Kabla hujaanza kulima, mkulima hebu zingati yafuatayo

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
1)Eneo shamba lilipo
Kabla hujaanza kulima zao lolote, hebu kwanza angalia mahala shamba lako liipo. Je linafaa kwa kilimo au kulima zao ambalo unataka kulilima. Katika eneo lako hebu zingatia yafuatayo:-
  • Aina ya udongo sio kila udongo una uwezo wa kusapoti kila aina ya zao lililopo shambani. Kuna baadhi ya mazao hayahitaji udongo unaotuamisha maji kabisa na mengine huwezi kupanda kwenye udongo usiotuamisha maji. Mfano huwezi kupanda ufuta kwenye udongo wa mfinyanzi na mpunga kwenye udongo wa kichanga.
  • pH ya udongo kitu ambacho wakulima wengi huwa tunafeli ni kulima lima hovyo mtu ananunua eneo au anakodi eneo halafu anapanda hovyo zao lolote bila kujua pH ya udongo kwa ufupi sio kila zao linafaa kwenye kila aina ya udogo.
  • Kiwango cha chumvi chumvi na madini mengine kwenye udongo hiki kitu watu huwa wanakipuuzia sana japo kina umuhimu mkubwa sana hasa kwenye swala zima la umwagiliaji na utumiaji wa mbolea za viwandani.
  • Chanzo cha maji eneo jirani na shamba lilipo kabla hujaanza kulima hebu angalia je maji yapo karibu ili hata mvua zikikosekana uweze kumwagili mazao yako kwa urahisi na haraka ili usipate hasara.
  • Kufikika kwa urahisi wapo baadhi ya wakulima wamepata hasara sababu tu ya kushindwa kutoa mazao yao shamba na kuyapeleka sokoni kwa wakati sababu ya ubovu wa barabara na kwingine hata hizo bara bara hazipo kabisa na hakuna usafiri unawea ukafika shambani.
2)Uandaji wa shamba
Kabla hujaandaa shamba zingatia yafuatayo
  • Kuondoa visiki kama shamba ni jipya
  • Kuondoa mawe na vitu vingine visivyooza
  • Kuandaa matuta na vitalu kama vitahitajika
3)Uchaguzi wa mbegu bora
Chagua mbegu kuendana na mahitaji yako, Chagua mbegu zinazozaa kwa muda mfupi na zinazostahimili ukame, Chagua mbegu zinazoweza kustahimili magonjwa.

4)Upandaji na utunzaji wa mazao
Kila zao lina kiwango chake cha uhitaji wa mbolea uvumilivu kwa maginjwa na wadudu hivyo basi baada ya kupanda hakikisha unautunza mmea wako shambani kadri itakavyohitajika palilioa kwa wakati pulizia dawa za magonjwa na wadudu kwa wakati weka mbola kwa wakati .
Jitahidi kutembelea shambani kwako mara kwa mara ili uweze kujua na kufatilia hali za mazao yako kwa ukaribu hii itafanya iwe rahisi kudhibiti magonjwa na wadudu hatarishi shambani.

5)Uvunaji na utunzaji wa mazao
Vuna mazao yaliyokomaa na kukauka vizuri hakikisha unatunza mazao yako vizuri ili yasiadhiriwe na wadudu hadi kupelekea kupunguza ubora wake.

KUMBUKA
`KILIMO HUANZIA SOKONI NA KUISHIA SOKONI NI BORA KUJUA SOKO HALISI NA LA UHAKIKA KWA MAZAO YAKO KABLA HUJALIMA ILI KUEPUSHA HASARA ZINAZOWEZA KUEPUKOKA

33
 
Pia kuzingatia iwapo kutahitajika ulinzi wa wanyama na ndege waharibifu Kama vile ngedele, nyani , tumbili n.k

Shamba zuri ni la katikati.
 
Je Wafanyakazi utapata maeneo ya karibu na shamba au itabidi watoke mbali?

Bajeti za chakula , nauli , malazi n.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom