Kwanini Tanzania hakuna TV station ya kilimo?

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
4,493
2,000
Hongera kwa majukumu popote ulipo!

Uchumi wa Tz kwa kiasi kikubwa unategemea au umefungamana na kilimo.

Kwa kumbukumbu zangu, niwie radhi kama nakosea, hakuna chaneli ya TV inayorusha matangazo /makala kuhusu kilimo pekee.

Je, ni kwa nini hakuna chaneli ihusuyo kilimo tu kwa lugha ya Kiswahili?

Nimekuwa nikifuatilia masuala ya kilimo kupita TV za nje.

Kwa maoni yangu, hii ni fursa kwa wadau wa media.

Na kazi njema iendelee!
 
Narubongo

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
2,769
2,000
Tuzo za ejat kama yule jamaa wa azam wa kipindi cha twende shambani ameshinda tuzo ya makala bora ya kilimo kwa mara ya 3 mfululizo, sababu iliyotolewa ni yeye peke yake amekuwa akituma makala hiyo kuwania tuzo na hivyo ni mgombea pekee kwahiyo anapita bila kupingwa na kupewa ushindi wa mezani. Kuna shida upande wa waandishi wa habari wa makala za kilimo.

Kuna vipindi kama kile cha korosho cha Dr kapinga channel 10 kimenipa maarifa mapana sana.

Kipindi cha lulu itv hawapo serious wanaenda kumtembelea mkulima wa eka 1 dar, mkulima wa parachichi mwenye miti 30!

Vipindi vya kilimo na ufugaji wa kisasa wa kustaajabisha huwa naangalia channel za Kenya hawa jamaa wapo level za ulaya. Wamewekeza sana kuzalisha mbegu bora za kilimo na ufugaji ndio maana wanafanikiwa
 
Star onair

Senior Member
May 31, 2020
146
250
Tuzo za ejat kama yule jamaa wa azam wa kipindi cha twende shambani ameshinda tuzo ya makala bora ya kilimo kwa mara ya 3 mfululizo, sababu iliyotolewa ni yeye peke yake amekuwa akituma makala hiyo kuwania tuzo na hivyo ni mgombea pekee kwahiyo anapita bila kupingwa na kupewa ushindi wa mezani. Kuna shida upande wa waandishi wa habari wa makala za kilimo.
Ni kweli kabisa mkuu wakenya wametuacha mbali kabisa yaani wale jamaa ni wajanja hatari
 
Prodigal Son

JF-Expert Member
Dec 9, 2009
1,010
2,000
Hongera kwa majukumu popote ulipo!

Uchumi wa Tz kwa kiasi kikubwa unategemea au umefungamana na kilimo.

Kwa kumbukumbu zangu, niwie radhi kama nakosea, hakuna chaneli ya TV inayorusha matangazo /makala kuhusu kilimo pekee.

Je, ni kwa nini hakuna chaneli ihusuyo kilimo tu kwa lugha ya Kiswahili?

Nimekuwa nikifuatilia masuala ya kilimo kupita TV za nje.

Kwa maoni yangu, hii ni fursa kwa wadau wa media.

Na kazi njema iendelee!
Kuna sehemu nadhani tunakwama both sector binafsi na serekali

kuna kipindi nilishajiuliza kulikuwa na umuhimu gani wa SUA kuwa na radio na TV ilihali hawatoi mafunzo ya uandishi wa habari,,nilijiuliza baada ya kuona vipindi vingi havihusiani na kilimo wala majibu ya tafiti wanazofanya

Ni kwanini Vyuo vyote hususani vya serekali visinge ungana na TBC na kuanzisha channel ya KILIMO kama TANAPA, NGORONGORO na TTB walivyoungana wakaanzisha safari channel

zipo tafiti nyingi zinaishia kwenye vitabu, mfano juzi nilikuwa namuangalia Mwanafunzi moja wa PhD Ardhi University anatafiti namna ya kuweka BIOGAS kwenye MITUNGI taarifa ni nzuri ipo kwa ENGLISH je mfugaji wa TANDAHIMBA au KAMACHUMU hii habari itamfikiaje???anyway tujitahidi tufanye kitu ili wakulima na wafugaji wapata taarifa kirahisi

