HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Sema usemavyo na kinadharia unaweza kuwa uko sahihi. Lakini katika uhalisia mambo mara nyingine hayaendi kama ilivyotarajiwa!! Tutazunguka sana lakini mchawi hapa ni pesa!! Mara nyingi huwa hazipatikani kwa wakati kama ilivyotarajiwa!! Mipango huwa inatangulia halafu pesa zinakuja nyuma kuja kuwezesha utekelezaji wa mipango. Haiwezekani usubiri pesa zipatikane ndio upange!! Bunge linapopitisha bajeti kwa ajil;i ya utekelezaji wa mipango tarajiwa ya mwaka haina maana kuwa hizo pesa zipo, lakini inatarajiwa kuwa zitapatikana kutokana na vyanzo mbalimbali hasa MAKUSANYO YA KODI, hii ni pamoja na mipango ya kuajiri katika sekta m,balimbali!!

Sekta fulani ikiomba kibali cha kuajiri, ni kwa sababu imeweka fungu la kuajiri katika bajeti yake kwa mwaka husika na bajeti hiyo imeshapitishwa tayari bungeni. Wizara yenye dhamana ya kutoa kibali cha kuajiri ikijiridhisha kuwa anayeomba kuajiri analo fungu la ajira kwenye bajeti yake, hutoa hicho kibali cha kuajiri. Sekta husika ikishapata kibali hicho huwasiliana na WAKALA mwenye jukumu la kutangaza, kufanyisha usaili na kupanga waajiriwa KWA NIABA YA SEKTA INAYOAJIRI. Wakala huyo ni PSRS.

Inaweza ikatokea kuwa pesa iliyotarajiwa kwa ajili ya waajiriwa wapya aidha haijapatikana bado au imepatikana kiasi fulani na si kiasi chote. Kama haijapatikana yote watachukuliwa baadhi tu ya waajiriwa na wengine wabaki nwanasubiri. Kama haijapatikana kabisa maana yake ni kwamba watasubirishwa hadi ipatikane!! Makusanyo ya kodi hayako constant!! na kuna watu hukwepa kulipa kodi na athari yake ni hiyo!! Bado watanzania walio wengi huwa hawaoni umuhimu wa kulipa kodi. Ni mara ngapi umenunua bidhaa na hukupewa risiti ya EFD na wewe hukuona sababu ya kuidai hiyo risiti? Usipodai risiti unamwezesha mfanyabiashara kuiibia serikali mapato yake, na moja ya madhara yake ni haya ya kuchelewesha placement!!

Hakuna wizara hata moja ambayo hufanikiwa kupewa pesa yote iliyokuwa imeidhinishiwa kwenye bajeti yake kwa sababu hiyo pesa haikupatikana yote na hiyo iliyopatikana huenda haikupatikana kwa wakati uliotarajiwa! Hii ina maana kuwa kuna mipango kadhaa ambayo huwa imeshindikana kutekelezeka na kusubirishwa kwa wakati ujao. Ingia kwenye tovuti ya wizara yoyote usome hotuba ya bajeti yake. Huwa wanatoa mrejesho wa bajeti iliyopita na kueleza ilitekelezeka kwa asilimia ngapi!!

Huu ndio ukweli ambao tunalazimika kuumeza hata kama ni mchungu!! Wazo linalotolewa kuwa watu waambiwe kuwa wamepangwa kwenye ajira sekta fulani halafu wakae wakisubiri kuitwa. Hilo ni sawa lakini linaweza kuibua makelele ya aina yake, na yanaweza kuwa makubwa zaidi!! Unaonaje mtu akakukaribisha mezani na una njaa, halafu ukakaa mezani kwa masaa sita kabla ya chakula kuletwa mezani!! Mbaya zaidi ukifia mezani wakati unasubiri chakula kitatokea kitu gani?

Nafahamu kuna watu hupenda kuambiwa maneno matamu hata kama hayo maneno hayana ukweli!! Wanasiasa hutumia ufahamu huo kudanganya watu ili tu watu wafurahi!! Tujifunze kuukabili ukweli ili tuwe katika nafasi ya kutafuta suluhisho!! Narudia tena, mchawi ni pesa na huwa haipatikani kwa wakati na kwa utimilifu kam,a ilivyotarajiwa. Tutafute suluhisho hapo ili pesa ipatikane yote na kwa wakati!! Suluhisho ni kukubali kuwa waadilifu na waaminifu kila mtu kwa nafasi yake!! Tuondokane na mawazo ya kutafuta kula rushwa, na kukwepa kulipa kodi!! Ukimwona mtu anakwepa kulipa kodi huyo ni sawa na jambazi!! TUKUBALI KUWA WAZALENDO.

