Hongera ndugu, ndio maana tunasema wakati wa Mungu ndio wakati sahihi, tusikate tamaa , japo kama hivi pdf zinapotoka inaumiza sana kibinadamu pale unapokuta jina halipo , lakini huzunika kidogo tu ila usimnung'unikie Mungu yeye ni mwema sana hutuazia mema daima na hutupa pale ambapo yeye huona pana tufaa, sisi tunapanga ila yeye Baba yetu wa Mbinguni ni muamuzi, tusikate tamaa , daima huwarehemu maelfu kwa maelfu ya wanadamu wanaomtumainia ukiwepo Wewe na Mimi cha msingi tuendelee kumtegemea na kuyatenda mapenzi yake katika maisha yetu, kwa hakika atatupa asali ( Ajira) wote hapa ndani kwa mapenzi yake, pia katika sala na dua zetu tusisahau kuwaombea watumishi wa PSRS ili Mungu azidi kuwaongezea weledi na kutenda haki katika majukumu yao, Mungu wetu ni mwema na msikivu na ndiye muweza wa yote tukianza na yeye na kumaliza na yeye hakuna litakaloshindikana yeye ni ALPHA NA OMEGA( Mwanzo na Mwisho).