Kwanini Uber haziruhusiwi kuchukua abiria Mwalimu Julius Nyerere International Airport?

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
8,130
8,330
Ni dhahiri kwa tuliowahi kutoka safari mbalimbali kupitia uwanja wa ndege wa JNIA bila watu wa kutulaki na kutaka kutumia Uber tutakuwa tumepata adha ya kulazimika kutembea hadi nje ya uwanja huo ili kupata usafiri huo. Najua mtasema "kwanini usipande taxi za ndani ya uwanja?" lakini jibu ni kuwa taxi hizi huwa na gharama kubwa sana.

Ukiita uber atakwambia tukutane Petrol Station ya PUMA na kulazimika kubeba mizigo yako hadi nje. Ukiwauliza sababu, wanadai hawaruhusiwi kuingia ndani na kuchukua abiria na wanaogopa kufanyiwa fujo na madereva wa taxi wa Airport.

Sababu za msingi za katazo hilo ni zipi hasa katika ulimwengu huu wa technolojia?
 
Nawasubiri nikipata dereva taxi wa pale airport itasaidis zaidi.
 
Kwa uraratibu wa huko siujui ila sehemu nyingi duniani madereva wanaoruhusiwa kuingia airport ni wale wana licence kama chauffeur licence
Na bei unakuta ipo juu ya taxi
Kwa Marekani uber/lyft nao wametengewa maeneo yao ya kuegesha na pia sehemu ya kupakia wateja katika viwanja vya ndege, kama ilivyo kwa taxi za kawaida.
 
Sina hakika na hilo, leo nimetoka airport na Uber kwenda town.... Ukitaka no. ya gari nakupa. Labda km aliingia kwa kujificha........ But the ride was ok!
 
Sijajua unamaanisha nini unaposema "UBA haziruhusiwi" wale madereva tax wa airport kuna chama chao na kama sikosei kuna malipo wanalipa kwa kupaki pale kwa ajili ya kusubiria abiria.

Kwa mtazamo wangu, dereva wa UBA kusubiria foleni na abiria ambae hana ahadi nae pale ni hasara vilevile itamlazimu aingie kwenye huo umoja kitu kinachoongeza gharama za kazi yake.

Naamini ukiita UBA kuja kukuchukua airport, gari itakuja na kukuchukua bila wasiwasi, ilimradi airport gari binafsi zinaruhusiwa, sioni kwanini UBA izuiliwe kuingia na kutoka maadam analipa parking. Ikumbukwe hazina utambulisho wowote wa kufanya zijulikane na kuzuiliwa kuingia uwanja wa ndege.
 
Na mimi nilitaki nitoe angalizo hili hili. i.e. Ukichukua Uber eg mjini kwenda airport utapelekwa vizuri tu kwani hazina utambulisho hivyo zinaingia kama gari lolote binafsi linapompeleka msafiri. Na wakati wa kutoka vile vile ukimwita mwenye Uber anaweza kuja kama gari binafsi linapokuja na kukuchukua. Labda kama utakuwa unawazodowa wenye tax pale kuwa ''subiri niite Uber nyie si mnajifanya wajanja''!.
 
Mi nikishuka zangu natoka nje Puma pale nakula bodaboda hadi nilikopaki gari fresh,niliwahi kupaki gari mle ndani kwa wiki moja niliimba alelele…bado kuna ujinga kwamba aliepanda ndege ana hela sana,dhana potofu na ya kipumbafu
 
UBBER ZINWVIBAOO VYARANGI YA BIASHARA...RAHISIIKUJUAA..HAPAASHIDAA ZILETAX ZAWAH PALENDANI KYRUHUSU N KULAZAWATOTO NA CHOOKILAINI EBO..JIPANGENI
 
Mi nikishuka zangu natoka nje Puma pale nakula bodaboda hadi nilikopaki gari fresh,niliwahi kupaki gari mle ndani kwa wiki moja niliimba alelele…bado kuna ujinga kwamba aliepanda ndege ana hela sana,dhana potofu na ya kipumbafu
Tanzania kila kitu ni shaghala baghala! Nchi nyingine hii service ya kuacha magari airport ni nzuri na ya uhakika. Wanachaji fee ya kueleweka na huduma ni ya kuaminika.
 
Back
Top Bottom