarajiwa. Tutafute suluhisho hapo ili pesa ipatikane yote na kwa wakati!! Suluhisho ni kukubali kuwa waadilifu na waaminifu kila mtu kwa nafasi yake!! Tuondokane na mawazo ya kutafuta kula rushwa, na kukwepa kulipa kodi!! Ukimwona mtu anakwepa kulipa kodi huyo ni sawa na jambazi!! TUKUBALI KUWA WAZALENDO.

Niombe radhi kwa wale watakaoona nimewakera kwa kuweka kipande kirefu kama sehemu ya mchango wangu kwenye kutoa elimu hii ya uraia!!

​
 
NAKUPONGEZA SANA!!! Unajua hapa kuna watu wana maumivu sana ya kusubiri kwa muda mrefu!! Ila ukweli hata kama ni mchungu ni kwamba PLACEMENT ni suala la fedha!!

Kuna kijana mmoja alisema, kama hawana fedha kwa nini wanaitisha usaili? Jibu ni kwamba iko kwenye bajeti kwa matazamio kuwa pesa itapatikana!! Ikitokea haijapatikana inabidi tuelewe!! Hakuna wizara ambayo hufanikiwa kupewa fedha iliyopangiwa kwenye bajeti kwa asilimia 100. Hii ni kwa sababu serikali haijafanikiwa kukusanya pesa kutoka kwenye vyanzo vyake kwa asilimia 100!! Na chanzo kikubwa cha mapato ya serikali ni KODI!! Tuisaidie serikali kukusanya mapato yake kwa kudai risiti za EFD katika manunuzi tunayofanya!!​
 
Ukiwa mtumishi wa umma utaelewa ninachokisema. Wizara inapangiwa bajeti may be 700B lakini mwisho WA siku hadi mwaka unaisha wamepewa 400B. Hapo lazima mipango mingine ife.
Kuna mengi sana vijana hamyajui mnatakiwa mjifunze lakini nyinyi mnakuja kutoa lawama. Hao wenyewe ni waajiriwa tu. Swala la muhimu watoe MATOKEO ya Oral interview ila PLACEMENT ni swala la Fedha na bajeti.
Kama hakuna bajeti ya kutosha kuajiri, hautoi ajira. Very simple.

Sio unatoa kibali cha ajira wakati hauna uhakika wa fedha za kuzihudumia hizo ajira.

Hii ni basic understanding ya planning.

Shida ni kwamba watu wa serikalini kila kitu mnakiletea ugumu ionekane kwamba mambo hili haliwezekani.

At least tunawaelewa nyie mliopo serikalini muda mrefu mkiwa na mentality hiyo. Kitu kibaya ni kuwaaminisha wanaoingia sasa kwamba serikalini sio sehemu sahihi ya fikra mpya zenye mrengo wa kukwamua masuala.

Tunahitaji watu wanaoingia sasa waje na fikra mpya za kutatua pale tulipo kwama.

Cha kushangaza wazee wetu mnazidi KUKAZA, kuleta sababu laki moja kwanini mambo yaendelee kuwa hivi yalivyo.

Inadequate solvers.
 
Tofautisha kati ya bajeti na pesa!! Bajeti siyo pesa!! Bajeti ni kibali au idhini ya kutumia kiasi fulani cha pesa ili kukidhi mipango inayokusudiwa kutekelezwa. Kuwepo kwa bajeti haina maana pesa ipo, maana pesa inakuwepo tu wakati imeshakusanywa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Bajeti inatekelezeka tu kama pesa itakusanywa yote kama ilivyotarajiwa!! Hakuna anayesema mambo yaendelee hivi yalivyo. Ila ufumbuzi wake si mwepesi kama unavyofikiria, hasa kwenye jamii yetu ambapo watu hulipa kodi kwa kulazimishwa na kubanwa!! Mambo yatabadilika kama kila mtu ataona ni FAHARI kulipa kodi ili kuwezesha serikali kutimiza mipango yake!! Kila mtu aone ni aibu kukwepa kodi, ni aibu kutoa na kupokea rushwa!! Mpaka hili litakapowezekana ndipo itawezekana bajeti kupatikana kama ilivyopangwa na mipango kutekelezeka kama ilivyopangwa!! Vinginevyo tunataka tukaribishane mezani kula ugali wakati hata hayo mahindi ya kusagia huo unga wa ugali hayajavunwa bado yako shambani!! Je ukikaribishwa kwa staili hiyo utafurahi?​
 
Hapa ndio mjue kuchelewa Placement sio swala la Psrs Bali ni serikali. Sasa hivi hakuna placement sababu mwaka mpya wa fedha. Placement ni beyond Psrs boundaries. Psrs wanapanga ila lini waajiriwa wapya waanze kazi hawawezi amua.
Kuna kauli N/w Kikwete ameongea Bungeni kunamarekebisho kidogo wanafanya Utumishi ....
 
