DOKEZO Kwanini Tiketi Mtandao haitumiki?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Tanzania Mpya

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
253
144
App ya tiketi mtandao ilizinduliwa ili kumsaidia abiria kuchagua basi, kuchagua siti na kulipa nauli moja kwa moja mtandaoni yeye mwenyewe bila kusumbuka kupiga simu au kwenda kwa makampuni ya mabasi.

Lakini App hii au mfumo huu haufanyi kazi, na ni muda mrefu hakuna marekebisho wala maboresho.

Wahusika tunaomba mshughulikie mfumo huu ufanye kazi. Tatizo liko wapi??? Kwa nini abiria waendelee kusumbuka kwenda kusumbuana na wapiga debe au kupiga simu ambazo hazipokelewi kwa wakati ili tu kukata tiketi?

LATRA pls, shughulikieni hili tatizo na liwe historia sasa. Tunajiuliza, Kuna haja gani sasa ya Waziri kufanya uzinduzi wa mfumo huu lakini taasisi husika isisiumamie??

Kama Serikali imeufuta basi tuambiwe wananchi.

===========

UPDATES...
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Salum Pazzy amesema

"Bado sijathibitisha kuhusu hilo kwa kuwa uratibu wa ukataji tiketi tunafanya kwa kushirikiana na watu wa NIDC ambao ndio wanaosimamia mfumo.

"Sisi kama wadhibiti tunafanya vikao mara kwa mara, tunafanyia kazi changamoto mbalimbali, maafisa wetu wanasimamia mikoa mbalimbali kwa kuwa Sheria yetu inawataka abiria kutumia mfumo wa tiketi mtandao.

“Kuhusu shida ya mtandao huwa inatokea time to time lakini si kwa kiwango kikubwa kiasi hicho, ni kama vile ilivyo benki ambapo mfumo unaweza kusumbua.

“Mfumo wa kununua tiketi mtandaoni mtu anaweza kununua tiketi popote alipo lakini wasafirishaji wengi wanachofanya wao wanapokea cash kisha wanawakatia kwa kutumia mashine zinazotoa tiketi ya mtandao.”
 
USIKATAE...SEMA SIJUI...

ILIBIDI MNYANG'ANYWE HAYO MAGARI YA SERIKALI NA NINYI MUWE MNAPANDA MABUS TO OBSERVE HIZO KERO...

TICKET MTANDAO INAFANYA KAZI KWENYE SIMU NA VIFAA VYA MAKAMPUNI YA MABUS TU...SIO SIMU ZETU...

HUO ULIKUWA UTARATIBU WA KUMPA MNAYEMTAKA TENDA...NA MLISHAPATA ASILIMIA ZENU BASI...
 
NINGEKUWA RAIS OFISINI KWENU MSINGEKUWA NA GARI HATA MOJA LA SERIKALI...MNGEPANDA MABUS NINYI...TENA KWA NAULI ZENU...HUTAKI ACHA KAZI...WATAAJIRIWA WENGINE.
 
Back
Top Bottom