Kwanini tunaogopa sana wazungu?

Kwanini tunaogopa sana wazungu?

Wazungu sio watu wa kuogopwa hata kidogo,ni watu tu kama watu wengine tofauti yetu ni rangi tu

Huyu alikutawala akakufanya mtumwa akakubeba kama gunia la mihogo mpaka kwenye mashamba yao huko akakulimisha kwa viboko bila ujira..mtu mweusi ana haki na kila sababu ya kumuogopa mzungu..usijidaganye kama tupo sawa..mzungu ni wa kuogopwa tu na mtu mweusi akiamua anakufanyia kitu mbaya utake usitake
 
Hili ndilo shamba la bib yaan Africa!! Wana chukua malighafi! Kwa bei chee Kisha wana kuletea, magari ,Mashinne na mitambo mbali mbali! Kwa bei wanayotaka wao. Wamekuletea teknolojia nzur uli uwe soko lao, kama vile haitoshi wakatengeneza na ukimwi!! Ulio tishio kwetu ! Kisha Arvs!!!!
Hatishi bwana mzungu ni ndugu yetu wewe jidanganye!!

Una nn wewe mpaka uwe na ujasiri!
Kamuulize mugabe nchi yake ilikuwa ya pili Dunia kwa uchumi enzi hizo iliitwa South Rhodesia!!! Ilikuwa ndio kapu la Africa kwa kuzalisha chakula!
Wako wapi Leo kiuchumi baada ya kuwatimua wazungu, ili watu weusi wafaidi mashamba yao? Sasa hivi Zimbabwe ni nchi ya nne kwa umaskini duniani!
Kwa kifupi ni kwamba kujiamn kwa yule mzungu wa jana hata akaamua kuja anajua kisheria hamta muweza wala hakuna atakacho walipa kikiwa nje ya mkataba tulio ingia naye!!
Kama tuliwatuma wawakilishi wetu ambao wamekuwa wapumbavu! Hiyo haimuhusu mzungu wa watu, kama uli saini basi itakula kwako!! Watch and learn!!![emoji102]
 
Ninachoangalia si kuja wala kutokuja ila kwa nini tunaona wanaweza tufanya kitumbaya? Maana wengi tuliona kuna vitisho vingi sana.
CCM na serikali yake ndiyo wanaowaogopa wazungu. Kubwa la wezi toka Canada limekuja lakini likaishia kupigwa kiyoyozi Ikulu badala ya kukamatwa. Ccm ni janga la taifa
 
Ninachoangalia si kuja wala kutokuja ila kwa nini tunaona wanaweza tufanya kitumbaya? Maana wengi tuliona kuna vitisho vingi sana.
Kwa sababu uwezo wa wengi kufikiri hapa nchini ni mdogo ( kwa mujibu wa tafiti ya Twaweza) hamna anayeona kama wameshawafanya kitu mbaya. Mngekuwa mna maono ya mbali mngeshajua kuwa hao wazungu wameshawaona nyie wapiga kelele tu msio na mbinu yoyote ya kuwashinda.

By the way kuna chochote ambacho mmesha achieve mpaka sasa? Au kufungia gazeti ndiyo achievement? Au kupiga maruufuku JK na Mkapa wasitajwe? Na hata ule mchanga pale bandarini mtauachia tu. Ni suala la muda.

Wengi wanaunga mkono juhudi za kuzuia wizi unaoendelea kwenye sekta ya madini ila wenye akili wanapingana na approach yenu ya kisanii.

Cha msingi Wekeni mikataba yote ya madini mezani ipitiwe upya na sheria zote za madini na gas zibadilishwe kwa manufaa ya nchi. Vinginevyo mtaendelea kupiga picha na wazungu ikulu na kuwazuga wajinga tu ambao tafiti za Twaweza zimethibitisha pasi na shaka kuwa ndiyo wapiga vigelegele wenu
 
JIBU NI MOJA NA NI FUBI,SABABU YA MWAFRIKA KUMUOGOPA MZUNGU NI KWA SABABU YA "MWAFRIKA KUFANYWA KTK BIASHARA YA UTUMWA"MPAKA LEO HII SAIKOLOJIKALI INAMSUMBUA MWAFRIKA KUANZIA VIONGOZI WETU HADI WSTU WA KAWAIDA....

PERIOD...

