Pesa wanayokata kimahesabu ni kubwa maana ni asilimia 2 (2%). Kwa kadri mshahara unapopanda na kiasi unachokatwa kinapanda!! Kwa kianzia mshahara cha 765,000/= makato ni sh 15,300/= kwa mwezi, kwa mwaka ni 183,600/=. kwa miaka kumi ni 1,836,000/=. Lakini pia mshahara hupanda kwa hiyo makato pia hupanda!! Kuna wakati utalazimika kukatwa zaidi ya 30,000/= kwa mwezi na muda utafika utakatwa 40,000/= kwa mwezi. Mpaka kuja kustaafu utakuwa umechangia mamilioni ya shilingi!! Kila mwaka wanakudanganyia kwa kupewa T/shirt ya 15,000/= wakati wa sikukuu ya mei mosi!!