HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
72.-(1) Mkataba unaomlazimisha mfanyakazi kuwa
mwanachama wa chama cha wafanyakazi hauna nguvu za kisheria.
(2) Chama cha wafanyakazi kinachotambuliwa na mwajiri
wanaweza kufikia makubaliano ya pamoja yanayotoa duka la uwakala.
(3) Mahitaji ya makubaliano ya duka la uwakala linalobana ni:
(a) mkataba utatumika kwa wafanyakazi waliopo kwenye
chombo cha majadiliano tu;
(b) wafanyakazi ambao si wanachama wa chama cha
wafanyakazi hawalazimishwi kuwa wanachama;
(c) ada ya uwakala iliyokatwa katika ujira wa mfanyakazi,
ambaye si mwanachama, ni sawasawa, au chini kuliko,
michango ya chama inayokatwa na mwajiri kutoka
kwenye ujira wa mwanachama;
(d) kiasi kinachokatwa kutoka kwa wanachama wote na wasio
wanachama kitatakiwa kulipwa kwenye akaunti tofauti
inayosimamiwa na chama cha wafanyakazi;
(e) fedha katika akaunti hiyo inaweza kutumika tu kwa ajili ya
kuendeleza au kutetea maslahi ya kijamii na kiuchumi ya
wafanyakazi katika sehemu hiyo ya kazi na hazitakiwi
kutumika katika kulipa-
(i) ada ya kujiunga na chama cha siasa; au
(ii) michango yoyote kwenye chama cha siasa kwa
watu wanaosimama katika ofisi ya siasa.
(4) Bila kujali masharti ya sheria yoyote au mkataba mwajiri
anaweza kukata ada ya uwakala chini ya makubaliano ya duka la
uwakala linalofuata masharti ya kifungu hiki kutoka kwenye ujira wa
mfanyakazi bila ridhaa ya mfanyakazi huyo.
Tujengeane uzoefu hapa wadau
 
Mazungumzo ya duka la uwakala ni Kati ya mwajiriwa na chama au Kati ya mwajiri na chama?
Inawezekana mkuu ukatusaidia wengi kufafanua Agency Fee
Mwajiri hahusiki kabisa!! Mazungumzo ni kati ya wafanyakazi wasio wanachama wa chama cha wafanyakazi na maafisa wa chama cha wafasnyakazi. Lengo ni kujaribu kuwashawishi wasio wanachama kuwa na wao wananufaika na huduma ya chama cha wafanyakazi hatya kama si wanachama!! Sasa huo umekuwa ni mlima mkubwa sana kwa vyama vya wafanyakazi. Havina kabisa hoja zenye vielelezo kuwa huduma yao huwafaidisha pia wasio wanachama!! Iwapo hakuna mifano hai ya vyama kuwafaidisha wanachama wao, itawezaje kupata mifano ya kuonesha inavyosaidia kunufaisha walio wanachama?

Matokeo yake kiuhalisia hakuna chama cha wafanyakazi chenye ubavu wa kuendesha mazungumzo ya duka la uwakala!! Ndio maana hata huu msamiati u7mebaki kwenye maandishi tu na watu wengi hawaujui!! Nimekuwa mtumishi wa umma kwa takriban miaka 30, sijawahi kuona hayo majadiliano ya duka la uwakala kati ya chama cha wafanyakazi na watumishi wasio wanachama wa chama chya wafanyakazi? Hiyo kwa sasa ni nadharia isiyotekelezeka kwa vitendo!!

Mwajiri hahusiki, yeye ni mtekelezaji tu wa makubaliano kama yapo. Na makubaliano hayo ni lazima yawe kwa maandishi na mtumishi ajaze fomu maalumu ya kumwelekeza mwajiri kufanya makato waliyokubaliana. Bila mtumishi kujaza hiyo fomu mwajiri hana mamlaka ya kukata mshahara wa mwajiriwa yeyote!!
 
Wazee mnatuchanganya sisi tunataka kazi nyie mnaweka comment ya vyama vya wafanyakazi

Inatusaidia nini sisi jobless ebu mkaanzishe uzi wenu uko.
Hapo ndipo mnapokosea!! Taratibu za ajira unatakiwa uzijue kabla ya kupata ajira!! Vinginevyo utajikuta unapoteza haki zako nyingi tu!! Kama vile taratibu za kuishi na mwenza unatakiwa uzijue kabla ya kumpata huyo mwenza (ili maadam unatarajia kumpata mwenza wa maisha). Vinginevyo kuna watu wanajazishwa fomu za kujiunga na chama cha wafanyakazi kana kwamba ni lazima kumbe ni hiari!! Utakapokuja kushtuka umeshaliwa sana tu!! Ni vizuri mno kujua haki na wajibu wako mapema!!
 
Mkuu me nashukuru sana, nina kufatilia na pia najifunza mengi kutoka kwako. Usichoke kutoa elimu.
 
Hatari mkuu placement hakuna, status zinataka kuniua ehe mora nivushe kwenye hiki kipindi.
Status pamoja na kuwa imesemwa sana kuwa ni kiashiria, lakini bado si taarifa ya uhakika. Kuna mtu ninamfahamu hadi leo status yake kwenye app inasema: Short listed (kwenye kada yao hawakuwa na written) kabla ya kufanya hiyo oral. Status hiyo haijawahi kubadilika japo keshamba asali siku nyingi!!
 
Ngoja tuone vichwa vinauma hatari, na maisha kitaa hayasomeki usingizi hata aupandi.
 
Back
Top Bottom