Hapana Psrs ndio kikwazo...mwajiri anahitaji manpower.Alipewa majibu rahisi kwa maswali magumu!! Alijibiwa kama mtoto mdogo ambaye hawezi kuustahimili ukweli halisi. Ni kama kina mama wengine wakijifungua mtoto halafu wakaulizwa na watoto wao wadogo je huyu mtoto mchanga ametoka wapi?. Huwajibu kuwa ametoka hospitalini!! Wengine husema tumemnunua mjini tulikoenda!!
Kama mcheleweshaji ni PSRS waajiri wasingekubali wacheleweshewe kwa takriban mwaka mzima manpower wanayoihitaji sana ili kufanikisha kazi zao. Pitia tena post yangu #34,047 kwa utulivu, ninaamini utaelewa. Nayajua maumivu uliyonayo, lakini maumivu hayo yasikunyime fursa ya kuufahamu ukweli!!
Huu ujumbe kwa WAKWEPA KODI ingekua vizuri ungewaandikia MIJIZI YA SERIKALINI ambayo kila siku tuona kwenye ripoti ya CAGBajeti kupangwa na kuidhinishwa na bunge ni kitu kimoja na pesa iliyoko kwenye bajeti kupatikana ili itumike kama ilivyokusudiwa ni kitu kingine kabisa!! Bajeti hupangwa na bunge kwa matarajio kuwa TRA itafanikiwa kukusanya kodi kwa wakati ili kukidhi haja. Lakini pia bajeti hupangwa kwa matarajio kuwa pesa iliyopangwa kuombwa kama mkopo itapatikana kwa wakati. In practice pesa huwa haipatikani yote kwa wakati kama ilivyotarajiwa!! Hapo kuna wakwepa kodi!! na wakati mwingine kunyimwa au kupunguziwa mkopo mliotarajia kupewa. Pesa ikichelewa kupatikana na michakato mingine yote inayotegemea upatikanaji wa pesa lazima ichelewe ikiwemo ajira mpya!! Huu ndio ukweli mchungu unaopaswa kufahamika na kukubalika na WATU WAZIMA.
Ukimwona mtu anakwepa kodi, huyo ni mtu mharibifu sana, analeta madhara makubwa sana kitaifa. Watanzania walio wengi huwa haiwaumi kuona mtu anakwepa kodi kwa sababu hawajui madhara yake. Wanaosubiri ajira iliyokwisha idhinishwa kabisa wamelazimika kuonja machungu yanayosababishwa na wakwepa kodi. Kuna ajira zilitangazwa May 2022, lakini lakini usaili ulifanyika February 2023, na placement kuanza kufanyika mdogo mdogo April 2023. Kasi ya mchakato inategemea kasi ya upatikanaji wa fedha iliyopangwa kwa kusudi hilo, na hakuna namna nyingine!!
Si kitu kigeni mtanzania anapotaka kununua kitu akaambiwa kuna bei mbili. Bei moja ya juu kidogo ni kwa wale wanaotaka kupewa risiti na bei ya pili nafuu kidogo ni kwa wale wasiohitaji risiti. Watanzania walio wengi hukubali kutokudai risiti na kusababisha serikali kukosa mapato. Ndiyo maana nchi zilizoendelea hakuna kosa baya linalomfanya mtu aonekane wa ovyo kwenye jamii kama kosa la kukwepa kulipa kodi!! Ukigundulika kuwa uliwahi kukwepa kodi pamoja na kwamba utalazimika kuilipa na faini juu, lakini pia unakosa sifa ya kushika nafasi yoyote ya kazi kwenye jamii. Elimu ya kodi ilipaswa kufundishwa toka chekechea!!. Kila unaponunua bidhaa bila kudai risiti ya EFD utakuwa umemsaidia mtu kuiibia serikali mapato yake!!
Ni kweli mwajiri anahitaji manpower ndiyo maana aliiomba! Lakini japokuwa iko kwenye mpango lakini hajawezeshwa bado kuwapokea!! Atawapokea kwa kadri anavyowezeshwa!! Vinginevyo mwajiri ndiyo angeilalamikia PSRS!! Hivi ni mwajiri gani atamvumilia wakala (PSRS) kutumia mwaka mzima ndo atekeleze jukumu alilopewa? Kama inmgekuwa hivyo waajiri wangeshamlalamikia PSRS siku nyingi!!Hapana Psrs ndio kikwazo...mwajiri anahitaji manpower.
