Kwanini usijengwe ukuta katikati ya barabara za mikoani kupunguza ajali?

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Shida kubwa na chanzo Kikuu cha ajali ndani ya nchi yetu ni Kama zifuatazo;

1. Uchovu wa Madereva wakiwa barabarani.
2. Magari mengi Ni mabovu hasa malori hivyo ni Kama majeneza yanayotembea
3. Ulevi kwa madereva, Tanzania tunajifanya Sheria haziruhusu kuendesha ukiwa tayari umeshakunywa pombe wakati tunaona bar Nyingi walevi wanakuwa wamepaki magari wakiwa bar wanakunywa na wakitoka wanaenda kuendesha magari huku Polisi wakiangalia tu kisubiri ajali itokee wapige pesa ndefu.
4. Kutokufuata Sheria za barabara, huu ni ugonjwa wa Madereva wengi wa Tanzania hasa wakati wa ku overtake ,tunatake risk sana, ajali nyingi zinatokana na kuovertake sehemu isiyoruhusiwa.

Turudi kwenye mada kuu, ajali nyingi za siku hizi ni kwamba roli linahama upande wake linaenda upande wa pili halafu chuma zinagongana uso kwa uso, na ni nyingi sana ajali za namna hii kwaKuwa malori ni mengi mno nchi hii wameua reli, sasa sijui reli ije tu ili waondoe haya malori kwa road.

Sasa kwanini serikali isijenge ukuta katikati ya barabara Ili Lori likitaka kuhamia upande wa pili lishindwe hivyo kuepusha Ajali.

Wanaweza wakaweka ukuta hata mita moja, ukuta mgumu na mrefu, kwakuwa ajali zimezidi sana na wewe unaesoma muda wowote utapata ajali ya kugongana uso kwa uso na roli.
 
KUHUSU BARABARA NCHI YETU ILIFANYA VIZURI MAENEO MENGI SIJUI MDUDU GANI AMETUVAMIA MFANO NILIWAHI KUPITA TUNDUMA FORENI YA KUINGIA MPAKANI INATISHA SABABU KUBWA NI BARABARA KUWA NYEMBAMBA SIONI SABABU ZA KUSHINDWA KUPANUA BARABARA KM 10.
WAKATI HUDUMA ZA BANDARI ZINABORESHWA NI MUHIMU KUBORESHA LANGO LA UTOAJI MIZIGO.
 
Ni shida chanzo Kikuyu Cha ajali za kwetu ni Kama zifuatazo

1. Uchovu barabarani.
2. Magari mengi mabovu hasa malori.
3. Ulevi, Tanzania tunajifanya Sheria haziruhusu kuendesha ukinywa wakati tunaona kila bar walevi wamepaki magari wakitoka bbar wanapenda kuendesha na Polisi wanaangalia tu, wakiwa huko barabarani ndo ajali.(Eg. Zorro daughter)
4. Kutokufuata Sheria za barabara, huu ni ugonjwa wa Tanzania hasa wakati wa ku overtake ,tunatake risk sana, ajali nyingi zinatokea na kuovertake sehemu isiyoruhusiwa.

Turudi kwenye mada, ajali nyingi za siku hizi ni kwamba roli linahama upande wake linaende upande wa pili ngoma zinagongana kichwa kwa kichwa, na nyingi hizi kwa maana malori ni mengi mno, sijui reli ije tu waondoe haya malori.

Sasa kwanini serikali isijenge ukuta katikati ya barabara Ili Lori likitaka kuhamia upande wa pili lishindwe hivyo kuepusha Ajali.

.wanaweza wakaweka ukuta hata mita moja mgumu mrefu, ajali zimezidi sanaYani
Huo ukuta ndio utakua chanzo kikuu cha ajari
 
Ajali haina kinga, unaeza kujengwa ukuta na ajali nd zikazidi vile vle pia ili kuw na ukuta ama kingo ,njia za kwnda n kurudi lazima ziongzeke upana wake ili incase gari ikiharbika iczuie gari zngne kupita.
 
Umewaza nje ya box kama uhuru wako unavokuruhusu... Ni Jambo zuri

Lakini Akili yako ulisahau kuitoa nje ya box ili ikusaidie mambo mawili matatu...

Anyways acha wajenga barabara waje kuboresha wazo lako.
 
Ni shida chanzo Kikuyu Cha ajali za kwetu ni Kama zifuatazo

1. Uchovu barabarani.
2. Magari mengi mabovu hasa malori.
3. Ulevi, Tanzania tunajifanya Sheria haziruhusu kuendesha ukinywa wakati tunaona kila bar walevi wamepaki magari wakitoka bbar wanapenda kuendesha na Polisi wanaangalia tu, wakiwa huko barabarani ndo ajali.(Eg. Zorro daughter)
4. Kutokufuata Sheria za barabara, huu ni ugonjwa wa Tanzania hasa wakati wa ku overtake ,tunatake risk sana, ajali nyingi zinatokea na kuovertake sehemu isiyoruhusiwa.

Turudi kwenye mada, ajali nyingi za siku hizi ni kwamba roli linahama upande wake linaende upande wa pili ngoma zinagongana kichwa kwa kichwa, na nyingi hizi kwa maana malori ni mengi mno, sijui reli ije tu waondoe haya malori.

Sasa kwanini serikali isijenge ukuta katikati ya barabara Ili Lori likitaka kuhamia upande wa pili lishindwe hivyo kuepusha Ajali.

.wanaweza wakaweka ukuta hata mita moja mgumu mrefu, ajali zimezidi sana
Hiyo budget itoke wapi mkuu
 
Safi sana kwa kufikiri vyema mtoa mada. Usifadhaishwe na wapumbavu wanaoamini wanatunza familia kwa mawazo yao bora ilhali hawana uwezo wa kufikiri.

Naamini ulilenga kuwasilisha kitu kama Concrete Barriers, yes inawezakana concrete ni urefu 2 to 4 feat na inaweza kuzuiza magari kuintervene. Mamlaka zifanyie kazi wazo lako.

M6-barrier-excavator-lift-1200x828.jpg

Kama picha inavyoenesha ukianza kwenda hadi tamati au eneo rasmi la kuingia njia nyingine hii imesaidia sana mataifa mbalimbali kupunguza ajali.
 
Back
Top Bottom