Bigbootylover
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 2,847
- 1,820
Habarini wakuu,
Nina wazo moja katika hili swala la Udalali wa Nyumba/Vyumba. Kwa nini Serikali isiifanye kuwa kazi rasmi ili kupunguza tatizo la ajira na kipato kwa ujumla. Kwa sasa mtu akikutafutia nyumba/chumba inatakiwa umpe kodi ya mwezi mmoja kama pesa yake au malipo ya yeye kukutafutia nyumba au chumba baada ya hapo mmemalizana nae.
Ushauri ni kwamba madalali wasichukue hayo malipo ya mwezi mmoja, bali kuwepo na asilimia flani wanapewa na mwenye nyumba kila mwezi yule mpangaji anapolipa kodi mpaka ambapo yule mpangaji atamaliza mkataba katika hiyo nyumba. Mfano kodi yangu mimi nalipa laki moja kwa miezi sita (6*100,000=600000), na tuchukulie labda kiwango cha dalali ni 20% hivyo 20%*100000=20,000. 20,000*6=120000, hii 120000 inakuwa ndio pesa ya dalali kwa miezi sita, pindi mpangaji akilipa kodi tena yule dalali anapata hiyo asilimia yake kama kawaida sababu yeye ndo alimleta hapo.
Maoni yangu tu hayo wakuu ili kupunguza tatizo la ajira