Kwanini tunakimbilia India kwa Tiba?

Huduma zetu za afya ni hafifu ... kama wale wanaositahiri kuziboresha huduma za afya hapa kwetu kujenga mahospitali makubwa kwa ajili ya huduma mbalimbali wanakimbilia India sisi tufanyeje tena ?

Ha ha haa! Umenikumbusaha jana Nilikuwa nacheki Taarifa ya Habari nikaona Wanafunzi Shule ya Musoma Sekondari wanaharisha damu kutokana na Mazingira Mabovu yau ukosekanaji wa maji, Vyoo nakadhalika! Wakaonyesha vile vyoo kwa kweli niliumia sana
 
attachment.php
 
that was and still is my worry.. wanaharibu vya kwetu ili walete vya kwao kwa kutumia vyetu!

teh teh teh
mzee mwanakijijiji nifafanulie una maanisha nn hapa . sijui oxgen kwenye ubongo wangu hauzunguki vizuri hapa bado najaribu kudadavua na sijaelewa
 
Mimi nimekaa India na nina ifahamu kwa kiasi fulani na wagonjwa wengi wanaopekwa huko ni baada ya magonjwa yao kuwa jameshindikana hapa Tanzania na sababu huwa ni vifaa na madaktari.
Kiukweli watanzania tuna matatizo sana katika suala la utaalamu si wa kitabibu tu hata wahandisi na technolojia kwa ujumla.maana hata ujenzi wa barabara si wataalamu wote wanatoka nje.sasa tujiulize na hilo!
Nenda pale Apollo Hyderabad hadi wahudumu wa Kihindi sasa wanajua kiwahili maana ndo wangojwa wanao wahudumia kila kukicha.
Na kwa mwaka huu ukienda Apollo Hospital pale Hyderabad au Ahmedabad utakuta watanzania ni wengi kuliko wageni wote wanaofika India kwa matibabu.
Na Tanzania ni nchi inayotajwa kuwa ni wateja wakubwa wa Apollo Hosptials India,kwa ushahidi bofya hapa:

http://www.apollohospitals.com/hosp...-installed-at-apollo-hospitals-hyderabad.html

watanzania tunabidi tujiulize wapi tunaelekea maana ni aibu.
 
tuanakimbilia India kwa matibabu kwa sababu madaktari wetu wavivu wakufanya kazi.
nasema hivyo kwasababu moja kubwa, mie tangu ule mkasa wa mtu kupasuliwa kichwa badala ya goti , na goti badala ya kichwa , ikanifanya niamini kweli nnchi hii hatuna madaktari ila tunawauguzi watupu.
inakuwaje umfanyie tiba ya upasuaji wa makosa mgonjwa kisha unapogundua umekosea unashindwa kumrudishia ulivyomkuta ?
walimkosea yule mgonjwa wa goti wakampasua kichwa, kisha wakakuta haumwi chochote kwanini wasikirudishie kamam walivyokikuta ?
mfano fundi wa gari akifungua kitu fulani kisha akashindwa kukirrudishia naamini imani yako kwake itapotea kabisa, hii ni sawa na madaktari wetu hapa TZ.
Mengine ya mazingira duni , hospitali zisizo na vifaa ni nyongeza.
 
Nilkuwa India karibuni kwa matibabu, self paid!!!
Afya ya mtu si mahali pa pata potea if you are serious with your health.Kama una fanya kazi basi unafanya hivyo kwa vile you are healthy.
Sekta ya afya nchini imezorota sana na si siri katika miaka 20 iliyopita.
Madaktari wanaingia mgomo, wahudumu vilevile.
Nenda Mwanyanyamala at your own risk!!
Katika siku ya leo ambapo unaweza katwa kichwa badala ya operation ya mguu is a serious problem.Tena very serious kwa Hospitali kuu nchini, MNH, Muhimbili Medical Centre.
Mgonjwa wa akili anaua wagonjwa wenziwe wodini!
Madaktari na matibabu karibu wote hawalipwi vizuri na wana miradi yao ya pembeni, concentration kazini hakuna.Daktari atafanya operation akifikiria ukata uliopo nyumbani.
Katika scenario hii mkuu MKJJ ukijipeleka Muhimbili ukiwa na kauwezo ka kujilipia , then you are not serious with your health.
Najua vizuri kuwa kupelekwa katika hospitali zetu kwa wakati mwingine ni jambo ambalo haliepukiki lakini nawahurumia sana wazalendo wenzangu.