Inawezekana kabisa wanamlalamikia kakini mm na wewe hatujui.Ni kweli mwajiri anahitaji manpower ndiyo maana aliiomba! Lakini japokuwa iko kwenye mpango lakini hajawezeshwa bado kuwapokea!! Atawapokea kwa kadri anavyowezeshwa!! Vinginevyo mwajiri ndiyo angeilalamikia PSRS!! Hivi ni mwajiri gani atamvumilia wakala (PSRS) kutumia mwaka mzima ndo atekeleze jukumu alilopewa? Kama inmgekuwa hivyo waajiri wangeshamlalamikia PSRS siku nyingi!!
Unamaanisha katinya psrs na mwajiri nani mwenye nguvu???Ni kweli mwajiri anahitaji manpower ndiyo maana aliiomba! Lakini japokuwa iko kwenye mpango lakini hajawezeshwa bado kuwapokea!! Atawapokea kwa kadri anavyowezeshwa!! Vinginevyo mwajiri ndiyo angeilalamikia PSRS!! Hivi ni mwajiri gani atamvumilia wakala (PSRS) kutumia mwaka mzima ndo atekeleze jukumu alilopewa? Kama inmgekuwa hivyo waajiri wangeshamlalamikia PSRS siku nyingi!!
kuna viashilia vingi vinavyofanya niamini psrs wanazingua tena sana. Japo idea ya wao kusimamia haya mambo ni nzuri lkn baadh ya taratibu zao ( hasa kuchelewesha placement na kurefusha muda kwenye mambo yao ) zina madhara mengi kiasi ambacho naona ni bora tyuu sasa wasingekuwepo iwe kama zamani watu wabebane potelea mbali.Alipewa majibu rahisi kwa maswali magumu!! Alijibiwa kama mtoto mdogo ambaye hawezi kuustahimili ukweli halisi. Ni kama kina mama wengine wakijifungua mtoto halafu wakaulizwa na watoto wao wadogo je huyu mtoto mchanga ametoka wapi?. Huwajibu kuwa ametoka hospitalini!! Wengine husema tumemnunua mjini tulikoenda!!
Kama mcheleweshaji ni PSRS waajiri wasingekubali wacheleweshewe kwa takriban mwaka mzima manpower wanayoihitaji sana ili kufanikisha kazi zao. Pitia tena post yangu #34,047 kwa utulivu, ninaamini utaelewa. Nayajua maumivu uliyonayo, lakini maumivu hayo yasikunyime fursa ya kuufahamu ukweli!!
Tukubaliane kutokukubaliana kwa amani: Siyo suala la nani ana nguvu bali ni suala la nani ana majukumu gani, na wote wanatekeleza majukumu yao chini ya Rais, ambaye ndiye mwajiri mkuu wa watumishi wote wa umma kwa niaba ya watanzania. Na Rais mwenyewe akiwa ni mwajiriwa wa watanzania, waliyemwajiri kwa kura zao, ili awatumikie kwa mujibu wa katiba.Unamaanisha katinya psrs na mwajiri nani mwenye nguvu? PSRS unatakiwa ujue wapo chini ya Rais.
Ni bora wasitangaze anira kabisa kuliko wanachofanya,awamu ya tano hawakuajili kwa winginlakini chache zilifanyika kwa wakati,au shida ya hela imeanza juwa miaka ya karibuni tu,mbona kipindi cha nyuma haikuwepo hii kitu??
Kuna uzembe upo mahali na sio kuutetea tu ambapo hakuna maana.
Mkuu unatumia nguvu nyingi kuwatetea psrs wakati utendaji kazi wao upo wazi tunaona,kiukweli ile taasisi ina shida kwenye utendaji wake tuwe wakweli bila kuficha jambo..kwanza huu utaratibu wa kuita watu kwa mafungu ni utaratibu wa hovyo sana wameuanzisha mwaka huu,
Kuna haja gani ya kuita watu interview kama huna hela za kuwaajili??
Maana wasailiwa wenyewe unawaharibia bajeti zao kwa kitu ambacho hujakiandaa,au ndio wanafanya makusudi kufunika kombe kwamba tumefanyisha saili!!
Unasema serikali inakuwa haina pesa kwa wakati niambie ni lini posho za viongozi zilikosekana na kila mwaka ripoti inakuja pesa zimechotwa.
