HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Ee Mungu Baba yetu wa Mbinguni, twajua ya kuwa wewe ni mwema maishani mwetu na unatupenda, umesema tusizitegemee akili zetu , bali tukutegemee Wewe uliye Muweza wa Mambo yote, basi twakusihi Baba yetu, utuangalie wanao humu ndani tunao subiria fursa za Ajira kwa saili mbalimbali tulizofanya kupitia Sekretariati ya Ajira ni Wewe Baba ndiye ulie tuwezesha kutufikisha katika saili za mahojiano kwa maana bila Wewe hata hatua hii tusingeweza kuifikia kwa nguvu zetu wenyewe, tunaomba utupe uvumilivu kwa kipindi hiki tunaposubiria majibu ya saili zetu, utuangalie kwa jicho lako la huruma Baba ili wote humu tuliofikia hatua ya sahili za mahojiano tukapangiwe vituo vya kazi kwa sifa na utukufu wa Jina lako, na wale ambao hawajaweza kufika hatua ya usahili wa mahojiano , basi uwabariki awamu hii wakaweze kuifikia hatua hiyo ili nao Baba, kwa huruma zako ukawapatie nafasi za Ajira, ili Ukuu wako na Utukufu vikapate kukurudia Wewe mwenyewe.

Tumeomba hayo tukiamini Baba utatenda katika Kristo Yesu Bwana na Mwokozi wetu.
Amen
 
Back
Top Bottom