Tufanye taratibu ku-subotage matibabu katika hizo hospitali huko nje ya nchi (kokote kule) ya wale wote wanaochota (maana hakuna kulipiwa, we can't afford it now) fedha za Taifa wakienda huko nje ya nchi. Kila sehemu huko nje ambako mlalahoi atakuwepo, kwa mfano kwenda kumtembelea na kumkashifu (kama wanavyokashifika wagonjwa wetu nchini kimatibabu) huko huko aidha kwa maandamano au individually. Na demand ni lazima iwe wazi kwamba "NI LAZIMA ARUDISHWE AKATIBIWE MWANANYAMALA, MUHIMBILI AU BUGANDO, kama sio Peramiho au Lindi, as simple as that. Ipi ni jinai zaidi baina ya hii na ufisadi???? Kama ni hii, basi I drop my case, lakini ufisadi ndio kichwa cha matatizo yote, umasikini, kurudi nyuma kimaendeleo, chuki na vijiko baina ya watu, nk, kwa kifupi ni uvundo. Kama atakatwa kichwa badala ya mguu, akipigwa sindano kwenye tundu ya haja kubwa badala ya takoni, shauri yake, nyumbani. Any life is sacred, we all deserve proper healthcare and the means we have are for all, not some.

Na katu hayatotokea hayo, na wanajua hivyo. Badala yake ulazima wa kuyashughulikia maslahi ya madaktari, wahudumu, na wengineo katika sekta ya afya nchini watayapa kipau inavyostahili badala ya "ufisadi" ambayo itasaidia kuboresha mapenzi, hamasa na ufanisi wa kazi zao katika kuwahudumia kwa awali kabisa wao wenyewe viongozi na kwa mapana na marefu ni kwa sisi sote wananchi. Hii kwa mtazamo mrefu itasaidia maendeleo ya sekta husika, kwa maana kama ni gunea pigs katika medical experimentations, basi sote ni guinea pigs, isitoshe ni yupi guinea pig mzuri kwa medical experimental research, fisadi aliyeshiba au mlalaho mwenye njaa???

Ni haramu kumfanyia hivyo aliyejigharimia mwenyewe bila ya pesa za ufisadi kwa maana utajiri ni kitu kitakatifu na ni dhamana na mtihani wa yule aliyemchagua Mwenyezi Mungu kumpa, autumie vizuri umuokoe na moto na autumia vibaya umsukumize motoni. Tajiri bora katika hili ata hand-pick na kuongozana na wagonjwa walalahoi wenye matatizo sawa angalau wawili au watatu, hii ndio kufuzu mtihani wa kupewa utajiri, utaendelea kufanya hivi mpaka moyo huzoea kiasi cha kutoweza kutulia bila ya kufanya hivyo na huku utajiri ukiongezeka, maana mtoaji ni Mwenyezi Mungu (SW). Lakini mafisadi viburi are worst of cteatures, filthy.

Natoa hoja.
 
Mmeongea vitu vya maana. Tatizo ni maslahi duni kwa matabibu wetu. Ujuzi pia unaonyesha vitu vinavyoendeshwa kiuma ni uozo mtupu. Hakuna uwajibikaji. Muhimbili madokta wanaiba wagonjwa na kuwapeleka kwenye zahanati zao. Mi mmojawapo kuibwa. Nadhani ni mpango wa siri wa serikali na wafadhili kuzorotesha sekta kama ya afya, kilimo, na elimu. Inashindikana vipi kumpa dokta sh. 1.5m wakati anaiba zaidi ya hizo kupitia madawa na kuiba wagonjwa? Nani asiependa kuridhika? Ukimpa daktari hela nzuri hatajisumbua kuhangaika na vizahanati, dawa hazitaenda huko... Mambo ni mengi
 
Kwanini huyu ndugu yetu ambaye amekuwa akitafuta wawekezaji kote duniani hajapata wawekezaji (siyo wahisani) wa kusaidia huduma ya afya?

a. Wawekezaji ambao watasponsor kufundisha madaktari wetu kwenye vyuo vyetu katika specialities mbalimbali?

b. Wawekezaji ambao wataleta vifaa vya kisasa kuupgrage our aging ones?

c. Wawekezaji ambao wataona kuwa ilipo Hospitali ya Muhimbili sasa hivi pamepitwa na wakati na kutusaidia kujenga the New Muhimbilli Healthy Systems badala ya kuongeza majengo na kupaka rangi mpya. Hiyo Muhimbili ilivyo sasa ibakie kuwa a true Medical Teaching University..

d.
 
Mmeongea vitu vya maana. Tatizo ni maslahi duni kwa matabibu wetu. Ujuzi pia unaonyesha vitu vinavyoendeshwa kiuma ni uozo mtupu. Hakuna uwajibikaji. Muhimbili madokta wanaiba wagonjwa na kuwapeleka kwenye zahanati zao. Mi mmojawapo kuibwa. Nadhani ni mpango wa siri wa serikali na wafadhili kuzorotesha sekta kama ya afya, kilimo, na elimu. Inashindikana vipi kumpa dokta sh. 1.5m wakati anaiba zaidi ya hizo kupitia madawa na kuiba wagonjwa? Nani asiependa kuridhika? Ukimpa daktari hela nzuri hatajisumbua kuhangaika na vizahanati, dawa hazitaenda huko... Mambo ni mengi

mkuu,samahani natoka nje ya mada kidoogo,hivi mshahara wa daktari ni kiasi gani?? dakatari mzoefu sio yule anaeanza kazi kwani naamini muhimbili kumejaa wazoefu ikiwemo maprofessor wanaotibu na kufundisha palepale.
 