Pesa zinazoonekana zimeliwa kupitia ripoti za CAG zingeweza kupunguza tatizo la ajira na kuongeza ufanisi makazini kwa asilimia kubwa lkn leo kaka unawatetea kwamba bajeti inakuwa shida why kwa sisi wanatupotezea pesa zetu kwa interview ambayo haijulikani hata lini itatoka.
Braza ukubali ukatae PSRS ni tatizo kwa afya ya akili ya vijana wasaka ajira,mchangiaji hapo juu ametolea mfano yeye binafsi kabisa,unapofanya oral huwa tunajiasses kabisa ulichojibu kama kipo sawa kwa vile maswali yao huwa ni clear yana majibu yanayofahamika sio ya uelewa kwamba utafikiria uuungeunge,sasa watu wanapojiasses na kuona kuwa alijibu sahihi na majibu yake humpi na husemi tatizo nini ndio shida inapokuwa kubwa,.tungekuwa tunajenga hoja kwa pamoja kuwadai matokeo ingekuwa ni vizuri zaidi.Tukubaliane kutokukubaliana kwa amani: Siyo suala la nani ana nguvu bali ni suala la nani ana majukumu gani, na wote wanatekeleza majukumu yao chini ya Rais, ambaye ndiye mwajiri mkuu wa watumishi wote wa umma kwa niaba ya watanzania. Na Rais mwenyewe akiwa ni mwajiriwa wa watanzania, waliyemwajiri kwa kura zao, ili awatumikie kwa mujibu wa katiba. Kama ugali haujaiva, haujaiva tu, huwezi kulazimisha ukaribishwe mezani!! Na kama mtu akikukaribisha mezani wakati ugali bado unaandaliwa, utasubiri sana hapo mezani hadi kero!! Ni rahisi sana kupata matokeo ya oral interview kuliko ya written, kwanza oral interview inahusisha wachache!! Kama kila kitu kingekuwa tayari, placement ingekuwa inafanyika kwa haraka zaidi kuliko matokeo ya written yanavyotoka!! Ukiona placement inachelewa ujue kuna mambo yanatakiwa kuwekwa sawa!!
Makofia alisema kuna taasisi tamu zimekubali wa database naona kuna watu wamelamba asali TPDCAiseee ni zaidi ya asali leo
Makofia jamaaa anajua sana
Taarifa zake ni za ndaaaaaani kabisaMakofia alisema kuna taasisi tamu zimekubali wa database naona kuna watu wamelamba asali TPDC
Hilo linaweza kufanyika ila pia watalalamikiwa sana na hawataeleweka kama wanavyolalamikiwa sasa.Na ikiwa wewe unachosema ni kweli kwamba taasisi ndo zenye shida kwa nn h psrs wasitoe placement mapema. Coz kusubirisha wachache ambao wanajua wamepata kazi ni bora
Kwanini watoe tangazo May 2022 huku wakijua mwaka wa fedha ni wa 2023?Hilo linaweza kufanyika ila pia watalalamikiwa sana na hawataeleweka kama wanavyolalamikiwa sasa. Tuchukue mfano wa posts za MDA&LGA ambazo zilitangazwa May 2022. Baada ya mwezi mmoja wangeitisha usaili yaani June 2022 na June hiyo hiyo 2022 wangetoa placement. Lakini ujue kuwa ajira hizo zilikuwa zimewekwa kwenye bajet ya 2022/2023 ambazo pesa yake bado haijakusanywa hata shilingi moja maana mwaka wa fedha huanza Julai mosi!! Halafu wangelazimika kusubiri hadi April 2023 ambapo ndiyo MDA&LDA wameanza kupata hilo fungu walilotengewa kwenye bajeti baada ya kuwa limepatikana!! Je unafikiri kusingekuwa na malalamiko? Kuna watu hawajui kama serikali inaweza kuwa haijapata pesa ilizotarajia. kwa hao ni vigumu sana kuelewa! Narudia tena, serikali yoyote haina ujanja wa kupata pesa zaidi ya makusanyo ya kodi, mikopo, na gawio mahali ambapo imewekeza. Lakini chanzo kikuu ni kodi!! Kama kodi ingekuwa inakusanywa kwa kasi iliyotarajiwa matatizo haya yangepungua sana. Ni kweli kabisa wizara nyingi kama siyo zote huwa hazifanikiwi kupewa pesa yote iliyoidhinishiwa kwenye bajeti. Ikitokea hivyo mambo hutekelezwa kwa vipaumbele, na mambo mengine husubirishwa!!.