Kwanini uandae shamba kabla ya kupanda mazao?

Jesusfreak08

JF-Expert Member
Jul 20, 2019
823
1,797
Habari yako
Naamini unaendelea vizuri na kama haupo vizuri basi MUNGU afanye wepesi kwaajili yako.

Karibu tujifunze pamoja

Kwenye kilimo kuna mambo mengi sana ambayo huchangia sana katika mavuno baadae ikiwamo kuandaa shamba kuchagua mbegu,kutunza shamba na kulinda shamba .

Miongoni mwa mambo hayo jambo la muhimu na lakuzingatia kabla ya chochote katika shamba lako ni KUANDAA SHAMBA hili ni jambo kuu na la kwanza kwa maneno mengine hili ni msingi kabisa.

Hili ni msingi Kwasababu taratibu zote zinafuata baada ya hii ya uandaaji hutegemea sana hii hatua ya kwanza na hatua hii ya kwanza inaweza kuleta urahisi kama ikifanywa vizuri au ugumu kama ikifanywa vibaya

Hebu tuangalie faida kadhaa kama ukifanya vizuri

1. Utaweka mazingira mazuri ya mbegu yako kukua vizuri kwa kuwa udongo utakuwa umeandaliwa vizuri kwaajili ya kuoteshwa mbagu utakuwa na kila sifa ya kuusaidia mmea kukua

2. Utaweka urahisi wakati wa kupanda ,udongo ulioandaliwa vizuri ni rahisi pia wakati wa upandaji tofauti na udongo usio andaliwa

3. Utaepusha ukuaji wa magugu kwa haraka,kwasababu huwezi kuandaa shamba bila kuondoa magugu kwaiyo utaweza kuepusha magugu hayo kukua kwa haraka

4. Utaweka mazingira mazuri ya kutokuwa na wadudu hatarishi kama panya ,nyoka n.k kwasababu mazingira yenye vichaka ni makazi mazuri ya hawa wadudu kama mazingira hayo yakiondolewa au kuchomwa moto basi wadudu hao hutoweka pia

5. Kuwepo kwa urahisi wakati kupanda mbegu zako,eneo liliandaliwa vizuri halichukui nguvu nyingi sana wakati wa kupanda kwasababu ya mazingira yameandaliwa vizuri

Kama usipoandaa shamba vizuri.
1. Utatengeza mazingira magumu kwa mbegu kuota ,kuwepo na magugu ambayo yatatinga mimea kwa kunyang'anyana chakula ,kuwepo kwa ardhi ngumu isiyo weza kusaidia mbegu kukua vizuri kwasababu ya kukosa kuandaliwa vizuri.

2. Utakaribisha wadudu hatarishi kuwepo kwa vichaka visivyo safishwa vizuri ni mwanzo wa kuakaribisha wanyama hatari kwa mazao na hata kwako pia

3. Ugumu wakati wa upandaji ,mazingira sio rafiki kwaajili ya upandaji inapelekea kutumia nguvu nyingi wakati wa kupanda mfano kutoa magugu wakati wa kupanda kwasababu ya eneo kutosafishwa vizuri.

4. Kuongeza gharama zinazoepukika kwa mfano kununua mbegu tena sehemu ambazo mbegu hazijafanikiwa kuota.

Ni vizuri kuandaa shamba anza vizuri ili umalize vizuri na upate mavuno mazuri.
 
Back
Top Bottom