Sema usemavyo na kinadharia unaweza kuwa uko sahihi. Lakini katika uhalisia mambo mara nyingine hayaendi kama ilivyotarajiwa!! Tutazunguka sana lakini mchawi hapa ni pesa!! Mara nyingi huwa hazipatikani kwa wakati kama ilivyotarajiwa!! Mipango huwa inatangulia halafu pesa zinakuja nyuma kuja kuwezesha utekelezaji wa mipango. Haiwezekani usubiri pesa zipatikane ndio upange!! Bunge linapopitisha bajeti kwa ajil;i ya utekelezaji wa mipango tarajiwa ya mwaka haina maana kuwa hizo pesa zipo, lakini inatarajiwa kuwa zitapatikana kutokana na vyanzo mbalimbali hasa MAKUSANYO YA KODI, hii ni pamoja na mipango ya kuajiri katika sekta m,balimbali!!

Sekta fulani ikiomba kibali cha kuajiri, ni kwa sababu imeweka fungu la kuajiri katika bajeti yake kwa mwaka husika na bajeti hiyo imeshapitishwa tayari bungeni. Wizara yenye dhamana ya kutoa kibali cha kuajiri ikijiridhisha kuwa anayeomba kuajiri analo fungu la ajira kwenye bajeti yake, hutoa hicho kibali cha kuajiri. Sekta husika ikishapata kibali hicho huwasiliana na WAKALA mwenye jukumu la kutangaza, kufanyisha usaili na kupanga waajiriwa KWA NIABA YA SEKTA INAYOAJIRI. Wakala huyo ni PSRS.

Inaweza ikatokea kuwa pesa iliyotarajiwa kwa ajili ya waajiriwa wapya aidha haijapatikana bado au imepatikana kiasi fulani na si kiasi chote. Kama haijapatikana yote watachukuliwa baadhi tu ya waajiriwa na wengine wabaki nwanasubiri. Kama haijapatikana kabisa maana yake ni kwamba watasubirishwa hadi ipatikane!! Makusanyo ya kodi hayako constant!! na kuna watu hukwepa kulipa kodi na athari yake ni hiyo!! Bado watanzania walio wengi huwa hawaoni umuhimu wa kulipa kodi. Ni mara ngapi umenunua bidhaa na hukupewa risiti ya EFD na wewe hukuona sababu ya kuidai hiyo risiti? Usipodai risiti unamwezesha mfanyabiashara kuiibia serikali mapato yake, na moja ya madhara yake ni haya ya kuchelewesha placement!!

Hakuna wizara hata moja ambayo hufanikiwa kupewa pesa yote iliyokuwa imeidhinishiwa kwenye bajeti yake kwa sababu hiyo pesa haikupatikana yote na hiyo iliyopatikana huenda haikupatikana kwa wakati uliotarajiwa! Hii ina maana kuwa kuna mipango kadhaa ambayo huwa imeshindikana kutekelezeka na kusubirishwa kwa wakati ujao. Ingia kwenye tovuti ya wizara yoyote usome hotuba ya bajeti yake. Huwa wanatoa mrejesho wa bajeti iliyopita na kueleza ilitekelezeka kwa asilimia ngapi!!

Huu ndio ukweli ambao tunalazimika kuumeza hata kama ni mchungu!! Wazo linalotolewa kuwa watu waambiwe kuwa wamepangwa kwenye ajira sekta fulani halafu wakae wakisubiri kuitwa. Hilo ni sawa lakini linaweza kuibua makelele ya aina yake, na yanaweza kuwa makubwa zaidi!! Unaonaje mtu akakukaribisha mezani na una njaa, halafu ukakaa mezani kwa masaa sita kabla ya chakula kuletwa mezani!! Mbaya zaidi ukifia mezani wakati unasubiri chakula kitatokea kitu gani?

Nafahamu kuna watu hupenda kuambiwa maneno matamu hata kama hayo maneno hayana ukweli!! Wanasiasa hutumia ufahamu huo kudanganya watu ili tu watu wafurahi!! Tujifunze kuukabili ukweli ili tuwe katika nafasi ya kutafuta suluhisho!! Narudia tena, mchawi ni pesa na huwa haipatikani kwa wakati na kwa utimilifu kam,a ilivyotarajiwa. Tutafute suluhisho hapo ili pesa ipatikane yote na kwa wakati!! Suluhisho ni kukubali kuwa waadilifu na waaminifu kila mtu kwa nafasi yake!! Tuondokane na mawazo ya kutafuta kula rushwa, na kukwepa kulipa kodi!! Ukimwona mtu anakwepa kulipa kodi huyo ni sawa na jambazi!! TUKUBALI KUWA WAZALENDO.

Niombe radhi kwa wale watakaoona nimewakera kwa kuweka kipande kirefu kama sehemu ya mchango wangu kwenye kutoa elimu hii ya uraia!!

​
Huo ndio ukweli wenyewe, unajua shida ni kwamba walio ndani ya mfumo wanalijua jambo hili vizuri ila kwa ambao wapo nje ya mfumo ni ngumu kulijua jambo hili, ushauri wangu kwa vijana ni kuwa na uvumilivu tu Mungu ni mwema wakati ukifika wa kubarikiwa kwa upande wa kazi mambo yote yatakuwa sawa. Serikali mambo yake ndio hivyohivyo mdogomdogo, mambo mengi yanahitaji upatikanaji wa pesa kusonga mbele.
 
Back
Top Bottom