Kwanini Ukraine haishambulii Russia moja kwa moja?

Kwanini Ukraine haishambulii Russia moja kwa moja?

Ukweli ni kwamba so NATO na USA hawawezi kuivamia Russia moja kwa moja...!

Wanachohofia wao na ambacho hawataki kitokea ni kwamba endapo wataivaa Russia au kuingia Vitani Ukraine moja kwa moja, inakwenda kutokea Vita Kuu ya 3 ya Dunia, ambapo Watu wengi zaidi wasio na Hatia watapoteza Maisha kuliko sasa hivi...!

Vita hivi tu vya Ukraine vimesababisha hari ya Uchumi kwa nchi Masikini kama Tanzania kutetereka, Mafuta yamepanda Bei na gharama za Maisha zimepanda!

Sasa hari itakuaje ikitokea Vita ya 3 ya Dunia...!?

Thats why nchi za Ulaya na USA wanatoa tu msaada wa Vifaa vya kivita bila kujiingiza moja kwa moja...!
Nato hawajali 'watu wengi sana wasio na hatia'. Wanachoogopa ni wao wenyewe kufikiwa na vita tena vya nyuklia.

Wangekuwa wanajali sana raia wasohatia wangewekeza nguvu nyingi kwenye kusuluhisha huu mgogoro kidiplomasia na sio kijeshi kwa kumpump Ukraine na silaha nyepesi ambazo zinafanya vita iendelee japo kwa muda kidogo ila kwa uhakika mwishoe ukraine atapoteza. Km primary concern yao ni innocent people basi primary solution ilitakiwa iwe diplomacy. There's no way utapromote vita alafu iwe unajali raia wasio na hatia, you just can't have it both ways.

Na Kama kweli wanataka Ukraine ashinde uvamizi wa Russia basi wampe silaha za nguvu kweli wampe makombora ya masafa marefu eg. Tomhawk, wampe mifumo ya ulinzi wa anga ya kisasa eg. Patriot/thaad, wampe ndegevita kama f22 raptors au f35 stealth, wampe drones, wampe black hawks, wampe melivita, manowari, strategic bombers, wampe kila aina ya silaha zitazoweza kujilinda dhidi ya urusi ikibidi waingize na majeshi yao.



Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hapa hoja ilikuwa na huyo aliyekuwa anasema kuwa Serikali ya sasa imeingia madarakani 2019 tu.Hilo la wananchi kukubali kutawaliwa na mtu mmoja tangu 2000 sina uhakika sana japo huwa inawezekana.Si unaona hata kwetu CCM inatutawala tangu ikiitwa TANU [emoji3]
Nadhani uja muelewa ali maanisha serikali ya sasa ya Ukraine na si ya Urusi.

Suala sio kuongoza muda mrefu suala ni je unatatua matatizo ya wananchi wako?

Putin kaitoa Urusi kwenye hali mbaya sana mpaka sasa angalau imepata nguvu ya kujitutumua,baada ya kuanguka Usoviet Urusi ilikuwa haina uwezo hata wa kulipa wafanya kazi wake mshahara maana ilipoteza zaidi aslimia 45 ya uchumi wake kwa hiyo Putin ni muhimu sana kwa Urusi.

Maana ss hapa tuna badilisha viongozi kila kukicha lakini hakuna cha maana kilicho badilika.
Hata ukifuatilia Ujerumani makansela wake huwa wanadumu sana madarakani.
 
Nadhani uja muelewa ali maanisha serikali ya sasa ya Ukraine na si ya Urusi.

Suala sio kuongoza muda mrefu suala ni je unatatua matatizo ya wananchi wako?

Putin kaitoa Urusi kwenye hali mbaya sana mpaka sasa angalau imepata nguvu ya kujitutumua,baada ya kuanguka Usoviet Urusi ilikuwa haina uwezo hata wa kulipa wafanya kazi wake mshahara maana ilipoteza zaidi aslimia 45 ya uchumi wake kwa hiyo Putin ni muhimu sana kwa Urusi.

