Kwanini tunakimbilia India kwa Tiba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tunakimbilia India kwa Tiba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 11, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kwa muda mrefu sasa nimeanza kuona mambo fulani makubwa mawili yakitokea inapokuja huduma ya afya.

  a. Magonjwa mbalimbali ambayo awali yaliweza kutibiwa katika hospitali zetu yanaanza kupelekwa India. Mtu kamwagiwa tindikali anapelekwa India, mtu anaumwa meno anapelekwa India, mtu kavunjika mguu hadi aende India. Nakumbuka zamani kubwa ilikuwa ni masuala ya moyo. Sasa hivi imefikia hata regular check up inafanywa India, japo zamani tulikuwa tunakimbia hata Nairobi na kwa sisi wengine tunaenda Ndanda au Peramiho.. au hata Bugando. Tumefikaje hapa?

  b. Kwa kadiri ya kwamba tunaendelea kutafuta njia mbadala ya kupata tiba na hasa kwa kadiri ya kwamba tunaendelea kuwalipia watawala kwenda kufanyiwa check up na tiba ya magonjwa ya aina yote nje ya nchi, watu hawa hawatofikiria kamwe kuboresha huduma ya afya ya nchini na kuileta kwenye kiwango cha juu cha kimataifa. Zaidi ya yote wataendelea kufungua cliniki na vituo vya afya lakini hawatofikiria kuanzisha kitu kama National Children Hospital au kuigawanya Muhimbili kuwa Muhimbili Healthy Systems badala ya sasa walivyoifanya kuwa tu National Hospital (whatever this means!). Je, kwa kuendelea kuwalipia hawa kana kwamba ni "haki" hatuoni kwamba tumewapa kibali cha kufikiria suala la afya kwa Watanzania kama ni suala "letu" kuliko "lao" kwani wao hawana wasiwasi wapi watatabiwa na nani atawalipia wakiumwa?

  Je ipo haja ya kuangalia upya utaratibu wa kuwagharimia viongozi mbalimbali kwenda nchi kwa uchunguzi wa kawaida? Je, tukitaka uchunguzi wa kawaida wote ufanyike nchini yawezekana wakaona uharaka na ulazima wa kuupdate our medical and health facilities?

  Ni kwa namna gani suala la afya linaweza kuwa kwenye ajenda ya mwaka huu iili kuweza kuwalazimisha wanasiasa wetu waanze kufikiria hayo mambo mawili hapo juu na kutuongoza kuelekea mabadiliko ambayo yatabadilisha mwelekeo wa sekta yetu ya afya na kuiinua?
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Nilkuwa India karibuni kwa matibabu, self paid!!!
  Afya ya mtu si mahali pa pata potea if you are serious with your health.Kama una fanya kazi basi unafanya hivyo kwa vile you are healthy.
  Sekta ya afya nchini imezorota sana na si siri katika miaka 20 iliyopita.
  Madaktari wanaingia mgomo, wahudumu vilevile.
  Nenda Mwanyanyamala at your own risk!!
  Katika siku ya leo ambapo unaweza katwa kichwa badala ya operation ya mguu is a serious problem.Tena very serious kwa Hospitali kuu nchini, MNH, Muhimbili Medical Centre.
  Mgonjwa wa akili anaua wagonjwa wenziwe wodini!
  Madaktari na matibabu karibu wote hawalipwi vizuri na wana miradi yao ya pembeni, concentration kazini hakuna.Daktari atafanya operation akifikiria ukata uliopo nyumbani.
  Katika scenario hii mkuu MKJJ ukijipeleka Muhimbili ukiwa na kauwezo ka kujilipia , then you are not serious with your health.
  Najua vizuri kuwa kupelekwa katika hospitali zetu kwa wakati mwingine ni jambo ambalo haliepukiki lakini nawahurumia sana wazalendo wenzangu.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Lole Gwakisa.. thats is exactly the point.. the other side of the story kuna wengine ambao wameapa hawawapeleki ndugu zao India at all kwa sababu watu wanapukutika kiurahisi huko kama nini..
   
 4. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nadhani point kubwa na ya msingi ni kwa watala wetu kutibiwa katika hospitali za hapa nyumbani. Na hili litawezekana endapo serikalii itapiga marufuku watala kwenda kutibiwa nje ya nchi. (Kitu ambacho sidhani kama kitatokea hivi karibuni - sio kwa utawala uliopo)

  Inasikitisha sana kuona afya ya wananchi sio kipaumbele cha nchi kabisa! Sasa sijui hilo taifa litajengwaje kama matibabu ni duni kiasi hiki?! Gwakisa kaelezea vizuri sana kwann watu wanakimbilia nje ya nchi kutibiwa.
  Je kwa wasio na huo uwezo?

