Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini tozo kwa makosa ya uvunjifu wa sheria za usalama barabarani zisishabihiane na uzito wa kosa husika kama ambavyo kodi ya PAYE inavyoshabihiana na ukubwa wa mshahara?

(1) Kwanini dereva wa gari iliyofanya kosa la wrong packing pamoja na dereva aliyefanya kosa la kutosimama wakati taa nyekundu imewaka au overspeeding wanalipa tozo inayofanana ya 30,000/=?

(2) Mbona mfanyakazi anayepokea mshahara basic wa 1,500,000/= pamoja na mwingine anayepokea 300,000/= wanalipa viwango tofauti vya kodi ya PAYE?

(3) Katika kuvuka daraja la Mwalimu Nyerere pale Kigamboni wanalipa kulingana na ukubwa wa gari na kwanini hakuna tozo za kufanana?

(4) Kwanini kusiwe na madaraja ya makosa barabarani na faini zake kama ilivyo kwa P.A.Y.E ukifanya kosa dogo ulipe faini kulingana na kosa husika kama ni dogo unalipa kidogo kama ni kubwa unalipa faini kubwa?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hapo tufanye limepita hilo wazo lako.

Hivi unafahamu hizi gari rahisi zina risk kubwa zaidi kuliko hizo zingine boss. Upande wa safety.

Kwa haraka haraka magari haya ya walala hoi mengi yakipiga mzinga unaokota karatasi/uji kabisa.

Sasa kosa barabarani kwenye vyombo vya usafiri hivi si tungesema 100,000/= maana kiuhalisia tu mtu anakuwa kwenye risk zaidi.

Kuliko hawa wengine
Vipato havifanani kwanini tozo zifanane?
 
Shukrani kwa kushiliki

Mwingine mwenye hoja mbadala anyoshe kidole juu

Tufanye haraka muda wa chakula umekaribia tafadhali
 
Assuming magari yanaenda at same speed, wewe uko na ki corolla chako halafu ukagongwa na Vitz Vs kugongwa na Cruiser lenye ngao, will it be the same?
Hapo ngoja wana CCM waje watujibu.
ElmOZ0cX0AYmNPa.jpg
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini tozo kwa makosa ya usalama barabarani zisishabihiane na ukubwa wa engine ya chombo (CC-Cubic Centimetres) kama ambavyo kodi ya PAYE inavyoshabihiana na ukubwa wa mshahara wa mtumishi?

Kwanini gari kama IST pamoja na Landcruiser V8 yote yakitenda kosa moja la usalama barabarani kama vile overspeeding wanalipa tozo inayofanana ya 30,000/=?

Mbona mfanyakazi anayepokea mshahara basic wa 1,500,000/= pamoja na mwingine anayepokea 300,000/= wanalipa viwango tofauti vya kodi ya PAYE?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Nilikuwa nakuona una akili kumbe hamnazo.
Unafahamu ujira wa madereva wa magari makubwa?
Unafahamu kipato Cha madereva wa malori ukilinganisha na hao wanaopushu luxurious cars?
Be brave
FB_IMG_16041016351482743.jpg
 
Back
Top Bottom