Do you know how the universe came to its existence?
The facts that unakwepa hili swali ni kwasababu lipo beyond you logical capability of thinking.
You can be god to your followers, but OMNISCIENT AND OMNIPOTENT GOD, ALPHA AND OMEGA LORD? No You can't be the one and never anybody shall be!
Sijawahi kusema najua ulimwengu umeanza vipi.
Na kutokujua jibu la swali hili, hakumaanishi jibu ni Mungu, kunamaanisha sijui ulimwengu umeanza vipi.
Usitake kulazimisha kwamba, mimi kutojua ulimwengu umeanzaje, maana yake ulimwengu umeanza kwa kuumbwa na Mungu.
Hii ni logical fallacy inaitwa "logical non sequitur".
Ngoja nikueleze kwa mfano, labda utaelewa vizuri.
Mimi natumia contradiction kukuonesha jibu fulani si sahihi, hata kabla sijajua jibu sahihi.
Akija mtu mwanamme, John, ana miaka 30 leo, akawa na binti wa kike mchanga, wa miezi 6 leo, Anna, halafu huyu John (30) akasema huyu binti wa miezi 6 leo Anna ni mama yake mzazi John, kwamba huyu binti Anna mwenye miezi 6 leo ndiye aliyemzaa John, mwanamme mwenye miaka 30 leo, tutajua kwamba hii habari si sahihi.
Kwa nini?
Kwa sababu ili Anna awe mama mzazi wa John, inabidi Anna awe mkubwa kuliko John na awe na umri wa kuweza kumzaa John.
Hapo tumejua kuwa Anna hawezi kuwa mama yake mzazi John. Bila hata kumjua Mama mzazi wa John.
Hatuhitaji kumjua mama yake mzazi John ili kujua kuwa Anna si mama yake mzazi John.
Sasa, mimi nakwambia Anna si mama mzazi wa John. Wewe unaniuliza, "Sasa Mama mzazi wa John ni nani?". Hili swali sihitaji kujua jibu lake ili kujua kuwa Anna si mama mzazi wa John.
Swali ni zuri, lakini ni irrelevant katika kujua kama Anna ni au si mama mzazi wa John.
Unauliza swali irrelevant.
Contradiction ya timeline inatuonesha Anna mwenye miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa John mwenye miaka 30 leo.
Mfano mwingine.
Tukijua kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, halafu mtu akaja akasema 10 ni square root ya 2, tutajua jibu hili si sahihi, hata kabla ya kujua square root ya 2 ni nini.
Tutajua vipi? Tutajua kwa sababu square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, na 10 ni kubwa kuliko 2, hivyo 10 haiwezi kuwa square roit ya 2. In fact tunaweza kuonesha kuwa 10 ninsquare root ya 100, na 100 si 2, hivyo 10 si square root ya 2.
Tunaweza kujua jibu fulani si sahihi, bila hata kujua jibu sahihi.
Sasa mimi nakuambia sijui square root ya 2 ni nini, ila najua 10 si square root ya 2.
Wewe unalazimisha, square root ya 2 ni nini? Kimsingi Unaniambia "Ukishindwa kujua square root ya 2, basi lazima jibu ni 10".
Huoni contradiction katika number line.
Dhana ya kuwepo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, aliyeumba ulimwengu wenye kuweza kuwa na baya lolote, ina contradiction.
Contradiction hiyo, inaonesha Mungu huyo hayupo, katungwa na watu katika hadithi tu.
Huyo Mungu tushamuondoa, kimantiki, kama vile tulivyoondoa jibu la "10 is the square root of 2" au "Anna who is 6 months old today is the biological mother of John who is 30 years old today".
Sasa, ukileta swali la ulimwengu umeanzaje, hata nikisema sijui jibu lake, mimi kutojua jibu la swali la ulimwengu umeanzaje haimaanishi jibu ni Mungu, inamaanisha sijui ulimwengu umeanzaje tu, lakini najua haukuanza kwa kuumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote. Kwa sababu ya contradiction niliyoitaja hapo juu.
Kama vile ambavyo ninaweza kujua mtoto wa kike wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme wa miaka 30 leo.
Kama vile ninavyoweza kujua kuwa 10 haiwezi kuwa square root ya 2.
Tatizo unakuja na swali irrelevant.
Nakwambia mtoto wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa mtu mzima mwenye miaka 30 leo, unaniuliza mama wa huyu mtu mzima ni nani? That questionnis irrelevant and does not negate my logic hata kama sijui jibu.
Nakwambia 10 haiwezi kuwa square root ya 2. Unaniuliza sasa square root ya 2 ni nini? Sijasema najua square root ya 2 ni nini, nakwambia square root ya 2 itafute chini ya 2, si juu ya 2. Namba yoyote itakayokuwa square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2. 10 haiwezi kuwa square root ya 2.
Swali lako la ulimwengu umeanzaje ni tofauti na irrelevant kwenye hoja yangu ya kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Jinsi yoyote ulimwengu ulivyoanza, haukuanza kwa kuumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.