  This should not be an aption, things need to be worked out, na starting point ni kuwalipa madaktari vizuri!

  Ila sidhani kama watawala wanafikiria kama tunavyofikiria!

  I doubt!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Wenyewe wanasema wako "entitled".. sasa sielewi.. why? Nadhani wangehakikishiwa kama Watanzania wengine kuwa endapo kitu hakiwezi kuchunguzwa ndani ya nchi au hakuna mahali kinaweza kutibiwa basi watagharimiwa kwenda nje ya nchi... lakini sasa hivi tumefungua mlango tu..
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  baadhi ya sababu za kukimbilia india ni hizi hapa bila kufuata mlolongo

  PRIVACY=Kwa Mh Waheshimiwa nadhani wanajisikia huru kutibiwa na dk patel wa india au hindumandal badala dk lema au dk Juma wa muhimbili. Majukwaani wanasema tununue bidhaa za nyumbani??????

  INFERIORITY= wanasiasa wenyewe hawaamini wataalam wetu sasa donda hili limeshuka mpaka kwetu raia wa kawaida. Mtu akiwa na kidonda kidogo anataka kikafungwe muhimbili sio mwananyamala au temeke. Muhimbili ndio INDIA na SA yetu sisi wa kawaida

  OPPORTUNITY= wengine kuugua akiwa na nafasi fulanini opportunity ya kufanya safari kulipwa posho ya kimataifa ya kuugua, n.k. Sometime nahisi wabunge wanawaomba madaktari wao binfasi waandikie kuwa tatizo walilonalo linahitaji checkup zaidi nje. Kwa nn wasiwe wazalendo wakatumia taratibu zile zile walizokuwa wantumia kabla ya kuukwaa uongozi au madaraka.naamini na wabunge wamo humu kwa hiyo wamefumbwa midomo kama kawaida ulivyo ujanja wa serikalikuwapa chambo.

  HUDUMA DUNI na UHABA WA VIFAA: hili sijui wakulishugulikia ndio hao hao wanaokwenda huko india na SA.


  Kuna mwandishi aliwai kuhoji wananunua mashangingi ili wasitengeneze barabara au hawatengenezi barabara ili wanunue mashangingi ? It is the same story
   
 7. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  -JKN alikwenda matibabu St Thomas hospital ,London
  -Amir Jamal alikuwa Canada
  -Balali alikuwa states
  -Mrema alikwenda India juzijuzi
  -Hata juzi tu,Warioba amekwenda Sauz.

  You never know viongozi wangapi wa sasa wanakwenda Ulaya/India /Sauz kwenye check ups!

  Ina maana Muhimbili na madaktari wetu hawaaminiki.Walala hoi ndio wanaotibiwa kwenye hizi hospital.
  Tuna hypocricy kubwa sana.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  that was and still is my worry.. wanaharibu vya kwetu ili walete vya kwao kwa kutumia vyetu!
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Huduma zetu za afya ni hafifu ... kama wale wanaositahiri kuziboresha huduma za afya hapa kwetu kujenga mahospitali makubwa kwa ajili ya huduma mbalimbali wanakimbilia India sisi tufanyeje tena ?
   
 10. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0


  Mkuu Mtazamji

  Hii mfano unajenga hoja ambayo inasumbua sana jamii yetu.

  Kwa kuongeza tu kwenye Elimu ni hivyo, wenye uwezo wa elimu na fedha wanasomesha watoto wao kwenye Expensive English Medium schools. Kufanya hivi [japo hawataki tuamini hivyo] kunawaondoa wao kabisa kwenye mchakato wa kuboresha Shule za Serikali.

  Mifano iko mingi na yote ukiangalia chanzo chake utaona inafanana kitu kimoja muhimu sana "Priority za Taifa", sasa hivi ni tuna kauli mbiu tu. Taifa linapokuwa na priority kila mtanzania anakuwa anajua wajibu...

  Nitatumia kipindi cha kwanza cha Rais Mkapa; Serikali iliamua kwa dhati kuwa Taifa ni lazima tulipe madeni ya ndani na nje...sidhani kama kuna Mtanzania asiyejua kuwa Serikali inalipa madeni.