Niombe radhi kwa wale watakaoona nimewakera kwa kuweka kipande kirefu kama sehemu ya mchango wangu kwenye kutoa elimu hii ya uraia!!

​
Wakala mwingine wa psrs unatutoa kweli reli issue sio pesa wala nn ni uzembe na kutafuta per Diem kwa hao watumishi wa psrs. Mbona halmashaur nyingine waliwapigia watu wakaripoti kazi za LGA MDA kabla psrs hawajatoa placement
Eti watu walipe Kodi kwani hawalipi mm jobless unanishaur nilipe Kodi kwa kazi gani uliyonipa au biashara gan nafanya kama hata machinga Tu serikali haituthamini
Embu tuondolee upuuz kwann psrs wanachelewa kutoa placement ndio swala la msingi hapa.
Matokeo ya oral ni haki yetu
 
Ukiwa mtumishi wa umma utaelewa ninachokisema. Wizara inapangiwa bajeti may be 700B lakini mwisho WA siku hadi mwaka unaisha wamepewa 400B. Hapo lazima mipango mingine ife.
Kuna mengi sana vijana hamyajui mnatakiwa mjifunze lakini nyinyi mnakuja kutoa lawama. Hao wenyewe ni waajiriwa tu. Swala la muhimu watoe MATOKEO ya Oral interview ila PLACEMENT ni swala la Fedha na bajeti.
Kutoa majina ya waliofaulu oral nayo inahitaji bajeti 👉🐸
 
Nawaelewa vizuri sana mnaojaribu kuliweka vzuri hili suala la placement jinsi linavyohusiana na masuala ya budget & pesa, binafsi ata mm naamin iko ivo.

Lakin ntaenda tofauti kidogo. Tukiachana na suala la placement yan "kupangia watu vituo vya kazi".

Wakati wanasubiri masuala ya fedha yakae sawa ili wapangie watu vituo,
Kwann wasitoe matokeo ya oral ikajulikana mapema wanaosubiri placement(waliopita), waliongia database na waliopata below 50%.

Unajua watu tuna depression iliyochangiwa na matumaini hewa tuliyoyajenga, unasubiri ktu ambacho hujui kam kipo ama hakipo, it's not easy. Watu wanashindwa kufanya mamb mengne sababu ya kusubiri kitu kisicho fahamika hatima yake.

Imagine 3 days after oral, matokeo yanatoka ata kma utakua umekosa n maumivu ya mda mfupi una move on na unaendelea na mishe zingne.
Imagine tena 3 days after oral, matokeo yanatoka na umepita direct. Depression itoke wapi as long as una uhakika ushaingia kwnye system?

Kuna mdau katolea mfano scenario ya kukaribishwa chakula mezan afu usubiri chakula kwa mda mrefu. Binafsi ntakisubiri tu as long as nshaona dalili huko jikoni(uhakika) wala hutoniona huko nje(dodoma) naminyana kutafuta kingne(usaili).

"Kidogo cha ndani n bora kuliko kikubwa cha nje"
"Something is better than nothing"

Ujue kuna saili watu wanaenda first priority yao ikiwa ni atleast aingie data base especially hiz post chache chache. Sasa mm kma niliwahi piga oral huko nyuma na matokeo yalitoka niko above 50%, obviously aina iyo ya saili siwez enda,

Watoe matokeo ya oral tupunguziane unnecessary costs.
Hiyo ndo point yangu, na sijaanza kuiimba leo.
Nishaiandikia na Uzi mara tu baada ya kujoin JF heading
"Suruhisho la kwanini utumishi wanachelewa kutoa placements"
 
Hilo la kutoa matokeo ya oral tuko pamoja!! Ila ujue wanaofaulu ni wengi wakati nafasi za placement ni chache!! Wakati tukidai matokeo ya oral tujiandae pia kisaikolojia kuona mtu amepata marks 90 na akakosa placement kwa sababu nafasi kapewa aliyepata 91, wote wengine waliofanya oral wana marks zaidi ya 80 kwa mfano. Lakini pia tujiandae kuona mtu amepata marks 58 na kupata placement kwa sababu ndiye aliyepata alama nyingi kwenye oral yao!. Na ukifaulu bila placement unakuwa kwenye database ambako hakuna guarantee/uhakika wa kupata placement baada ya kusubiri kwa muda fulani!! Na data base pia nadhani ina expiry date!! Fikiria mtu ambaye anajua alipata marks 90 halafu asipate placement hadi expiry date ya data base yake ikafika atajisikiaje? Hiyo naona itaibua uzi mwingine "kwa nini utumishi wanaweka watu kwenye data base kwa muda mrefu bila kuwapa ajira hadi data base ina-expire?" Nadhani kukwepa kuwapa watu matumaini yasiyokuwa na uhakika ndiyo sababu iliyopelekea psrs isitoe matokeo ya oral, I may be wrong, but I suppose so!!.​
 
