Kwa taarifa yako kupigiwa simu haina maana kwamba mwajiri amejiandaa kukupokea na kukupa pesa za kujikimu. Maana yake ni kwamba umeshaingizwa rasmi kwenye pay roll ya serikali na uhakiki wa vyeti umekamilika. Wapo waliopigiwa simu na bado hawajapata posho ya kujikimu na nina mifano halisi!! Ilikuwa hivi: Waliporipoti na barua ya psrs waliishia kujaza taarifa binafsi, kuonesha vyeti na kuambiwa rudini tutawaitya kwa simu. Baada ya wiki mbili wakapigiwa simu. Walipofika kazini walipewa barua rasmi za ajira, kupewa maelekezo ya majukumu yao, wakapewa fomu za kuomba ruhusa siku 14 na wakaondoka. Huku nyuma wakaambiwa posho zao. zinashughulikiwa! Kuna wengi ni miezi sasa posho bado ni kitendawili!!