Kongole LATRA kwa kusimamia mfumo mtandao

Apr 9, 2022
66
32
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imepongezwa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa kusimamia mfumo wa tiketi mtandao hatua hiyo imesaidia kupunguza kero kwa abiria wa usafiri Nchini.

Pongezi hiyo imetolewa wakati Kamati hiyo ikipokea taarifa ya Utendaji ya Mamlaka, Kaimu Mwenyekiti Mtaturu amesema miongoni mwa faida za mfumo huo ni pamoja na kupunguza mianya ya uvujaji wa mapato kupitia mfumo huo abiria anakuwa na uhuru wa kukata tiketi, huku mfumo ukimruhusu mmiliki kuona idadi ya siti zilizokatwa.

“Nawapongeza sana LATRA sababu kupitia mfumo wa tiketi mtandao sasa hivi abiria anaweza kukata tiketi akiwa popote bila kulanguliwa na maajenti, lakini mfumo huu umerahisisha ukusanyaji wa mapato kwa wamiliki na Serikali sababu unaweza kuona idadi za tiketi moja kwa moja kupitia mfumo’’ amesema Mtaturu.

Wakati huo huo Mtaturu ameitaka LATRA kuhakikisha Kampuni ya Reli Tanzania (TRC) na Kampuni ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) zinaharakisha kuingia kwenye mfumo wa tiketi mtandao ili kuwarahisishia abiria kwani wamekuwa wakitumia muda mrefu kupanga mistari katika stesheni ili kupata tiketi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA Habib Suluo ameihakikishia Kamati kuwa itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu na kufanyia kazi ushauri uliotolewa kwa lengo la kuboresha shughuli za usafirishaji ikiwemo kuendelea kuwatahini madereva ili kuhakikisha abiria wanasafiri kwa usalama.
 
Aibu hii
 
Back
Top Bottom