Madaktari hawathamini wagonjwa. Mama yangu alikuwa anamatatizo ya moyo, kila akipewa appointment Muhimbili anakaa kumsubiri daktari hata masaa sita, daktari akitokea anaona wagonjwa watatu anasema wengine wapewe tena appointment after waiting for 6 hours!!! mara nyingine daktari hatokei kabisa!!! I cannot remember the name of the doctor nikilikumbuka nitaliweka
 
mkuu,samahani natoka nje ya mada kidoogo,hivi mshahara wa daktari ni kiasi gani?? dakatari mzoefu sio yule anaeanza kazi kwani naamini muhimbili kumejaa wazoefu ikiwemo maprofessor wanaotibu na kufundisha palepale.

sheme za mabingwa zitakuwa juu vya kutosha, tatizo hawawezi kuacha zahanati zao kwani walizianzisha wakiwa na mishahara midogo. Besides, mabingwa wapo wachache kitu kinachosababisha kugombewa pia na hospitali zilizopo. Tabu ni kwa hawa madaktari wanaoanza kazi. Wakiwa na maslahi madogo wataishia kama mabingwa. Ili kuzuia hili, scheme zao ziwe za kuridhisha ili watulie kwenye vituo vyao vya kazi
 
watu wengi wanaoweza kumudu gharama za matibabu wanakimbia muhimbili,sababu ni huduma mbovu,kinachosababisha huduma mbovu kila mtu anakijua,u dont have to be a brain surgeon,hao ma-dr wasisingizie mishahara midogo hata wakipewa tsh 10million ni yaleyale tu kwani wanaochukua rushwa wote hawana shida kama tunavyodhani, tra mishahara mikubwa huduma zao mbovu kama wangekuwa madr wale hamna hata mgonjwa angeenda pale, WATANZANIA TUMELOGWA NA ALIYETULOGA AMEKUFA.
 
sheme za mabingwa zitakuwa juu vya kutosha, tatizo hawawezi kuacha zahanati zao kwani walizianzisha wakiwa na mishahara midogo. Besides, mabingwa wapo wachache kitu kinachosababisha kugombewa pia na hospitali zilizopo. Tabu ni kwa hawa madaktari wanaoanza kazi. Wakiwa na maslahi madogo wataishia kama mabingwa. Ili kuzuia hili, scheme zao ziwe za kuridhisha ili watulie kwenye vituo vyao vya kazi

unaona sasa hapo kwenye red,hio ni ukosefu wa professionalism na selfishness,tatizo sio mshahara wanaposho kibao hao watu.
 
mimi binafsi nishakwenda muhimbili 10yrs ago wakataka kunifanyia operation fulani,on top of that surgeon akataka apewe tsh 80,000 ili iwe "fast track",wazee wangu wakakataa nikaenda nje ya nchi wakaniambia hilo tatizo litaisha taratibu(nilipewa dawa) baada ya muda fulani kweli likaisha,through hii experience do you think nitakuwa na imani kupeleka mtoto wangu muhimbili???
 
mimi binafsi nishakwenda muhimbili 10yrs ago wakataka kunifanyia operation fulani,on top of that surgeon akataka apewe tsh 80,000 ili iwe "fast track",wazee wangu wakakataa nikaenda nje ya nchi wakaniambia hilo tatizo litaisha taratibu(nilipewa dawa) baada ya muda fulani kweli likaisha,through hii experience do you think nitakuwa na imani kupeleka mtoto wangu muhimbili???

Hili ni tatizo lingine, kuna Hospitali zengine wanaweza kukufanyia operation ambazo hauhitaji, ili mradi wapate hela.
Yaani wanakupasua, kisha wanakurudishia, mambo ya ajabu kweli!
 


Benno Ndulu ana swimming pool kwake,na nyumba iliyofanyiwa ukarabati wa billions of Shillings!
T U M E LO G WA NA K U LA A NIWA!
Tunamchukia Mzungu,lakini at least Mzungu anajali Mzungu mwenzake!
Ndio maana Kuna Eropean Union,nchi za Magharibu zimeamua kuwasaidia watu wa East toka ukoministi.
 
Waheshimiwa wabunge wangetusaidia sana kuhakikisha hizi hospitali zetu zinaboreshwa. Lakini inasemekana na wao wako entitled kutibiwa nje !!
 
Back
Top Bottom