Kwanini ukimuambia/ Ukimpa mwanamke taarifa zako zote kwa haraka atakuacha?

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Wanawake ni viumbe wanaopenda kufanya udadisi hasa linapokuja suala la mahusiano. Hii ni kwasasabu wanawake hawaridhiki mpaka wapate kile wanachokitaka, kabla hawajakipata hicho kitu mawazo yao na hisia zao muda mwingi zinakua juu ya hicho kitu. Kumfanya mwanamke awe mtafiti kwako ni moja ya changamoto mwanamke anazohitaji ili aendelee kuwa nawe kimapenzi.

Akikutambua 100%, atakua hana cha kufanyia utafiti, hana cha kumpa mawazo, hana cha kumfanya ajisikie hisia za kuna kitu hakijui kuhusu wewe, hana cha kumpa changamoto, inabidi akuache ili atafute sehemu nyingine ya kumpa hulka ya utafiti na akibaki utajikuta upo kwenye mazoea na mwanamke, jambo ambalo sio zuri kimapenzi, mnaishia kufanya mapenzi kutimiza wajibu tu.

Hii ndio sababu wanaume wanaowadanganya wanawake wanaendelea kupendwa na kuishi nao, sababu mwanamke anakua hana jibu sahihi na ataendelea kuwa naye mpaka aone ukweli ni upoje. Unakuta mwanamke anayedanganywa ataolewa kila mwaka anaendelea kuwa na huyo mwanaume na kujipa moyo lakini anamkataa mwanaume anayemuweka wazi kwamba anataka amuoe na kila kitu kipo tayari, alafu anashangaa kwanini amekataliwa.

Ukisema udanganye, uongo una madhara yake, utaishia kutengeneza mahusiano yenye sumu, na penye uongo hakuna maendeleo. Ukisema ufiche kila kitu utaonekana huna upendo pia hakutakua na maendeleo ya muda mrefu kifamilia.

Njia ipi ni sahihi sasa?
Mpatie mwanamke majibu taratibu. Utatengeneza mazingira rahisi ya kuchombezana na furaha (chombezo na furaha huimarisha mahusiano) kwa kuwa atakua anakuchombeza na kukubembeleza umpatie majibu. Pia na wewe unamchombeza na kumpatia jibu moja moja, alafu rudisha mada kwake kwa kumuuliza swali ajielezee.

Mfano, anakuuliza “unafanya kazi gani” na wewe unamjibu kiujumla, mfano we ni fundi wa kuweka vigae, unamjibu “nafanya kazi ya kupendezesha nyumba za watu” huku ukiwa na tabasamu sababu unafurahia kazi yako.

Kwa mwanamke ambaye anataka kukujua ni lazima atakuuliza maswali zaidi, wewe utaamua uendelee kumpa majibu taratibu au ubadili mada muda wowote ili abaki na maswali zaidi juu yako na kujitengezea picha nzuri/ ya kimapenzi kuhusu wewe yeye mwenyewe. Jambo litakalomfanya aendeleze utafiti juu yako.

Lakini ni muhimu ujue maswali ya kutoa jibu lote, na ni muda gani unatakiwa utoe majibu taratibu ili kumfanya mwanamke awe mdadisi zaidi juu yako, na kuendelea kukupa mawazo na hisia zake. Ukichanganya hayo utaonekana muongo au unataka sifa au mtu usiye makini na atakuchukulia kama mtu wa michezo tu na hutotengeza mahusiano matamu.

Ndio maana kuna kundi maalumu la wanaume (Whatsapp), kila siku utajifunza kuboresha mahusiano yako kwa njia zilizothibitishwa kumvutia na kumtunza mwanamke unayehitaji kujenga naye maisha.
 
Hukumu na hasira ya Mungu IPO juu ya watenda dhambi tubuni na kuacha dhambi na kumrejea Mungu wenu kabla hazijafika siku Mbaya.Muda ni mchache Sana kuendelea kuwaza, kuwawazua na kuwachambua wanawake.Hamna muda kabisa muda umeisha mwanamke HaweZi kusaidia kukupeleka peponi.Waza Mungu siku nzima ACHA kuwaza wanawake siku nzima maana chochote unachokipa muda na mawazo Yako zaidi ya Mungu kinakuwa mungu mwingine kwako.Usiabudu miungu mingine (Wanawake).Wacha waendelee na ghasia Yao ya uzinzi wewe endelea kumsifu Bwana.Jiandae na maisha baada ya kifo muda umebaki mchache Sana.

