Nini maana ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (International Airport)?

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,720
10,220
Unapoongea kuhusu kiwanja cha ndege cha kimataifa (InternationalAirport) ni pamoja na kituo cha forodha na uhamiaji.

Hapa abiria wanaweza kuingia au kutoka nje ya nchi kupitia ndege za moja kwa moja au zinazounganisha.

Kumbuka Uwanja wa ndege wa kimataifa pia unaweza kutumika kwa ndege za ndani kwa kutenga taratibu maalumu katika miundombinu husika.

Viwanja vya ndege vya kimataifa vinaweza kuwa na huduma tofauti kulingana na nchi ingawa vingine hufafanuliwa na hadhi ya viwango fulani vya anga, ingawa bado vitu vya msingi ni lazima kuwe na forodha, vituo vya ukaguzi wa usalama na kituo cha uhamiaji ndani ya kiwanja ili kuweza kuhudumia abiria na mizigo kutoka nchi nyengine.

Tofauti na viwanja vya ndani (Domestic Airports), viwanja vingi vya ndege vya kimataifa mara nyingi vina kituo cha ushuru, sehemu za kupumzika, sehemu za kusubiri, ofisi za kampuni ya ndege, vyumba vya huduma za dharura, vyumba vya ibada au ofisi za utalii n.k

Pia viwanja vya ndege vya kimataifa mara nyingi ni vikubwa kuliko viwanja vya ndege vya ndani na vinajumuisha miundombinu yenye kuweza kuhudumia ndege tofauti kutoka mataifa mengine.

Viwanja hivi vinajengwa kulingana na viwango vya kimataifa vya uwanja wa ndege vilivyoainishwa na Taasisi ya kimataifa ya mashirika ya usafiri wa anga 'IATA' na shirikisho la kimataifa la usafiri wa anga 'ICAO' na nambari zake hufafanuliwa pia katika viwanja husika.

Kiwanja cha ndege cha ndani (Domestic Airport) huwa kinahudumia ndege za ndani ya nchi tu pasipo kujali ukubwa wala uzuri wa miundombinu yake.

Mfano wa viwanja vya ndege vya kimataifa ni kama vile JuliusNyerere (JNIA), Kilimanjaro (KIA) na AmaniAbeidKarume (AAKIA)

Ndege hasa za abiria kutoka nchi nyengine huwezi kukuta inatua katika kiwanja cha ndani (Domestic) isipokuwa kwa dharura, mipango au shughuli maalum za serikali/diplomasia au mizigo ambapo uhamiaji na maafisa wengine pia hujipanga kwa muda kutoa huduma.

1684990272834.png
 
Back
Top Bottom