Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu usio na shida na dhambi?

Umeusoma na kuelewa huo mchoro wa Epicurean Paradox?

Umesoma hiyo part ya "The Problem of Evil" kutoka hicho kitabu cha "Philosophy of Religion:An Anthology" nilichokiweka hapa?
Simple tu
Kaumba Shida Na Dhambi Ili Ajue Nani Ni Mbora Kati Yetu,Kabainisha Njia Zote Mbili Kisha Katuacha tuwe Huru, Mwenye Akili ataacha dhambi Aliyekengeuka Atazifata
Just simple tu Hata Mtoto wa Kindergarten anaelewa.
 
Hujaelewa swali, hujaelewa swali, hujaelewa swali. Na hivyo umeshindwa kulijibu.

Nakuuliza John alishindwa kuzuia mguu wake usikanyage mwiba bila kuvaa kiatu?

Jibu lake ni ndiyo, alishindwa au hapana hakushindwa.

Ukianza kuleta mazungumzo ya ku justify kwa nini kavaa kiatu, hujajibu swali.

Zaidi, unaposema Mungu mjuzi wa yote anawapa watu shida na dhambi ili ajue nani ni bora kati yetu, huoni kwamba unaji contradict? Mungu anayejua yote kwa nini anahitaji kuwapa watu shida na ulimwengu wenye dhambi ili kujua nani ni bora, wakati hao watu kawaumba yeye na huo ubora kawapa yeye?

Mungu anajitekenya mwenyewe halafu anacheka mwenyewe?

Yani Mungu kaumba watu, kawapa akili, kawapa uwezo, wengine mkubwa, wengine mdogo, halafu ili ajue uwezo ambao yeye mwenyewe huyo Mungu kawapa hao watu, inabidi awape shida na dhambi?

Halafu unamuita huyo Mungu mjuzi wa yote?

Bila shida na dhambi huyo Mungu angeshindwa kujua nani bora na nani si bora?
 
Simple tu
Kaumba Shida Na Dhambi Ili Ajue Nani Ni Mbora Kati Yetu,Kabainisha Njia Zote Mbili Kisha Katuacha tuwe Huru, Mwenye Akili ataacha dhambi Aliyekengeuka Atazifata
Just simple tu Hata Mtoto wa Kindergarten anaelewa.
Super charged
 
Back
Top Bottom