Kwanini Tecno phones hazitambuliwi GSMARENA??

Kwanini Tecno phones hazitambuliwi GSMARENA??

Nilikua na note3 kila siku charge haikai hata Masaa 8 jamaa, akanishtua juzijuzi nikajaribu ki c8 nilivyoona inakaa na charge siku 2 niliamua kuuza ki note 3 na sasa nimechonga mzinga kabisa nikaongeza na phantom-z. Kwa sasa nimeamua kuwa mteja wao kabisa na sasa nataka kuuza hii c8 nasikia wameleta j8 na Mimi nina aleji na kukaa na simu moja mwaka mzima.
Unavyo sema inakaa na charge siku mbili unamaanisha nini... Screen on time ya hiyo simu ni ngapi? Maana kila simu unaweza kukaa na charge siku mbili lakini cha muhimu ni screen on time.. Kwa mfano nikitumia WiFi

Napata battery life
f1e9c31de8c9c5fa715746b07d034722.jpg


Je Tecno yako Inaweza pata screen on time ya 6. 5hrs full kutumia tu youtube, Facebook, whatsapp, instagram? Na 5hrs ukiwa unatumia 4G?
be42162f5a1939046b6a87455137f826.jpg

ce66672182e408c38180d66125a56d88.jpg


Hauwezi kusema tu simu yako ina battery life nzuri bila kutoa supporting evidence.
 
Njaa zinawasumbua watu wa techno eti nina C8 eti nina H6 ,,mbona wa iPhone 6S,7,Galaxy S7+ hawaongei ,,, mwenye ela huwa haongei bhana
 
Mwaka 2014 nilikuwa natumia nokia 1280 yani ya tocho au wengine huita obama , marafiki walinicheka wakinibeza na kasimu kangu na kuniambia nimeshindwa kununua hata tecno ya laki moja ,nikaona isiwe tabu nikaanza kutenge sh 1000 kila siku target yangu ikiwa ni kufikisha sh laki 3 za kitanzania nikanunue simu ya kweli sio mfano wa simu , basi baada ya miezi kadhaa karibia na krismas nikaenda kuchek kibubu nikakuta kuna sh 270000 basi nikabeba haela yangu nikaenda mlimani city pale au wenyewe watoto wa town wanaita kivulini basi ile naingia tu lango la mlimani nikaona bango limeandikwa samsung nikaona ngoja nijisogeze hapa ile nafika tu nakaribishwa na wafada wenye IQ inasoma kama 200 hivi basi nikaoneshwa samsung kali nikajichukulia simu yangu mpya kabisa basi nikabeba na kutaka kuondoka nikasikia sauti ya unyenyekevu ikisema kaka jisajili na warranty ya miaka miwili basi nikajisajili ..... mpaka leo nna simu yangu inang'aa hakuna kuchemka kama jiko wala nn ... simu duniani number one iphone ,number 2 samsung na ya tatu ni lumia
 
,ha ha ha ha ha haya bhana simu hatutengenezi sisi tunasumbua tu ,,toothpick zimetushinda ngoja tuwe ndo soko la kujaribishia vitu vya watu walioendelea duniani
 
Simu za Tecno Wana specifications za uongo. Wakiandika 1gb Ram lakini ni nusu yake. Processor 1.5-1.2ghz ujue ni nusu yake. Wana uongo sana ndio maana chukua samsung ya - 1gb inakuwa 512 mb. Kila kitu ni nusu ya specifications waizoandika apo
 
Simu za Tecno Wana specifications za uongo. Wakiandika 1gb Ram lakini ni nusu yake. Processor 1.5-1.2ghz ujue ni nusu yake. Wana uongo sana ndio maana chukua samsung ya - 1gb inakuwa 512 mb. Kila kitu ni nusu ya specifications waizoandika apo
Qualify your statements with evidence
 
mimi mkuu simu yangu ni LG-5 line moja ni bonge la simu.
 
Tecno H6is far better than Huawei Ascend Y530. Having used both.

Tatizo nililogundua wengi wanaoponda Tecno hawajazitumia. Hebu walioponda hapa watuambie exactly walitumia Tecno ipi kwa muda gani na ilikosa nini. Having used different brands I can see "I'm rich can't eat beans" kind of mentality. Watanzania kwa kujikweza mh..!

huhitaji kutumia simu kujua kama baadhi ya feature ni kimeo. mfano hio h6 gpu yake ni mali 400mp2 ni gpu dhaifu sana mtu ataclaim sichezi games lakini gpu bado ni muhimu. nenda ile thread ya kodi utaona watu kibao wanalalamika kodi inakua nyeusi anaskia sauti bila video ukimdadisi zaidi atakwambia natumia tecno gpu inashindwa kudecode video. inamaana akiplay video/movie anabakiwa na software rendering tu na ambayo hutumia sana cpu na kufanya simu iwe ya moto.