Sorry to say this but jamaa unatetea UJINGA
 
Hilo la kutoa matokeo ya oral ni sawa, lakini ujue kuwa kufaulu oral si kupata placement!! Wanaofaulu oral wanaweza kuwa wengi lakini nafasi za placement ni chache. Hii ni kwa sababu wanaoitwa kwenye oral ni wengi kuliko nafasi zilizopo. Ukizingatia kuwa hawa walifanya vizuri written na kuna uwezekano mkubwa pia wengi wao wakafanya oral vizuri. Labda tuseme hivi watoe pdf ya oral halafu wapige mstari waliopangiwa placement juu ya mstari na walio chini ya mstari waishi kwa matumaini kwa mpango wa data base just in case!!​
 
Ujinga upi natetea? Tuko pamoja watoe matokeo ya oral!! Ila kwa angalizo kuwa kufaulu oral si kupata placement maana wanaofaulu oral wanaweza kuwa ni wengi kuliko idadi ya placement inayotakiwa!! Hii ni kwa sababu wanaoitwa kwenye oral ni wengi kuliko idadi ya placement!!
 
Comment yako ya juu ilionesha kwamba hiki kitu hakiwezekani na ni bora tubaki kwenye mfumo ulipo.

Lakini sasa naona umeona kwamba inawezekana, swala ni namna gani bora ya kufanya.

Kama ilivyo kwenye written kuna watu wanafika marks 50 ila unakuta wanaanza kuchukuliwa wenye 65, vivyo hivyo kwenye oral kama nafasi zilikua 5 wachukuliwe wenye marks za juu, wenye 50 ionekane wapo database, below 50 waendelee na maisha mengine.

Mfumo wa sasa hivi upo kama kuku aliyekatwa kichwa, mtu hujui umepata placememt au umefaulu oral upo database au umefeli mazima
 
Hilo la kutoa matokeo ya oral tuko pamoja!! Ila ujue wanaofaulu ni wengi wakati nafasi za placement ni chache!! Wakati tukidai matokeo ya oral tujiandae pia kisaikolojia kuona mtu amepata marks 90 na akakosa placement kwa sababu nafasi kapewa aliyepata 91, wote wengine waliofanya oral wana marks zaidi ya 80 kwa mfano. Lakini pia tujiandae kuona mtu amepata marks 58 na kupata placement kwa sababu ndiye aliyepata alama nyingi kwenye oral yao!. Na ukifaulu bila placement unakuwa kwenye database ambako hakuna guarantee/uhakika wa kupata placement baada ya kusubiri kwa muda fulani!! Na data base pia nadhani ina expiry date!! Fikiria mtu ambaye anajua alipata marks 90 halafu asipate placement hadi expiry date ya data base yake ikafika atajisikiaje? Hiyo naona itaibua uzi mwingine "kwa nini utumishi wanaweka watu kwenye data base kwa muda mrefu bila kuwapa ajira hadi data base ina-expire?" Nadhani kukwepa kuwapa watu matumaini yasiyokuwa na uhakika ndiyo sababu iliyopelekea psrs isitoe matokeo ya oral, I may be wrong, but I suppose so!!.​
Unatukosea sana na wewe kazi yako ni kutetea psrs mda mrefu nakufatilia na isitoshe huwa unajaribu kututoa kwenye reli hadi nimeccomment nimechoshwa na promotion zako unazowapa psrs.
Kwani oral wanafaulu wote kanuni si inasema nafasi 1 inagombewa na watu 3, then tuje kwenye oral kwani ni wote watatu wanafanya vizuri? Again tuje kwenye matangazo ya kazi mbona wanarudiarudia kutangaza post daily na kufanyisha usahili kila mara mfano post za accountant au hata tu uchumi ni kwamba database haina watu 🙄🙄🙄 alafu ukiangalia wanafanya hvy kutafuta posho bila kujali unawaumiza wangapi.
Wanashindwa nini kwenye oral kupitisha wawili kama huwa wanavyoongeza pass marks kwenye written interview
Kwanini wanatangaza kazi post zilezile wakat kanuni zao zinasema mpaka wawapangie wa database kazi ndio watangaze tena?

