Hello Guys
Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa Pumzi, sijawai kuchangia katika jukwaa hili especially kwenye huu uzi...
Naweza sema ni bahati lakini pia wakati wa Mungu ni sahihi leo hii nimedumbukia kwenye pipa la Asali..
nimefanya interview 04
nlianza fanya interview 2021 mwezi wa pili rasmi...
mwezi December nikafanya interview kwa kujiiba sana....
kwanza Niliitwa interview majina nikaja yaona zimebaki siku 2, niliomba ruhusa kwenye kijibarua changu nikanyimwa ikanibidi nisafiri usiku saa 2 kutoka Mbezi kwa Magufuri, nimefika Dodoma saa kumi usiku, nikakosa sehemu ya kulala nikalala lecture room, saa kumi na mbili umeme ukakatika hivyo kimsingi sikua nimesoma kibarua changu ninaingia saa 1 natoka saa 12 jioni nimefanya written kwa juhudi na idea tu, matokeo walisema wanatoa baada ya siku 2 ikawa tofauti mpk jumatatu matokeo hayakutoka na oral ilikua jumanne imefika jioni nikaamua kuondoka Dar pasipokua najua matokeo ila ni roho tu na Uwezo wa Mungu uliniongoza tu lengo lilikua ni kusogea mpk morogoro nikiskilizia matokeo nimefika Moro saa nne matokeo yametoka nipo na ni mtu wa tatu nikapanda gari mchomoko nimefika Dodoma saa 11 asubui nikaomba mahala nimeingia nikaoga nikavaa nikaenda interview kumbuka sijajiandaa na kitu apo ila ni roho Mtakatifu tu
aliniongoza oral nimefanya saa sita mchana sijala kitu toka asubui
kiukweli oral maswali 5 nlijibu maswali 4 vzr swali moja nlizingua na lingine nlijibu point 3 badala ya tano naweza sema ni ile knowldge na kwakua nlikua na tabia ya kusoma soma..
napenda kusema kwa Wasaka mirija wenzangu kua
1.Mungu kwanza
2. Wakati wa mungu ni sahihi nimekaa miaka 6 bila ajira ya maana kwa ujira mdogo uku nikiwa ni muhitimu tena mwenye vyeti vizuri
3. Maandalizi na kusoma sana ndio ngao yako usibweteke na maksi za written walioongoza written yetu wameachwa wote unapo apply tu status ikisoma received anza soma kama uko UE
4. Changamana na watu upate connection maana mimi sikusoma ila kupitia maongezi nilipata kitu
asanteni one oral interview one goal