Mzee Baba kuna vitu inabidi tuwe wa pole kuna mambo yanafanyika kinyume na utaratibu kabisa.Ilala naona malengo mazuri kabisa ya mkuu wa nchi, vibali vinatolewa ila usimamizi wa mchakato wa ajira na namna ya kuingia kwenye system kuna watu wamefanya kama kilakitu chakwao, wanaweka watu wao, hawafuati kanuni zinazo waongoza, wanafanya kazi kimazoea hawajui kuwa kuna kesho wao umri umeenda ndg zao wataingiaje kwenye asali baada ya wao kutoka hawafikirii. Wenzetu mataifa mengine wapo serious na ajira ambae anasifa anapewa bila konakona. Sasa ajira ilitangazwa mwaka jana tena may na june hii ni April na itafika july watu hata kazini hawajaitwa huu ni uzembe na ni magumashi ambayo Psrs hawana majibu ya kutupa tuwaelewe.Mambo ni nyoronyoro kama jongoo, yaani mwaka mzima wa fedha unasubiria kazi daah inaunmiza sana.
Hawa jamaa ifike sehemu wawe reliable mambo sijui paper limevuja, cjui nani alikuwa na maswali kabla ya interview, mara mnasubiri placement mwanka mzima tatizo ni nini.Mnajua data zote ni taasisi gani, wilaya gani zinataka watumishi kibali kipo tayari sasa siasa yanini kwenye hayo mambo,mkielemewa mseme muongezewe wataalam, nina hofu PSRS hamana wataalam wakutosha, Miundo mbinu na procedure zenu bado sana.
Maana kama una wataalam, professionals na watu wenye uzoefu hamuwezi enda hivyo. Hapo nimezungumzia wataalam wakutosha
Watu wa ICT tena Cerified IT ambao wapo current, watu wa mitihani maana hata paper zenu hazieleweki kesho hivi kesho vile ni vile mnajisikia kufanya au mtu kaamka anasema hii paper iwe hivi hamna utaratibu, tuna taka ethics za kazi yenu zizingatiwe.
Punguzeni mlolongo, mambo ya vikako kila siku vikao mambo yapo wazi yanawapunguzia ufanisi wa kazi.
Data base Data base ifanye kazi ,vijana tumechoka kurudi kufanya mausaili kila muda bila sababu. Leo mmetangaza wataalam wa maendeleo ya jamii lakini mnao wengi kwenye data base si walifanya mwaka jana usaili mmewaita wale wote, wapeni kazi madogo mtu kama amefaulu chuo na anaweza kujieleza kamati ya usaili imempa atleast passmark ya 50 mpeni kazi huo ndo utaratibu na ndio sheria, na kanununi inataka, tena mapaka waishe wote kwenye kanzi data ndio mtangaze..kuita kwenye usaili watu wanatoka tunduma, rombao, tarakea mwingine mbjnga, mwingine sengerema, nduta, nyasa, ludewa mnawatesa watoto wa watu provided hawana kazi za msingi za kuwainguzia kipato cha hayo magharama.
Hayo lazima tuongee na tutaongea mpaka kieleweke maana hiyo ni haki ya kila mtanzania .