  Tunahitaji vipaumbele vya aina hii, mfano kwa nini tusiifanye muhimbili kuwa ndio hospitali bora kuliko zote Afrika? Tukiipa kipaumbele inawezekana....
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ndugu mwanakijiji, sababu kubwa ni kuwa tukitibiwa hapahapa kutakuwa hakuna hela ya marupurupu ya safari ya kwenda kutibiwa. Hela ya hoteli, hela ya chakula, na milango ya ulaji kupitia kuidhinisha watu kwenda kutibiwa India itakuwa imefungwa. Tulifanya hivyo makusudi na tulimpiga vita Dk Massawe kwa sababu hiyo. Kama angeanzisha taasisi yake huko India basi tungemuunga mkono.
   
 12. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Katika huduma ambazo Tanzania ipo nyuma ni sekta ya afya!Ukienda vijijini ukaona huduma za afya utalia!Kwa mtazamo wangu Watanzania wengi wanakufa wa magonjwa yanayotibika!Watanzania wachache sana wenye uwezo wa kwenda kutibiwa nje!
  Kuna watu wanaugua huko vijijini wanashindwa hata nauli ya kuja kutibiwa mijini,kuna wengine wapo mijini wana kuwe watakiwa waende muhumbili wanashindwa hata nauli na pesa za matibabu.
  Siku hizi michango ya kuchangiana kwenda kutibiwa nje na hususan India imekuwa kama michango ya harusi ,kila mtu anataka kwenda India ,watu wameshakataa tamaa na tiba za hospitali zetu na huduma hovyo .
  Serikali inataka kujenga kila kata zahanati itakuwa kama shule za kata hakuna walimu hakuna vitendea kazi,tena walimu ni rahisi kuwapata hata wa form six wanakuwa walimu.
  Je hizi zahanati zitakazo jengwa kila kata kweli watapata madakatari kirahisi kama walimu?
  Juzi nilikuwa kijiji kimoja kuna zahanati lakini haina umeme ina vitendea kazi duni,kuna mgonjwa aliletwa hapo daktari akampa tiba ya malaria nikamuuliza umejueje kama anaumwa malaria?Kajibu ana dalili zote za malaria pia natumia uzoefu!Hakuna mabaara ya kupima malaria,Hivyo ndivyo ilivyo huduma za afya vijijini!Mgonjwa akizidiwa kupelekwa kwenye hospitali za mijini hakuna la gari la kubebea wagonjwa usafiri hakuna miundo mbinu duni!Inaishia watu kufa tu.
  Ukija kwenye hospitali zetu za mjini utakereka wauguzi matusi dr mmoja anahudimia watu elfu moja kwa siku .Kuna rafiki mmoja alikuwa anaumwa pumzi katibiwa muhimbili kaambiwa ana matatizo ya moyo kapewa dawa hapati nafuu,akaamua kuomba msaada kutibiwa India kwa bahati nzuri kachangiwa kwenda India kaambiwa hakuwa na matatizo ya moyo ilikuwa ana matatizo ya asthma!Hizo hospitali zetu!
  Mwanakijiji ukiona wagonjwa wanaokwenda India then wamefia huko then waliondoka Tanzania wakiwa wapo katika hali mbaya ya kutotibika tena utakuta mtu ana cancer grade 4 anaenda India eti apate tiba sana sana ataongezewa ma chemotherapy baada siku kadhaa anakufa!
   
 13. l

  lifelines Member

  #13
  Mar 11, 2010
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana. Inabidi tuzingatie maadili, good customer care,healthcare kwa shughuli za utibabu. Itabidi tuanzishe juhudi za kuendeleza Mind sets za wafanya kazi wa sekta husika na viongozi wetu.
   
