Kwanini ujenzi wa maghorofa umeshamiri Kariakoo?

Kwanini ujenzi wa maghorofa umeshamiri Kariakoo?

Habari zenu wana JF.

Kuna jambo gani ambalo linaendelea kariakoo maana kila ukienda kuna ghorofa lishavunjwa kwa ajili ya kujenga jingine. Ni kwamba bei ya vifaa vya ujenzi imeshuka au vipi?
Mkuu ukweli Maghorofa yanayojengwa kwa Wingi kkoo ni ya Serikali (NHC) yaaani wamebomoa yale majengo yao ya Kizamani wanajenga Mijengo mipya ya maaana. Mtindo unaotumika ni mtindo wa ubia kati ya Watu Binafsi na Serikali. Muda ni wako changamkia fursa, jichagulie Jengo kuukuuu la NHC nenda na ramani na bank statement Inayoonyesha uko vzuri, uombe mkataba uanze kushusha floor za maaana.
Narudia changamkia fursa wakati ni sasa!
Kwaheri
 
Thamani ya pesa yetu vs foreign currency ie $ inazidi kudorora
ukiweka 3b leo baadae mwakani unakuta ni 2.9b
Waloweka pesa ndani wanaona bora waweke kwenye assets sababu thamani yake inapanda na sio kushuka
This makes sense. Mfano mwaka huu shillingi ndio imeshuka kuliko sarafu yeyote ile duniani..
 
Yes. Solution ni kufungua account ya Dollar au kununua assets..

Dollar januari ilikuwa 2300 sasa ni 2700 kwenye banks na 3000 kwenye black markets...
Halafu tuna governor wa benk kuu na waziri wa fedha wako.kimya...

Nawahurumia hata wale wanaofanya UTT AMIS...eti wanawekeza hela huko na sh inazidi kuporomoka....sijui wanategemea nini
Hata dollar inashuka thamani sana tu. Dollar 1000 ya mwaka 2010 ni kubwa sana ukilinganisha na dollar 1000 ya 2025
 
Back
Top Bottom