sasa hivi kwenye video tumeshahamia x265 na vp9 kwenye codec tayari movie na series. series ambayo ilikuwa na mb300 kwa hd unaipata kwa mb 80 tu ikiwa hd hayo ndio maajabu ya x265 je gpu zetu za tecno zinaweza? hata tecno ya laki 8 gpu yake haiwezi kuplay hizo video itategemea tu software rendering na kuna wakati pia hio nayo itashindwa sababu cpu za simu hazina nguvu sana.

pia cpu ya h6 ni cortex a7, sasa hivi tumeshahamia 64bit na minimum simu ya kununua 2016 atleast iwe na cortex a53 kwa android. utachat whatsapp na kufanya mambo madogo ila ukija vitu vikubwa hautafanya kitu hapo sihitaji kutumia simu kujua kama cortex a7 ni cpu mbaya.

simu haina 4g sihitaji kutumia simu kujua kama haina 4g

kioo chake kina resolution ndogo na pia huenda sio ips, utakuta hakina protection yoyote ya juu na rangi zake si halisi siku zote vioo vyake vimepauka.

pia soc za mediatek zinakula sana charge simu ya snapdragon yenye specs sawa na mediatek hukaa sana na charge.

at same price ya hio tecno h6 kuna simu za snapdragon 410 kama nyingi kama huawei y550, galaxy core prime, moto e second generation, na nyengine nyingi.
 
hao wanaoponda acha waponde tu Mimi tangia naanza kutumia simu za touch huwa ni mpenzi wa CMU za tecno na sasa hivi namiliki tecno phantom 5 ambayo nimenunua 800k huwa Nina jisikia vibaya sana nikitumia samsung, huawei na simu zingine..uwezo wa kununua hizo zingine upo ila kila mtu a upenzi wake tu..!! maana hawa wanaotumia hizo CMU zingine huwa wanatuona sisi wa tecno kama tuna mic kitu Fulani..huwa nawashangaa sana sisi waafrica huwa tuna tatizo somewher !! ukweli usiopingika kujiona,kujisikia, dharau, uadui tuna shida sana sisi viumbe..

don't take it too seriously !! just a life
Hahaha ni Sawasawa na mtu kusema anajisikia vibaya akiendesha VX V8 lkn akiendesha NISSAN MARCH anakua comfortable Zaid hahah
 
tecno na itel magumashi sana ndio maana hawatambuliki gsmarena.hata ukiinstal cpuz ktk simu hizi utaambiwa unknown manufacture sasa kama mtengenezaji hajulikani kwa nn watu wanakurupuka sana na hizi akina tecno?nunueni simu zenye viwango mfaidi pesa zenu.any way subirini tarehe 16/6 muone mitecno itakavyozimwa na tcra tehetehetehe
Mkuu umeandka lkn ulvyoandka kW kubeza kam konda wa dala2 nmehic kam nakuon ukiongea vleee an..... hhhaaaa
 
Vioo vya Tecno simu. Wakati wa Jua inakuwa na muonekano mbovu sana kingine ktk Bluetooth yake kalibia Tecno nilizoona aifanyi kazi.
 
Cjawah kutumia tecno na sina huo mpango....hehehee hiv ukitumwa simu ndo unapeleka tecno!!! Hhhhaaaa
 
Cjawah kutumia tecno na sina huo mpango....hehehee hiv ukitumwa simu ndo unapeleka tecno!!! Hhhhaaaa
Hahaha halafu wamiliki wa techno siku hizi Wana tabia ya kufuta label kwenye simu zao na kuivisha kasha, hahah sijui kwanini hawapendi kuonyesha superbrand phone yao.
 
Mbona Tanzania mna kila kitu lakini hamtambuliki zaidi mnaambiwa ni masikini kuliko nchi zote Africa sembuse Tecno na gsmarena wacha life isonge kutambulika sio kigezo
 
mimi sifanyi biashara ya simu bali nakufungua macho usiibiwe kwa kununua simu za low quality kama tecno kwa bei juu.bora hizo wanazoasamble dubai kuliko unknown manufacture
****
Ili product yako iingie gsmarena huna budi kilipa $200,000/-
MAKAMPUNI MENGI SANA DUNIANI HUPUUZA UJINGA HUU.
YAANI UJISAJILI KTK SOKO LA UMARIDADI KWA FEDHA ZOTE HIZO IS JUST A SHITS.
KIZURI KITAJIUZA TU.
ALIMRADI IMEA IS GENUINE NO, INTERNATIONALLY.
**WENYE MTANDAO WA GSMARENA NI WAFANYABIASHARA HIVYO NI HIYARI YAKO UJIINGIZE AU LA!!!
 
Back
Top Bottom