OVA
 
Huyu alikutawala akakufanya mtumwa akakubeba kama gunia la mihogo mpaka kwenye mashamba yao huko akakulimisha kwa viboko bila ujira..mtu mweusi ana haki na kila sababu ya kumuogopa mzungu..usijidaganye kama tupo sawa..mzungu ni wa kuogopwa tu na mtu mweusi akiamua anakufanyia kitu mbaya utake usitake
Wazungu walifanikiwa kutawala Afrika kwa msaada wa machifu wa kiafrika,bila kupewa msaada na wa afrika wenzetu wazungu wasingefanikiwa kununua kuuza binadamu wala kutawala Afrika

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
 
Maada iko wazi sana. Ni wazungu na sisi Waafrika hasa Tanzania.

Na pia nimeeleza jinsi ya wabunge walivyoonyesha kuogopa wazungu.

Hizo za akina JK na Magazeti si sehemu yake.
Kwa sababu uwezo wa wengi kufikiri hapa nchini ni mdogo ( kwa mujibu wa tafiti ya Twaweza) hamna anayeona kama wameshawafanya kitu mbaya. Mngekuwa mna maono ya mbali mngeshajua kuwa hao wazungu wameshawaona nyie wapiga kelele tu msio na mbinu yoyote ya kuwashinda.

By the way kuna chochote ambacho mmesha achieve mpaka sasa? Au kufungia gazeti ndiyo achievement? Au kupiga maruufuku JK na Mkapa wasitajwe? Na hata ule mchanga pale bandarini mtauachia tu. Ni suala la muda.

Wengi wanaunga mkono juhudi za kuzuia wizi unaoendelea kwenye sekta ya madini ila wenye akili wanapingana na approach yenu ya kisanii.

Cha msingi Wekeni mikataba yote ya madini mezani ipitiwe upya na sheria zote za madini na gas zibadilishwe kwa manufaa ya nchi. Vinginevyo mtaendelea kupiga picha na wazungu ikulu na kuwazuga wajinga tu ambao tafiti za Twaweza zimethibitisha pasi na shaka kuwa ndiyo wapiga vigelegele wenu
 
Wazungu walifanikiwa kutawala Afrika kwa msaada wa machifu wa kiafrika,bila kupewa msaada na wa afrika wenzetu wazungu wasingefanikiwa kununua kuuza binadamu wala kutawala Afrika

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app

Kwa msaada? Mzungu aliwezaje kufika huku africa?..aliona nini?..eti msaada..mzungu akili nyingi wewe usifananishe na akili za machifu waliorubuniwa kwa vitu vya kijinga
 
Kwa msaada? Mzungu aliwezaje kufika huku africa?..aliona nini?..eti msaada..mzungu akili nyingi wewe usifananishe na akili za machifu waliorubuniwa kwa vitu vya kijinga
Mzungu aliwezaje kufika Afrika? Afrika ni sehemu rahisi sana kufikika,toka bara la ulaya hadi afrika ni utofauti wa umbali wa kilometa chache sana hazizidi hata kilometa 400,kutoka Gibraltar moroko hadi Spain ni sawa umbali wa Dar hadi Zanzibar tu,kwa miaka mingi sana wa Afrika walikuwa wanaishi Ulaya pia kabla hata ya ukoloni,makabira ya kiafrika jamii za moors na Berbers walikuwa wanachangamana na wazungu kwa kipindi cha miaka zaidi ya 5000 iliyopita.
 
Unaulizwa swali ambalo jibu lake obvious! mfano mzuri tu angalia hata siku ile prof.John nani nani yule aliyetoka Canada na ndege binafsi, yaani amepanga safari siku ile ile na akakaribishwa mpaka ikulu bila hata kusubirishwa.

Kama mngekuwa hamuwaogopi Magufuli alitakiwa kumuonyesha jeuri siku ile ile kwa mwambia kuwa "Leo sina muda wa kuonana na wageni, nina majukumu mengine hivyo naomba uje siku nyingine".

Kwa kufanya hivyo ingeonesha kweli hatuna fear yoyote ile dhidi ya wazungu hasa kwenye mali zetu, lakini kitendo alichokifanya Magufuli cha kuhairisha ratiba zake za siku hiyo na kumkaribisha ikulu huku akimsifu kuwa jamaa ni mwanaume, naamini yule mzungu alimdharau sana.
 
Back
Top Bottom