Kwanini Tanzania inashindwa kuzalisha tena wachezaji ambao ni "University Graduates" kama akina Engineer Leodgar Tenga? Tunakwama wapi kama taifa?

Ume uliza kitu kizuri maana nasikiaga hiki kinacho tokea uganda leo walikujaga kuiga Tanzania miaka ya zaman ndio maana leo pale Uganda uona mchezaji kama Lwanda ni Engineer na anaupiga mpira wa kutisha ila Tz tuna wachezaj tulio waibua vijiweni ndondo
 
Footballers with degrees: Kompany, Mata & 10 players who went to university | Goal.com

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini Tanzania inashindwa kuzalisha tena wachezaji ambao ni "University Graduates" kama akina Engineer Leodgar Chila Tenga pamoja na ndugu Mohamed Mbwana Bakari "Junior"? Tunakwama wapi kama taifa?

Ninasikia huyu Mbwana Mohammed Bakari "Junior" alikuja kuwa boss mkuu (Commissioner General) wa idara ya uhamiaji hapa nchini baada ya kuacha kucheza soccer.

Ukijaribu kuangalia kwa haraka haraka katika kikosi cha timu ya taifa ya Soccer ya Tanzania (Taifa Stars) utakuta mchezaji mwenye elimu ya juu ni form six tu.

Kwanini vilabu vya soccer/michezo hapa kwetu havitoi msisitizo kwa wachezaji wao kujiendeleza kielimu ilhali inajulikana fika ya kuwa mchezaji hata kama akiwa ni tajiri sana akisoma anakuwa katika nafasi nzuri ya kusimamia vema mali zake?

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya mdau
Tenga kasoma alivyoacha mpira, Mayai kasoma akaacha mpira, hakuna msomi Tanzania ambae alimaliza university akaendelea kucheza mpira tusidanganyane
 
Tenga kasoma alivyoacha mpira, Mayai kasoma akaacha mpira, hakuna msomi Tanzania ambae alimaliza university akaendelea kucheza mpira tusidanganyane
Nilipokuwa benki kuu (BoT) kurugenzi ya utafiti na sera za uchumi niliambiwa na aliyekuwa mkurugenzi wa kurugenzi hiyo Dr. Joe Masawe kipindi hicho kuwa kuna mtu alikuwa anaitwa Mwalusako kama sikosei aliwahi kufanya kazi hapo, aliacha kucheza mpira akiwa Yanga miaka ya 90 mwanzoni akajiunga na benki kuu kama mchumi daraja la pili tayari akiwa na shahada ya Kwanza na ya pili ktk uchumi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 
Ulipiga kazi BOT? Upo vizuri sana mzee baba
 
Kwani nini Jombaa? Nilikuwa nanyoosha maelezo hapo juu ya mtu aliyekuwa anacheza mpira wa ushindani ngazi ya juu kabisa ( super league) huku akifanya full-time programme chuo kikuu hapa hapa Tanzania.
Mishahara ya BOT ni mireeefu sijapata kuona jombaa
 
Back
Top Bottom