Huwa nakusomasoma unavyoandika ila leo mkuu umepuyanga,Mimi sikuomba TRA ila kuwalaumu unawaonea sana,idadi ya waombaji automaticaly ni kubwa mnooo,sasa hata mwezi haujaisha unalaumu hukumbuki kuwa hizo za Tra mwaka jana watu wameomba mwezi wa nne wakaitwa usaili mwezi wa 12 au ndio kujisahaulisha??au hujui huko utumishi kuna watu wana received nyingine miaka miwili na nyingine hadi miaka mitatu,tusiwalaumu bure kwa kitu ambacho hakihitaji lawama,unawatetea utumishi ilihali kuna watu wamefanya interview mwezi wa kwanza mpaka leo hamna placement na mmetulia,vingine fikiria kabla ya kuandika mkuu na sio kutoa lawama,tatizo la humu tulishatofautiana mawazo kwa baadhi yenu kuona kila kinachofanywa na utumishi ni sawa,tungekuwa pamoja kama uzi ulivyoanzishwa basi haya mambo yansingekuwepo maana badala ya kuungana kusema madhaifu yao tunakuwa tunaletewa ajenda mfu humu mara mtu anakuja kuzungumzia mshahara,mara marupurupu,mara njia za kupata hela kazini,mara hii inakuwa hv...leongo ni kupoteza mantiki ya uzi.
Kuna watu wakilamba asali wanaleta mada za hovyo humu sasa mtu anakuja kuuliza mshahara humu wakati anajua humu kwa wasaka asali maana yake nn,unakuta mtu analalamika makato wakati kuna mtu humu buku la vocha kwake ni zoezi na anauhitaji wa hiyo kazi na makato yake.leo mtu anakuja kuwasema TRA kuwa wamechelewa ilihali taasisi anayoitetea haijakamilisha michakato na ndio kiini cha kuundwa huu uzi