Psrs ni jipu na Wana makandokando mengi sana tungeungana tukapaza sauti mama angetusikia na kulifatilia hili
 
Hilo la kutoa matokeo ya oral ni sawa, lakini ujue kuwa kufaulu oral si kupata placement!! Wanaofaulu oral wanaweza kuwa wengi lakini nafasi za placement ni chache. Hii ni kwa sababu wanaoitwa kwenye oral ni wengi kuliko nafasi zilizopo. Ukizingatia kuwa hawa walifanya vizuri written na kuna uwezekano mkubwa pia wengi wao wakafanya oral vizuri. Labda tuseme hivi watoe pdf ya oral halafu wapige mstari waliopangiwa placement juu ya mstari na walio chini ya mstari waishi kwa matumaini kwa mpango wa data base just in case!!​
Psrs ndio wanasababisha matatizo yote haya kwa sababu zifuatazo;
1 wanatangaza kazi kila mara kwa post ambazo wengi wameshafanya usahili (multiple advertisement in the same post e.g accountant etc)
2. Hawatumii database kama kanuni zao zinavyowaelekeza kwamba wasitangaze kazi hadi watu wa database waishe
3. Hawafuati kanuni ya post 1 kugombewa na watu 3 oral
4.
Unaweza ukaongezea zingine
 
Hilo la kutoa matokeo ya oral tuko pamoja!! Ila ujue wanaofaulu ni wengi wakati nafasi za placement ni chache!! Wakati tukidai matokeo ya oral tujiandae pia kisaikolojia kuona mtu amepata marks 90 na akakosa placement kwa sababu nafasi kapewa aliyepata 91, wote wengine waliofanya oral wana marks zaidi ya 80 kwa mfano. Lakini pia tujiandae kuona mtu amepata marks 58 na kupata placement kwa sababu ndiye aliyepata alama nyingi kwenye oral yao!. Na ukifaulu bila placement unakuwa kwenye database ambako hakuna guarantee/uhakika wa kupata placement baada ya kusubiri kwa muda fulani!! Na data base pia nadhani ina expiry date!! Fikiria mtu ambaye anajua alipata marks 90 halafu asipate placement hadi expiry date ya data base yake ikafika atajisikiaje? Hiyo naona itaibua uzi mwingine "kwa nini utumishi wanaweka watu kwenye data base kwa muda mrefu bila kuwapa ajira hadi data base ina-expire?" Nadhani kukwepa kuwapa watu matumaini yasiyokuwa na uhakika ndiyo sababu iliyopelekea psrs isitoe matokeo ya oral, I may be wrong, but I suppose so!!.​
Wanaofaulu ni wengi? uliyaona wapi hayo matokeo bro? M nadhan kwa huu mfumo wao, wao pekee ndo wanajua waliofaulu km n wengi au lah, mim na wew hatujui. Any way hii isiwe case.

umesema kutokutoa matokeo ya oral ina tupunguzia matumaini.. huoni kma ukiniambia nimepata 40% utakua umenisaidia niendelee na mishe zingne otherwise ntaendelea kujenga matumaini ya huenda bado nimo huku mishe zmesimama kumbe niko na 40% ata huko data base sipo. Na ukiniambia nmepata 52% utakua unanipungizia unnecessary cost za kuhudhuria zile saili ambazo first priority yangu n atleast kuingia data base tu.

Hili la mda kuisha mtu yuko data base tunalijua lipo, sio geni na wala halitoanza baada ya kuadopt mfumo wa kutoa matokeo ya oral.. binafsi niko tayari kwa hiyo changamoto.
Kikubwa tu wanimbie kama nmezingua ama nmefaulu.
Nahitaji kujitathimini pia.

All in all kila kitu kina faida na hasara zake.. lakini kwa haraka haraka unaona tu faida za kutoa matokeo ya oral ni nyingi san kuliko hasara. Faida za kutokutoa matokeo n chache mno..
 
Pia wakawa organized na kupunguza multiple advertisement mbona database watu watatoka faster nakumbuka ilivyoanza psrs walikua wanazingatia sana database, hamna matangazo ya kazi pasipo mpangilio mzuri kama wanavyofanya sasa rejea kwenye archives utaona.
Lakini siku hizi wanachojali ni posho ziwe nying na kuitisha sahili kila wiki.
Let say bajeti imepitishwa juzi na wamepata vibali vya kuajiri kiasi Fulani. Hapo kabisa unajua na kuelewa mwaka huu wa fedha tunahitaji wahasibu kadhaa na database tunao baadh basi unatakiwa kuwapangia waliopo database kazi then nafasi zinazobaki ndio utangaze lakin sidhani kama wanazingatia Hilo.

Na kigezo cha kujidai sijui taasis X haitaki watu wa database ni cha uongo na kijinga sababu Sheria ndio imesema hivyo. Je ungewapelekea watumishi hao hao wa database tuone kama wangekataa huoni ni wanaitisha usahili ili kutafuta posho?
Cha ajabu walewale waliopo database ndio haohao wanarud kufanya tena usahili na ajabu unakuta mtu amefaulu oral zaid ya 1 na anapata double placement alafu anaenda 1 ile ambayo hajaripoti mnaitangaza tena 😂😂😂 Yan kuwatesa tu jobless
 
Back
Top Bottom