Kwanini Tanzania inashindwa kuzalisha tena wachezaji ambao ni "University Graduates" kama akina Engineer Leodgar Tenga? Tunakwama wapi kama taifa?

Footballers with degrees: Kompany, Mata & 10 players who went to university | Goal.com

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini Tanzania inashindwa kuzalisha tena wachezaji ambao ni "University Graduates" kama akina Engineer Leodgar Chila Tenga pamoja na ndugu Mohamed Mbwana Bakari "Junior"? Tunakwama wapi kama taifa?

Ninasikia huyu Mbwana Mohammed Bakari "Junior" alikuja kuwa boss mkuu (Commissioner General) wa idara ya uhamiaji hapa nchini baada ya kuacha kucheza soccer.

Ukijaribu kuangalia kwa haraka haraka katika kikosi cha timu ya taifa ya Soccer ya Tanzania (Taifa Stars) utakuta mchezaji mwenye elimu ya juu ni form six tu.

Kwanini vilabu vya soccer/michezo hapa kwetu havitoi msisitizo kwa wachezaji wao kujiendeleza kielimu ilhali inajulikana fika ya kuwa mchezaji hata kama akiwa ni tajiri sana akisoma anakuwa katika nafasi nzuri ya kusimamia vema mali zake?

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya mdau
Mkuu nakushauri tu uungane na Magufuli lasivyo October mtapokea kipigo cha mbwa mwizi.
 
Mkuu, kwani hao wanafunzi wanaoenda huko UMITASHUMTA na UMISETA si ndio hao hao ambao wapo huku mtaani wanacheza ndondo cup na kuonwa na TFF?

Tatizo ni serikali au ni wanafunzi wenyewe?
Wanaompinga Rais Magufuli ni mafisadi, majizi,wauza madawa ya kulevya na wapiga dili.
 
Soka linamfumo wake hasa baada ya kuonekana ni ajira rasmi. Kwaasili soka ni mchezo unaomuajiri mtu Toka akiwa mdogo na kujikuta akivipa kisogo vitu Kama elimu. Hata ulaya wachezaji graduates wa soka niwachache Sana. Ndio Mana kwenye basketball hususani marekani wachezaji wa NBA wanalazimishwa lazima wawe graduates na mifumo ipo kuanzia vyuoni.
 
Soka linamfumo wake hasa baada ya kuonekana ni ajira rasmi. Kwaasili soka ni mchezo unaomuajiri mtu Toka akiwa mdogo na kujikuta akivipa kisogo vitu Kama elimu. Hata ulaya wachezaji graduates wa soka niwachache Sana.
Ninakubaliana na wewe mkuu...
 
Soka linamfumo wake hasa baada ya kuonekana ni ajira rasmi. Kwaasili soka ni mchezo unaomuajiri mtu Toka akiwa mdogo na kujikuta akivipa kisogo vitu Kama elimu. Hata ulaya wachezaji graduates wa soka niwachache Sana. Ndio Mana kwenye basketball hususani marekani wachezaji wa NBA wanalazimishwa lazima wawe graduates na mifumo ipo kuanzia vyuoni.
USA kuna scholarships za basketball kama sijakosea.

CC: Kiranga ninaomba ufafanuzi wako katika hili mkuu
 
Engineer Leodgar Chila Tenga alikuwa anaitwa timu ya taifa akiwa mwanafunzi pale UDSM
Nasikia alikwenda ziarani Brazili kama sehemu ya kikosi cha yanga miaka ile ya sabini akiwa na lecture notes na vitabu lukuki kujiandaa na University Exam. Alivyourdi tu, akakumbana na msema kweli pale mlimani na bado akapasua!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom