Kwanini ukiacha kazi NSSF hawataki kutoa hela zako? Je, ni baada ya muda gani watakulipa?

BWANA MISOSI

Member
Feb 11, 2020
39
24
wadau naomba kuuliza, mimi nilikuwa nafanya kazi kwenye taasis flani ya private lakini niliacha na kwenda serikalini. Nilikwenda kufuatilia pesa zangu NSSF wakaniambia kama umeacha huwezi kupewa labda ungefukuzwa, nikasema msinipe cash bali mpeleke kwenye mfuko wa serikali PSSSF lakini bado imekuwa ni tatizo. Wanasema sheria ya sasa hairuhusu kufanya hivyo. naomba kupata elimu juu ya ili na je pesa zangu nitazipataje?
 
Mwenyewe mpaka leo sijapata hiyo hela mkataba wangu uliisha nasubiri wajuvi waje tujue tunavutaje mpunga wetu
 
Pesa zinajenga madaraja na kumpa maisha bashite

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Labda nijaribu kukuelewesha tu kwa uelewa wangu mdogo (note mi sio mfanyakazi wao) ni lazima uende na barua ya kuacha/kuachishwa kazi ili kutoa taarifa ya kusimamisha malipo ya michango yote kupitia jina la mwajiri wako halafu kitu kingine cha kuelewa ni kwamba zile hela hazilipwi ovyo km wengi wanavyoelewa maana kuna mtu akiacha/kuachishwa kazi anakimbilia kule waweze kumlipa mafao yake. Watanzania tunachotakiwa kuelewa zile hela ni maalum tu kwa malipo ya baada ya kustaafu ukiona umelipwa ujue tu utu umetumika kulipwa kutokana na hali ya maisha yetu ya kitanzania maana kuna wengine hulamimika pasipokua na uelewa wowote.
 
nilikwenda na barua ya kuacha kazi ndio wakaniambia watalipa endapo ningekuwa nimeachishwa na sio kuacha mwenyewe kwa hiari. Na kuhusu malipo hawalipi ovyo kweli lakini kama mtu alikuwa anakatwa kwenye mshahara ni haki yake kudai hela yake. Sasa nachoshindwa kuelewa ni namna sheria inavyotaka ufanye ili uweze kupata stahiki zako. je usubiri mpaka ufike umri wa kustaafu au je ukiacha unatakiwa kulipwa baada ya muda gani au ukiacha kazi na pesa zako zinapotea au utaratibu ukoje?
 
Back
Top Bottom