Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,597
- 46,215
Watu wameanza kupatawa na mashaka ya kuja wimbi la tatu la COVID 19. Kwa sabubu kamati ya Rais kuhusu CORONA ilikwisha pendekeza chanjo ziletwe na kila anayetaka achanjwe kwa hiari yake ni vyema Wizara ya Afya ikatangaza kuwaita pamoja wadau muhimu haraka iwezekanavyo ili kuweka mpango mkakati wa pamoja katika kuagiza chanjo na kuzifikisha kwa wananchi wahitaji.
Jambo hili halipaswi kuendelea kucheleweshwa kwa sababu tutapoteza watu wengi kwa vifo bila sababu hasa wezee ambao wako katika hatari kubwa ya kifo endapo watapata hivi virusi. Kila uhai mmoja una thamani kubwa na kila dakika tunayochelewa kuleta hizo chanjo tuko katika ukingo wa kumpoteza mtu mmoja zaidi.
Tayari tumeona nchi nyingine jinsi chanjo zilivyoleta ufanisi ndani ya muda mfupi na kuokoa maisha ya mamilioni ya watu. Tutakuwa watu wa ajabu sana kama tutaka tubembelezwe hata kuhusu kuyathamini maisha yetu wenyewe.Tunaweza kufanya vyema.