Hilo linaweza kufanyika ila pia watalalamikiwa sana na hawataeleweka kama wanavyolalamikiwa sasa. Tuchukue mfano wa posts za MDA&LGA ambazo zilitangazwa May 2022. Baada ya mwezi mmoja wangeitisha usaili yaani June 2022 na June hiyo hiyo 2022 wangetoa placement. Lakini ujue kuwa ajira hizo zilikuwa zimewekwa kwenye bajet ya 2022/2023 ambazo pesa yake bado haijakusanywa hata shilingi moja maana mwaka wa fedha huanza Julai mosi!! Halafu wangelazimika kusubiri hadi April 2023 ambapo ndiyo MDA&LDA wameanza kupata hilo fungu walilotengewa kwenye bajeti baada ya kuwa limepatikana!! Je unafikiri kusingekuwa na malalamiko? Kuna watu hawajui kama serikali inaweza kuwa haijapata pesa ilizotarajia. kwa hao ni vigumu sana kuelewa! Narudia tena, serikali yoyote haina ujanja wa kupata pesa zaidi ya makusanyo ya kodi, mikopo, na gawio mahali ambapo imewekeza. Lakini chanzo kikuu ni kodi!! Kama kodi ingekuwa inakusanywa kwa kasi iliyotarajiwa matatizo haya yangepungua sana. Ni kweli kabisa wizara nyingi kama siyo zote huwa hazifanikiwi kupewa pesa yote iliyoidhinishiwa kwenye bajeti. Ikitokea hivyo mambo hutekelezwa kwa vipaumbele, na mambo mengine husubirishwa!!.