Kwanini website ya Tume/Sekretarieti ya ajira Tanzania (TPSRS) haipo kwenye freebasics.com ili kuwasaidia graduates wenye vipato vidogo?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini website ya tume/sekretarieti ya ajira Tanzania(TPSRS) haipo kwenye freebasics.com ili kuwasaidia graduates wengi wasio na vipato?

Click here>>> Free Basics

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba kuna kijana mmoja ni jirani yangu (jina simtaji) hapa Mbagala ninapokaa alihitimu chuo kikuu UDSM mwaka jana wa 2019 na hana kipato cha kumuwezesha kwenda internet cafe au hata kuweka bando la data la mara kwa mara ili kuweza kuangalia fursa za ajira mitandaoni.

Graduate akipata clue kupitia freebasics, sasa ndio analipa pesa kidogo anaenda internet cafe akiwa na uhakika kuwa kuna nafasi za kazi zimetangazwa, kuliko kwenda cafe kulipa pesa nyingi kisha akakuta hakuna fursa yoyote.

Kama JamiiForums inawajali watu wa vipato vya hali ya chini na kuamua kuwepo freebasics.com, kwanini tume ya ajira inashindwa kuwajali graduates "fresh from school" ambao ni watoto wa wanyonge/wakulima?

Kwani hii freebasics.com ni nini haswa?
==========
Free Basics provides people with access to useful services on their mobile phones in markets where internet access may be less affordable.

The websites are available for free without data charges, and include content on things like news, employment, health, education and local information.

By introducing people to the benefits of the internet through these websites, we hope to bring more people online and help improve their lives.
==========

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Unafahamu kuwa freebasics.com inatumia muundo proxy server kupata internet.

Yaani server ya facebook inasurf tovuti unayoitaka kwa niaba yako, mabadilishano ya data yanakuwa kati ya wewe na freebasic server, na sio tena wewe na tovuti husika.

Kama ni hivyo usalama wa data zako unazotuma ukoje? Kumbuka ni facebook inc hii. Wazo hata halifai.
 
I second this
Unafahamu kuwa freebasics.com inatumia muundo proxy server kupata internet.

Yaani server ya facebook inasurf tovuti unayoitaka kwa niaba yako, mabadilishano ya data yanakuwa kati ya wewe na freebasic server, na sio tena wewe na tovuti husika.

Kama ni hivyo usalama wa data zako unazotuma ukoje? Kumbuka ni facebook inc hii. Wazo hata halifai.
 
Kwani hii freebasics.com ni nini haswa?
==========
Free Basics provides people with access to useful services on their mobile phones in markets where internet access may be less affordable.

The websites are available for free without data charges, and include content on things like news, employment, health, education and local information.

By introducing people to the benefits of the internet through these websites, we hope to bring more people online and help improve their lives.
Nilikuwa sijaisoma hii mkuu. Nilisoma heading pekee kisha nikakurupuka kuanza kujibu
 
Hahaha wakifanya utakuja kulia wakulipe wamekuibia idea yako?!

Tanzania hii kazi ni ubunge, aliomba kushiriki kura za maoni?!

Ajira ngumu, form bado zinatolewa vyama vingine mshauri dogo apeleke maombi.
 
Back
Top Bottom