Tafuta kwanza Ufalme wa Mungu na mengine utapewa.Okoka mpe maisha Yako Yesu Kristo Sali na kusifu Kila siku usisahau kufunga mara Kwa mara.Maisha ya Dunia yanapita Usitake kuishi kama walimwengu.

Tafiti za mwanamke za kutenda hiki na kile hazitakaa ziishie na ukizifuatilia zitakutesa Bure.

Okoka Kisha ishi katika Sheria ya Mungu ya kutenda mema na kuacha maovu na kusamehe na kusali Kila siku.Utajikuta huyo mwanamke humwazi Bali unawaza Mungu na jinsi ya kufika mbinguni na kero zozote utakazozipata kutoka kwake utamtupia Mungu wako wala hutahangaika na huyo mwanamke anayeendeshwa na shetani sababu utajua anatumiwa na shetani.

Hutaogopa kufa akitaka kukuua sababu utamkimbilia Mungu katika Sala.Mungu pekee ndiye anaweza kumbadilisha umwombee tu na umsamehe BIla kinyongo.Utaishi Kwa furaha hata akikudharau akikataa kubadilika na atashangaa sababu furaha Yako Inatoka Kwa Mungu nasio kwake huyo mwanamke.
 
Kuna mmoja nilimuacha mkoani kwao nilienda kipindi kwa muda kikaz,ktk maongezi ananiuliza kuhusu gari yangu nikamwambia nishauza na hela cna nimefulia,sijatafutwa tena.
 
Kuna mmoja nilimuacha mkoani kwao nilienda kipindi kwa muda kikaz,ktk maongezi ananiuliza kuhusu gari yangu nikamwambia nishauza na hela cna nimefulia,sijatafutwa tena.
Haha, apo ulimpa taarifa zote kwaiyo hana cha kujiuliza.
Swali kama hilo unamrudishia ye mwenyewe, au jibu lako lisiwe wazi.
Mfano wa majibu unaweza kumpa.
"Vipi unataka kulinunua?"
"umemisi mambo yetu kwenye gari nini" unamchombeza.
"Gari limekua kubwa saivi na lenyewe lina mke wake"
Alafu unabadili mada, bado atabaki kujiuliza na atajitengenezea picha ya gari kama ndo ilikua silaha yako.
 
Haha, apo ulimpa taarifa zote kwaiyo hana cha kujiuliza.
Swali kama hilo unamrudishia ye mwenyewe, au jibu lako lisiwe wazi.
Mfano wa majibu unaweza kumpa.
"Vipi unataka kulinunua?"
"umemisi mambo yetu kwenye gari nini" unamchombeza.
"Gari limekua kubwa saivi na lenyewe lina mke wake"
Alafu unabadili mada, bado atabaki kujiuliza na atajitengenezea picha ya gari kama ndo ilikua silaha yako.
Nilimjibu hivo sababu alikua anang'ang'ana aje nimuoe.
 
Hao wanaopenda kudanganywa ni wanawake wepi?

Mimi the moment umenitongoza tayari najua hadi jina la utoto la mama yako, maex zako wote nawapimia nijue kama kwangu umekuja kutest au. Unakuta mtu ka date na wamama zaidi ya mara sita, au vidada vyeupe tu ndo type yake ghafla kakupenda wewe chiblack unajiuliza huyu kakosea njia au.

Mwanzo wa watu kuumizwa ni kuingia mzima mzima kama samaki. Chunguza hiyo ndezi achana na msemo wa bata ukimchunguza humli.

Ndo wengine mnaingia kwenye ndoa mnakufa kumbe huyo bwana ana desturi ya kuoa wanawake hawaishi wanakufa, au kwao wana historia ya kifafa, kila mtoto utakae zaa anadondoka na huo ugonjwa. Usipopekua utajuaje?
 
Bado siku saba tufikie kilele cha mapenzi, muwanunulie wapenzi wenu zawadi jamani....msisahau kuwapost

daaaah au basi msiwapost nimemkumbuka ghafla marehemu siku ya valentine wanawake watatu wote walimpost kwa pamoja na kila mtu akimuita mme wangu bahati mbaya hao wote hakua na mke wala.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom