Nyerere International Airport yawa ya pili kwa idadi ya abiria Afrika Mashariki

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,738
15,211
Dar es Salaam. Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, umeshika nafasi ya pili kati ya viwanja vilivyopo ndani ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa kusafirisha abiria wengi mwaka 2019.

Taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inaonyesha kuwa abiria milioni 4.472 walitumia uwanja huo mwaka 2019, huku ukiishinda viwanja vya ndege vya Entebbe, Kigali na Bujumbura.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata ndiyo ulioongoza kwa kusafirisha abiria wengi kuliko viwanja vyote Afrika ya Mashariki.

Zaidi ya abiria milioni 9.147 walipitia katika uwanja huo, idadi ambayo ni karibu mara mbili ya abiria waliopitia viwanja vinne vya ndege vilivyopo ndani ya umoja huo.Mbali na Tanzania, uwanja wa ndege wa kimatifa wa Entebbe ulipata abiria milioni 2.008, Kigali abiria milioni 1.144 na Bujumbura abiria 257,806.

Ili kushindana na uwanja wa Jomo Kenyata, Dk Abel Kinyondoa alishauri uwanja wa ndege wa JNIA utengenezwe na kuwa ‘HUB’ badala ya kuwa tu uwanja wa ndege wa kimataifa ambao watu wanautumia kuja nchini pekee.

“Jomo Kenyata wanapata abiria wengi kwa sababu uwanja wao ni kama Hub yaani mtu akifika pale anaweza kupata ndege za moja kwa moja kwenda mataifa mbalimbali duniani,” alisema.

Advertisement
Mchumi na mtafiti mwandamizi, Profesa Samwel Wangwe alisema kupungua kwa safari za ndege kunapaswa kufanyiwa utafiti ili kujua sababu ili itatuliwe jambo litakalofanya safari hizo kuongezeka badala ya kupungua.

Chanzo: ======

My take:
Kama nchi ya Tanzania tungefuata ushauri wa Zito Kabwe, Tundu Lissu na Chadema kwa ujumla wa kupinga ununuzi wa ndege na ukarabati wa terminal three, hao abiria wangehudumiwa na kupita uwanja upi?

Ifike mahali watanzania tuikatae Chadema kama tulivyowakataa kwenye uchaguzi mkuu vizazi vyote maana Chadema ni laana kwa taifa letu.
 
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tanzania (JNIA) kwa mwaka 2019 umesafirisha abiria millioni nne na kuwa wa pili Afrika mashariki nyuma ya Jomo Kenyata international Airport ya Kenya uliosafirisha abiria million tisa.
Loooo, bado tupo nyuma kiasi hiki. Hata nusu hatufikii?
 
Kabla ya jembe Magufuli tulikuwa na abiria million moja tu
1607063532531.png
 
Weka Takwimu zako vizuri.

Halafu siyo suala la kuwa wangapi katika kusafirisha abiria, vipi hebu weka faida ni kiasi gani pato la taifa limeongezeka.
 
What a shame!
Yaani pamoja na kutokuwa na lockdown bado tunazidiwa na waliokuwa na lockdown??!!
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Miaka yote walikuwa wanahudumiwa kwa kupitia uwanja gani kwani,yaani Jomo inaizidi ya Tzn mara 2 na chenji juu afu unakuja kujisifia? Uwanja wa Dar uwe unashindanishwa na uwanja wa Moi Mombasa,afu kwa wenzetu huku percentage kubwa ya wasafiri ni raia wao wakitafuta pesa duniani wakati huku bongo ni watalii na wageni wengine ,wazawa tunakula mihogo na madafu pesa hakuna
 
Sijawahi KUZIAMINI takwimu za SELIKALI YA KISHETANI ZIMEJAA UONGO NA ULAGHAI.

SHETANI MUONGO SANA.
 
Kwahiyo! Wanaotoka nchi za nje wanaletwa na ATCL! Utakuwa ujauzito umekushika usiku wa kuamkia leo.
Ukiambiwa Dream liner inaenda nchi za nje moja kwa moja huwa unaelewa nini?

Lofa mkubwa wewe
 
Ukiambiwa Dream liner inaenda nchi za nje moja kwa moja huwa unaelewa nini?

Lofa mkubwa wewe
Nenda uwanja wa ndege utaikuta inalalia, ndege ilikuwa inarudi na abiria chini ya kumi! Usishabikie kitu ambacho haukijui na haujaipanda hiyo ndege yenyewe, ujauzito unakutia hasira ila ukiushusha mzigo utatulia.
 
Nenda uwanja wa ndege utaikuta inalalia, ndege ilikuwa inarudi na abiria chini ya kumi! Usishabikie kitu ambacho haukijui na haujaipanda hiyo ndege yenyewe, ujauzito unakutia hasira ila ukiushusha mzigo utatulia.
Wewe ni Joyce Mkuya nyumba ndogo ya Mbowe una hasira ya kukosa ubunge wa viti maalum.
 
Back
Top Bottom