 14. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri hakuna lisilowezekana ila kwa nchi yetu yaliyo nje ya uwezo wetu ni mengi na ya msingi kuliko yaliyo ndani ya uwezo. Tatizo kubwa nchini ni pale watawala walipofanya kazi ya siasa kuwa agira yenye kipato cha juu kuliko kazi za kitaalamu. Mfano tujiulize kipaumbele cha afya kwa wanasiasa kuanzia wa chama tawala na hata wa upinzani ni nini? Bajeti ya wizara ukiifuatilia utakuta pesa kubwa zinaitumikia siasa ndani ya wizara husika. Wanaalipana marupurupu, posho za vikao, sijui chakula cha mh, anayetembelea wizara nk. Tatizo la kupeleka watu nje ya nchi kwa check up mimi sijajua kama ni mashine za vipomo hatuna au ni labda madaktari tulio nao hawakusoma kile walichosoma hao wa nje. Uendekezaji siasa umesababisha madaktari wetu kufungua vihosipitali vya uchochoroni na baazi yao wametimkia nchi za nje zenye tabia ya kuheshimu taaluma. Pale muhimbili tunaambiwa pana kitengo cha chuo kikuu cha tiba(muhimbili teaching hospital) wanafundisha nini ikiwa tools za wanachokifundisha hazimo? INAUMA SANA. Sasa ukipewa gharama ya mh mmoja kwenda check up nje ndo utashangaa mwenyewe. Na utakubaliana pato la nchi linaitumikia siasa.
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Tanzania wanafuata tu ulimbukeni wa rais wao kwa sababu tangu alipoingia madarakani yeye kiguu na njia kwenda nje, kwa hiyo kila kiongozi ameona kwenda nje kwa kutibiwa ni mtaji na hakuna sababu yoyote ile ya kuongeza bajeti za elimu, afya nk. WHY wao wenye nchi hawahitaji hizo hudumu hapa nchini watazipata kwa mgongo wa walipa kodi huko ughaibuni.
   
 16. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Huduma ya Afya TZ ni ovyo kabisa.
  Mimi nina ndugu kadhaa wapo kwenye Medical field, vitu wanavyoniambia vinatisha sana kusema ukweli, haya mambo ya kukosea kwenye operation yanatokea daily, sema mengi hayavuji publicly.
  Umeme unakatika katikati ya operation! Hakuna backup! Nawajua madaktari ambao imebidi walazimike kufanya operation kwa TAA YA SIMU! Mashine za oxygen nazo hazifanyi bila umeme, inabidi watumie manual, manual nazo za mwaka 64!

  Hata hizo so called "simple procedure" kama kuweka cast kwenye mguu nazo mara nyingi zinachemsha unakuta wameunga vibaya, so inabidi wakuvunje na kuweka upya.

  Na mbaya zaidi kuna ukosefu wa ethics kwa baadhi ya wauguzi, unaweza ukaambiwa drip fulani hatuna, kumbe ipo wameibana for some reason, mambo ya ajabu sana.

  Tatizo labda ni kutumia fedha za walipa kodi kugharamia matibabu ya viongozi, labda kama wana health insurance ambayo inagharamia.
   
 17. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wamerikani leo wanawatumia madaktari toka india, na pia picha zinatumwa toka US na kwenda India so wahindi wako juu kuhusu masuala ya tiba cha msingi ni Tanzania kuwekeza kwenye Huduma ya afya ikiwa na kusomesha madakari wengi zaidi kuliko ilivyo sasa hivi
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Mar 11, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nadhani Ndugu Reginald Mengi ndiye aliyeona mbali tu ktk hili maanake alikua na Mpango wa kuanzisha hospitali ya Moyo nchini

  Hii ni kutokana na yeye mwenyewe kuguswa kiukweli ukweli coz mara kwa amara amekua akijitolea kuwapeleka nje watoto wasio na uwezo especially India.Mungu Atamlipa kwa hilo

  Tungefanikiwa kuanziasha hospitali moja kubwa tu kama Apollo Indraprastha kwa kweli tungekua tumefanya jambo la maana sana

  Kusema kweli Appollo si hospitali ya kutisha sana,ila wana mtandao mzuri wa kuajiri madaktari bingwa wa kimataifa na specialists wa kutoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa.Tanzania inaweza kabisa kuanzisha mradi kama huu na tukapata wagonjwa kutoka nchi nyingine,ila tuwe makini katika usimamizi na uajiri wa madaktari wetu na wale wa kimataifa
   
 19. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,216
  Likes Received: 2,078
  Trophy Points: 280
  Ulafi ndio umefanya huduma za afya zikawa hafifu.
  Leo hii ukienda pale Muhimbili na wizara ya afya ukapendekeza kwamba unataka tuwe na hospitali ya kutibu wagonjwa wa moyo hapa nchini, unaweza kupotea bila mtu kujua ulipo. Kupelekwa wagonjwa nje ya nchi ni mradi wa watu huu ati! Haiingii akilini kwamba miaka yote hii ya uhuru hatuna daktari wa moyo hapa nchini! Si kweli!
  Fikiria walivyomnyanyasa Dr. Ferdinand Masau wa THI.
   
 20. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Hii sentensi imejaa HEKIMA - acha nitafakari zaidi
   
Loading...