Kwanini unaogopa kumwambia una mtoto?

Kwanini unaogopa kumwambia una mtoto?

My random thoughts:

1. Jamii imewafanya wawe hivyo. Tumezoeshwa kuwa mwanamke aliyezaa nje ya ndoa ni mhuni, easy, et al et al.

2. Lakini pia kuna extremes. Yani mwanamke kila sekunde mbili anamuongelea mtoto. huyu naye ni wa kumcheki kwa jicho la pili. [HASHTAG]#feminists[/HASHTAG] [HASHTAG]#myWorld[/HASHTAG]

3. Uhusiano na baba wa mtoto upoje? Kupendana ni sawa ila kuanzisha mahusiano naye ni jambo kubwa. Ili usijepata shida mbeleni ni vyema ukafahamu hili mapema.

4. Nawaza tu, na mimba tulizowatia mabinti wa watu wakazitoa (na mabinti waliotoa mimba) nayo inabidi tuseme

5. All in all ni mambo yanayoepukika. Kuzaa nje ya ndoa ni kujihakikishia kuwa unabeba baggage of your past wherever you go.

Best solution? Tuache zinaa kabla ya ndoa. Maana unaweza dhani mtoto ndo mzigo pekee lakini kwa kila mwanaume (mwanamke) uliyelala naye umebeba mzigo wake. Kwa mantiki hiyo kila mahusiano utakayoyaanzisha huanzi na a clean slate, yani sahani yako tayari ina chakula cha hoteli A wakati sasa upo hoteli B.
Inawezekana kuacha now..sitaki kuhubiri..but kuacha na kusafisha your mind of the past baggages you have been carrying za past relationships.

Kwako dada mwenye mtoto...hongera na pole. Hongera kwamba hukuchagua kutoa mimba (ingawa wengi wenu mngejua mapema kuwa ni waja wazito mngetoa au wengine mlijaribu vidonge vikagoma). Ila hongera tu. Jukumu lako ni kubwa.

Pole kwa kuwa jamii itakuhukumu. Ndiyo jamii yetu kuwa mwizi aliyekamatwa na kuku ni mkubwa kuliko mwizi aliyeiba mbuzi na hakukamatwa.

These are just random thoughts...
 
Lazima waogope maana kuwa na mahusiano na msichana aliye na mtoto yataka MOYO SN. WALIO WENGI hawaachani MOJA KWA MOJA NA baba watoto wao
Hawawezi kweli kuachana kwasbbu bado wataendelea kuwasiliana kuhusu mtoto, sasa shida huja kama baba wa mtoto bado hajaoa!? Hapo sasa ndio mengine
 
Kwangu mm mtoto siyo kikwazo kabisa, na nitalea kama mwanangu kabisa,
Kwaiyo bora aniambie ukweli tu
Na akitaka kumpeleka mtoto kwa baba yake pia umruhusu..wakakutane....
 
Mmmmh Jaman! Mwanaume mwenye Mapenzi ya Dhati hata Ukimwambia Una Watoto 2 Atakupenda tu.
Mara nyingi mwanaume atakuwa na amani kama baba wa mtoto hayupo duniani...lakini kama yupo ni fujo tu...kuna dada mmoja nimezaa nae first born wetu..tukaachana..ila kapanga sehemu nyumba nzima.anaishi na mwanae na house girl tu...sasa....kuna jamaa yupo nae kwa sasa..ANAGEGEDA....siku MOJA nimekwenda pale kumtazama mwanangu..kumbe kuna kidume ndni mle sebuleni...basi nikakaribia kwenye sofa nikaanza kuteta NA my son.. Kuhusu hili na lile.. Basi kile kidume kuniona alichukuwa GAZETI LA MZALENDO akaanza kulisoma huku kafunika uso kuanzia saa NNE hadi saa TISA mchana bado amejifunika Gazeti huku akipumua kwa shida mno...pumzi nazisikia zinapandana na kushuka...hadi naaga yule bwana bado kajifunika gazeti bado anasoma...nilipotoka nje nikasema adhabu anayopata yule jamaa...sitakii inipate na mimi....
 
Yani nina rafiki angu, ukikaa naye dk 2 lazima atammention her lil man. Sasa pata picha unakaa na mtu mwaka na hajamtaja mwanae hata kwa bahati mbaya. Itabidi tu ukimbie, sio kwa roho ngumu hiyo


Yaani ni roho ngumu haswa, mwaka?
Attachment ya miezi 9 lazima wanakuwa part of us, sijui utawezaje kujikausha kuwa huna mtoto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom