Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,209
- 42,071
Serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bwana Abel Makubi amesema kumeanza kujitokeza vitendo vya kujipatia vyeti feki vya chanjo ya Covid-19 hivyo amewaomba wananchi kuwa wasijaribu kujiingiza kwenye mkenge wa kujipatia vyeti feki vya Covid-19.
Katibu Mkuu amesisitiza kuwa kuwa Wizara ya Afya ndio pekee inatoa vyeti vya chanjo ya Covid-19 na kwa sasa iko kwenye mchakato wa kuandaa vyeti vya wote waliopata chanjo hivyo wasidanganywe kupata vyeti feki
Na pia ameendelea kuwaonya watu wote ambao hawajachanjwa chanjo ya Corona wasiendelee na mipango ya kujipatia vyeti feki vya chanjo kwani wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Chanzo: Magazeti
My take:
Katika hili Wizara ya Afya inatakiwa kuwajibika kabisa kwenye huu uzembe unaopelekea watu kuanza udanganyifu kwani walitakiwa kujiandaa kabisa kabla ya kuletwa chanjo , inakuwaje watu wachanjwe halafu wasubiri vyeti?
Kwanini mfumo ule wa utoaji wa vitambulisho vya kupigia kura usingelitumika? Kwanini tusiseme hii ni hujuma? Kweli Waziri na Katibu wake wako makini kweli?