Maana ss hapa tuna badilisha viongozi kila kukicha lakini hakuna cha maana kilicho badilika.
Hata ukifuatilia Ujerumani makansela wake huwa wanadumu sana madarakani.
Hapo nimekuelewa Mkuu
 
Mkuu nakukubali sana kule tech and gadgets, heshima kwako, hapa unepuyanga!
Mkuu jibu hoja kama mtu mzimq ambaye ni matured.

Kusema mtu umepuyanga sio maneno ya sawasawa kama mtu hukubaliani nae kimtizamo mquote weka maoni yako na maisha yaendelee mbona hupungikiwi kitu.

Huo ni ushauri tu mkuu kwa sababu sina uwezo wa kukupangia vipi uishi na vipi uandike.

Asante.
 
Wasalaam,

Nahitaji kujua kwanini Ukraine haishambulii moja kwa moja kwa makombora yake na kupiga maeneo mbalimbali ya Russia!

Asanteni.
Uwezo kiduchu na itakuwa sababu Kwa Russia kuichukua ukraine yote🏃
 
Huyu MBIGIRI mtu wa kutafuta huruma, inafaa aondoke haraka Ukraine kwa sababu kawaletea shida wa Ukraine.
JamiiForums1476420313.jpg
 
Hana attack weapons, Wana defensive weapons tu.

Russia iliwahi kuwapiga biti kwamba atayeiuzia Ukraine silaha ataona cha mtema kuni
NAto wakiingia hapo Ni vita ya tatu ya dunia. Wakifanya hivyo Mchina, Iran, Kiduku watajiunga na Mrusi. Na wote ambao ni maadui wa Marekani.

Pili, Ukraine si mwanachama wa NATO. Angekuwa mwanachama hata Putin asingeanzisha hii vita kwasababu cha moto angekiona. Sera ya NATO Ni kwamba mwanachama mmoja akishambuliwa Ni NATO yote imeshambuliwa. Wataingia vitani.

Mrusi akiruhusu Ukraine ijiunge NATO maana yake ameruhusu NATO kuweka miltary base pale Ukraine, kitendo ambachoeni kitanzi kwake.

Nne, ikiwa Ukraine itajiunga nato , mrusi anajua tayari Ukraine atakuwa na support ya kijeshi ya NATO, na hivyo Ukraine ataweza kuanzisha vita kuyakomboa maeneo ambayo Putin ameyachukua hasa hilo eneo la cremea ambalo Ni tajiri sana.

Pia ikumbukwe enzi za COLD WAR in the 1930s Soviet walitaka kuweka kituo pale Cuba, na Mmarekani alikataa kabisa kwamba itahatarisha usalama wake, na wakaingia makubaliano kwamba kituo kisiwekwe, na nafikiri ndiyo ilikuwa chachu ya kumalizika kwa Vita baridi kati ya Western block na ile Eastern block.

Leo mrusi anademand yale yale ambayo Marekani aliyataka miaka hiyo kwamba Ukraine kujiunga nato Ni kuhatarisha usalama wake Kwasababu atakuwa amemsogeza adui mpakani, sababu lazima NATO wataweka military base na watakuwa na uwezo wa kucontrol eneo lote.

Mrusi anajua anachofanya japo pengine approach yake ya vita si sahihi Sana.

Hi ni vita ya kiuchumi zaidi pia, japo watu wengi wanaitazama zaidi ktk jicho la kisiasa na kiulinzi.

Note:Hakuna bepari anayepigana vita visivyo na manufaa ya kiuchumi. Japo sijui hapa kama Russia anapata au anapoteza zaidi.

Ikumbukwe kwamba takwimu zinaonyesha biashara kati ya Russia na nchi za Ulaya kwa siku Russia inaingiza hela ya kitanzania sh, bilioni 700 kwa siku km ukiichenji hiyo dola kwa hela zetu, Ndiyo maana Putin ana kiburi.Alijipanga Sana na uchumi alikuwa nao.
 
Tayari nchi za magharibi baada ya kuona kwamba hivi vita vikiendelea kuchelewa kwisha itakuwa na madhara makubwa kwa chumi zao wameamua kuanza kuipa Ukraine silaha za mashambulizi na matokeo yake leo meli ya kivita ya Russia imepigwa kombora moja la kufa mtu kwenye bahari nyeusi na kuharibiwa vibaya sana.

