Wanjax jr
JF-Expert Member
- Jun 4, 2020
- 492
- 1,265
Kabla ya pidiefu status inasemaje ndg ,,??[emoji1][emoji1]au mwenye flash ya PDF yuko likizo..
Kabla ya pidiefu status inasemaje ndg ,,??[emoji1][emoji1]au mwenye flash ya PDF yuko likizo..
Hahahaha itakua alijisahau akaformat kwahiyo wanaandaa mkeka upya.Duuh sema jamaa anayekaa na flash ya Mapdf sijui huwa anajisikiaje akipita humu😂😂😂
Kwa upande wangu ipo Selected for Oral both App na WebKabla ya pidiefu status inasemaje ndg ,,??[emoji1][emoji1]
Ajira zilikuwa za mwaka wa fedha 21/22 lkn now imekuwa zinasuburi mwaka wa fedha 23/24..😂😂😂nchi ngumu sana hii
Unaweza ukaliaAjira zilikuwa za mwaka wa fedha 21/22 lkn now imekuwa zinasuburi mwaka wa fedha 23/24..😂😂😂nchi ngumu sana hii
Hapana.Hivi idadi iliyokuwa inatakiwa na MDA & LGA haijafikiwa bado? Isije ikawa idadi ilishafika ndio maana hawachangamkii tena kutoa mkeka.
Maana yake unaweza kuajiriwa sehemu yoyote ile kati ya LGA au MDA.Hivi mwajiri akiwa MDAs & LGAs inamaanisha utapata halmashauri tu au mkoani au na wizarani .... mwenye kufahamu ufafanuzi kidgo nielewe sijui hapa
Ok ok nmekusoma kakaMaana yake unaweza kuajiriwa sehemu yoyote ile kati ya LGA au MDA.
LGA = (Halmashauri za wilaya, miji, Manispaa, Majiji au sekretarieti za mikoa).
MDA = (Wizarani, wakala, idara na taasisi mbalimbali za serikali zinazojitegemea).
Kwahiyo unaweza kuajiriwa sehemu yoyote ile kati ya maeneo yaliyotajwa hapo juu.
Unaongea kwa nadharia, mimi nakupa hali halisi!! Agency fee hukatwa kwa makubaliano na si kwa lazima!! Ni lazima pande zote zinazohusika zikae kwenye majadiliano na zikubaliane asilimia ya kukatwa!! Sheria mama ni katiba ya nchi!! Mtanzania halazimiki kujiunga na chama chochote cha hiari!! Vyama vya wafanyakazi ni vyama vya hiari!! Mimi wakati bado ni mtumishi wa umma (kwa sasa nimeshastaafu) baada ya kuuelewa ukweli, nilimwandikia barua mwajiri asimamishe makato mara moja na chama cha wafanyakazi nikakipa nakala tu. Nilimtaka mwajiri anieleze kwa nini aliamua kunikata bila ridhaa yangu kinyume na taratibu zinavyotaka!! Makato yalisimama na sikukatwa tena mpaka nikastaafu. Mke wangu bado ni mtumishi wa umma hadi sasa, naye alipoona wanapigwa changa la macho naye aliamua KUJITOA kwenye chama cha wafanyakazi TUGHE ambako alikuwa mwanachama, na akasimamisha makato hadi leo.Sheria ya ajira na mahusiano kazini itafute. Kifungu cha 72. Mwajiri anaweza kukata Agency fee Kwa mwajiriwa asiyemwanachama wa chama chochote bila ya idhini yake.
Kwahiyo uwe na chama usiwe na chama wakiamua wanakukanda tu 2%
Nimekuaminia, uko vizuri!! Hii inaleta matumaini kwa wanaosubiri.Hapana.
Kuna baadhi ya kada bado hazijatimiza idadi ya waliotangazwa kuhitajika, zingine bado hawajaitwa kabisa.
Nitatoa mifano ambayo nina uhakika nayo, kama kuna mengine wadau wataongezea.
1. Afisa Uvuvi II zilitangazwa nafasi 100, hadi mkeka wa mwisho (May 24, 2023) wameita watu 41 (Tena hawa wote ni LGA, hakuna hata mmoja wa MDA). Kimahesabu ni kwamba bado watu 59.
2. Afisa ufugaji viumbe maji (Aquaculture officer) ilitangazwa nafasi 1, hadi sasa tunavyoongea bado hawajaita mtu.
3. Mteknolojia samaki, zilitangazwa nafasi 2, hadi sasa hajaitwa hata mmoja.
4. Afisa mifugo msaidizi (livestock field officer) zilitangazwa nafasi 360, hadi sasa wameitwa kazini watu "takribani" watu 340 (wote LGA).
5. Wengine wataongezea....
Kumbe hiyo nafasi moja ya aquaculture officer II bado haijajazwa hadi leo!! Kuna mtu namfahamu alikuwa ameitwa kwenye usajili wa hiyo nafasi lakini akiwa ameitwa pia kwenye nafasi za Fisheries Officer II. Akaamua asiende kufanya usaili wa aquaculture officer na kusubiri wa fisheries officer maana hakuwa na pesa za kukaa zaidi huko Dodoma walikokuwa wanafanyia usaili. Naona alipiga mahesabu vizuri maana tunavyozungumza alisharamba asali tayari kwenye hiyo fisheries Officer II.Hapana.