Nafikiri nchi za magharibi zinasubiri Russia aanze rasmi vita vyake vya Donbas kisha wamsome ndipo wamuingizie wapiganaji kibau kwa mgongo wa mamluki na hapo ndipo vita vitaamuliwa kwa Russia kuzidiwa na watajiondoa wenyewe Ukraine kwa aibu.

Wakati Marekani akipigana na Vietnam hasa kwenye miaka ya 1967-1972 Russia kando ya kuipa Vietnam silaha kali kali pia waliingiza wanajeshi wao kinyemela kuisaidia Vietnam huku wakiwapa misaada ya kijeshi ya dola milioni 300 kila mwaka sawa na dola bilioni 2.4 za sasa kila mwaka. Sasa Marekani wanaona ni muda muafaka kwao kulipiza kisasi.
 
Exactly na ndiyo maana kwa sasa Putin ndiyo mvamizi,nilikuwa naangalia jana Aljazeera,team ya War Criminal presecutors wapo Bucha kushuhudia kile majeshi ya Russia yalikifanya wakati ule mji ukiwa chini yao.Ni swala la muda tu lakini huko mbeleni pana mtu mwisho wake utakuwa kama wa Slobodan Milosevic
Slobodan milosevich.
Sidhani Kama Putin anaweza kufikia huko . Coz Russia sio drc.
 
Ni kweli kabisa Mkuu,hapo alipo kwa sasa yupo kwa dilema,hawezi kuondoa majeshi Ukraine kwa kutotaka kufedheheka lakini pia kuendelea na vita kunaigharimu zaidi Russia.Ndiyo maana nikasema mwisho wake ni mbaya sana,Dunia ya sasa Diplomasia ni silaha kubwa sana kuliko kutumia maguvu.China pamoja na 'uswahiba' wake kwa Russia lakini hapa wame mute,unahitaji zaidi uungwaji mkono na Sehemu kubwa ya Dunia ili ufanikishe kile unachokikusudia kupitia vita.Ukienda kichwa kichwa kama alivyofanya Putin unajikuta katika wakati mgumu sana kama alionao sasa,kilichomponza alijua na hapa itakuwa bussiness as usual kama alivyofanya Crimea na Georgia na Dunia ikamtazama tu.
Umechambua kijinga Sana....
 
Tayari nchi za magharibi baada ya kuona kwamba hivi vita vikiendelea kuchelewa kwisha itakuwa na madhara makubwa kwa chumi zao wameamua kuanza kuipa Ukraine silaha za mashambulizi na matokeo yake leo meli ya kivita ya Russia imepigwa kombora moja la kufa mtu kwenye bahari nyeusi na kuharibiwa vibaya sana.

Nafikiri nchi za magharibi zinasubiri Russia aanze rasmi vita vyake vya Donbas kisha wamsome ndipo wamuingizie wapiganaji kibau kwa mgongo wa mamluki na hapo ndipo vita vitaamuliwa kwa Russia kuzidiwa na watajiondoa wenyewe Ukraine kwa aibu.

Wakati Marekani akipigana na Vietnam hasa kwenye miaka ya 1967-1972 Russia kando ya kuipa Vietnam silaha kali kali pia waliingiza wanajeshi wao kinyemela kuusaidia Vietnam huku wakiwapa misaada ya kijeshi ya dola milioni 300 kila mwaka sawa na dola bilioni 2.4 za sasa kila mwaka. Sasa Marekani wanaona ni muda muafaka kwao kulipiza kisasi.
Nani kaipiga hiyo meli!??achana na mainstream media...propaganda za hovyo..nyie kwa nn hamshbulii Moscow?!...
 
Mkuu kwamba unajitoa ufahamu kabisa kuwa Putin amekuwepo madarakani muda wote,hata kipindi amejishusha kuwa PM bado yeye ndiyo alikuwa powerful kuliko hata Rais aliyekuwepo.Putin anajiona ni Almighty wa Russia kwamba bila yeye hakuna Russia in his imaginary World.
In his imaginary world!!?..pole mkuu..ifatilie Russia kabla Putin hajawa rais na amefikaje hapo...
 
Back
Top Bottom