Kuna baadhi ya kada bado hazijatimiza idadi ya waliotangazwa kuhitajika, zingine bado hawajaitwa kabisa.
Nitatoa mifano ambayo nina uhakika nayo, kama kuna mengine wadau wataongezea.
1. Afisa Uvuvi II zilitangazwa nafasi 100, hadi mkeka wa mwisho (May 24, 2023) wameita watu 41 (Tena hawa wote ni LGA, hakuna hata mmoja wa MDA). Kimahesabu ni kwamba bado watu 59.
2. Afisa ufugaji viumbe maji (Aquaculture officer) ilitangazwa nafasi 1, hadi sasa tunavyoongea bado hawajaita mtu.
3. Mteknolojia samaki, zilitangazwa nafasi 2, hadi sasa hajaitwa hata mmoja.
4. Afisa mifugo msaidizi (livestock field officer) zilitangazwa nafasi 360, hadi sasa wameitwa kazini watu "takribani" watu 340 (wote LGA).
5. Wengine wataongezea....
Hongera sana kwake, alifanya maamuzi ya busara sana na hakika yamemlipa.Kumbe hiyo nafasi moja ya aquaculture officer II bado haijajazwa hadi leo!! Kuna mtu namfahamu alikuwa ameitwa kwenye usajili wa hiyo nafasi lakini akiwa ameitwa pia kwenye nafasi za Fisheries Officer II. Akaamua asiende kufanya usaili wa aquaculture officer na kusubiri wa fisheries officer maana hakuwa na pesa za kukaa zaidi huko Dodoma walikokuwa wanafanyia usaili. Naona alipiga mahesabu vizuri maana tunavyozungumza alisharamba asali tayari kwenye hiyo fisheries Officer II.
72 (4) Bila kujali masharti ya sheria yoyote au mkataba mwajiriUnaongea kwa nadharia, mimi nakupa hali halisi!! Agency fee hukatwa kwa makubaliano na si kwa lazima!! Ni lazima pande zote zinazohusika zikae kwenye majadiliano na zikubaliane asilimia ya kukatwa!! Sheria mama ni katiba ya nchi!! Mtanzania halazimiki kujiunga na chama chochote cha hiari!! Vyama vya wafanyakazi ni vyama vya hiari!! Mimi wakati bado ni mtumishi wa umma (kwa sasa nimeshastaafu) baada ya kuuelewa ukweli, nilimwandikia barua mwajiri asimamishe makato mara moja na chama cha wafanyakazi nikakipa nakala tu. Nilimtaka mwajiri anieleze kwa nini aliamua kunikata bila ridhaa yangu kinyume na taratibu zinavyotaka!! Makato yalisimama na sikukatwa tena mpaka nikastaafu. Mke wangu bado ni mtumishi wa umma hadi sasa, naye alipoona wanapigwa changa la macho naye aliamua KUJITOA kwenye chama cha wafanyakazi TUGHE ambako alikuwa mwanachama, na akasimamisha makato hadi leo.
Ukweli ni kwamba hata kama wewe ni mwanachama, lakini unaweza kuamua kusitisha huo uanachama. Kwenye vyama vya hiari una haki ya kujiunga na una haki pia ya kujitoa!! Lakini pia unaweza kubadili cham,a cha wafanyakazi kwa kadri utakavyotaka. Ukweli ni kwamba hakuna mwajiri anayeruhusiwa kukata pesa ya mtumishi yeyote bila idhini ya MAANDISHI toka kwa mwajiriwa!! Mwanzoni walitutisha na hiyo agency fee lakini mwishowe tukapata elimu utaratibu wa hiyo fee kisheria!! si lazim,a ni makubaliano, na ambapo mnakubaliana pia kiwango cha hiyo agency fee!! Lakini hata baada ya kukubaliana na hiyo agency fee, mwajiri hawezi kuanza makato kabla hajaruhusiwa kufanya hivyo kwa MAANDISHI na mwajiriwa!!
Unasema nini na unakataa nini!! Hapo unazungumzia wafanyakazi walioshiriki maongezi na chama cha wafanyakazi chini ya "duka la uwakala" na si vinginevyo!! Kama makubaliano ya duka la uwakala hayajafanyika na mwajiriwa kuridhia kwa maandishi kuruhusu makato hayo, mwajiri hana uhalali wa kukata hiyo fedha. Mimi ninayezungumza nilikataa na makato yakasitishwa!! bNinaongea kwa uzoefu!72 (4) Bila kujali masharti ya sheria yoyote au mkataba mwajiri
anaweza kukata ada ya uwakala chini ya makubaliano ya duka la
uwakala linalofuata masharti ya kifungu hiki kutoka kwenye ujira wa
mfanyakazi bila ridhaa ya mfanyakazi huyo.
Mazungumzo ya duka la uwakala ni Kati ya mwajiriwa na chama au Kati ya mwajiri na chama?Unasema nini na unakataa nini!! Hapo unazungumzia wafanyakazi walioshiriki maongezi na chama cha wafanyakazi chini ya "duka la uwakala" na si vinginevyo!! Kama makubaliano ya duka la uwakala hayajafanyika na mwajiriwa kuridhia kwa maandishi kuruhusu makato hayo, mwajiri hana uhalali wa kukata hiyo fedha. Mimi ninayezungumza nilikataa na makato yakasitishwa!! bNinaongea kwa uzoefu!