Ni jukumu langu wewe na serekali, kwa namna gani pale tutakapokuwa na viongozi wasikivu, wabunifu wanaofikiria kutumia resources ndogo kusogeza hili gurudumu sio kila siku kusingizia ufinyu wa rasilimali
 
Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,283
2,000
Labda waangaliaji watakuwa siyo wakulima. Wakulima wengi hawana TV na umeme, hata huo umeme vijijini umeishia kwenye miji midogo iliyo vijijini, siyo majumbani
 
Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,232
2,000
Labda waangaliaji watakuwa siyo wakulima. Wakulima wengi hawana TV na umeme, hata huo umeme vijijini umeishia kwenye miji midogo iliyo vijijini, siyo majumbani
Mkuu taarifa ya taneseco wanasema nchi nzima imebaki vijijini chini ya 1000 havina umeme na wako na mpango wa kuweka umeme ,kwa hiyo hiyo dhana uanze kuisahau

Wekeni channel ya kilimo na ufugaji tuone tikiti inalimwaje tuone ngombe anafwanywaje Hadi atoe Lita 40 kwa siku

Inahamasisha Sana kufuga na kulima kuliko hivi tumebaki mabubu ili Hali sua inafyetua wataamu na hatujui wanaenda wapi
 
Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
13,168
2,000
Kuna sehemu nadhani tunakwama both sector binafsi na serekali

kuna kipindi nilishajiuliza kulikuwa na umuhimu gani wa SUA kuwa na radio na TV ilihali hawatoi mafunzo ya uandishi wa habari,,nilijiuliza baada ya kuona vipindi vingi havihusiani na kilimo wala majibu ya tafiti wanazofanya

Ni kwanini Vyuo vyote hususani vya serekali visinge ungana na TBC na kuanzisha channel ya KILIMO kama TANAPA, NGORONGORO na TTB walivyoungana wakaanzisha safari channel

zipo tafiti nyingi zinaishia kwenye vitabu, mfano juzi nilikuwa namuangalia Mwanafunzi moja wa PhD Ardhi University anatafiti namna ya kuweka BIOGAS kwenye MITUNGI taarifa ni nzuri ipo kwa ENGLISH je mfugaji wa TANDAHIMBA au KAMACHUMU hii habari itamfikiaje???anyway tujitahidi tufanye kitu ili wakulima na wafugaji wapata taarifa kirahisi

Ni jukumu langu wewe na serekali, kwa namna gani pale tutakapokuwa na viongozi wasikivu, wabunifu wanaofikiria kutumia resources ndogo kusogeza hili gurudumu sio kila siku kusingizia ufinyu wa rasilimali
Nakuunga mkono kwa asilimia zote.Upo sahihi.
 
Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
8,841
2,000
Hongera kwa majukumu popote ulipo!

Uchumi wa Tz kwa kiasi kikubwa unategemea au umefungamana na kilimo.

Kwa kumbukumbu zangu, niwie radhi kama nakosea, hakuna chaneli ya TV inayorusha matangazo /makala kuhusu kilimo pekee.

Je, ni kwa nini hakuna chaneli ihusuyo kilimo tu kwa lugha ya Kiswahili?

Nimekuwa nikifuatilia masuala ya kilimo kupita TV za nje.

Kwa maoni yangu, hii ni fursa kwa wadau wa media.

Na kazi njema iendelee!
Ipo SUATV, Morogoro inamilikiwa na Chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) lengo mojawapo la kuanzishwa kwake ni kutangaza issue za kilimo kwa ujumla wake.
 
Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
4,493
2,000
Ipo SUATV, Morogoro inamilikiwa na Chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) lengo mojawapo la kuanzishwa kwake ni kutangaza issue za kilimo kwa ujumla wake.
Je inapatikana satellite ipi? Tp zipi? Ndio nimeisikia leo, yawezekana ikawa inajulikana hapo SUA tu.
Angalau level za KTN Farmers huku mtaani tungeijua, ingetujua.
Kuna chaneli na vichaneli.
 
Black Mirror

JF-Expert Member
Oct 17, 2019
450
1,000
Mkuu taarifa ya taneseco wanasema nchi nzima imebaki vijijini chini ya 1000 havina umeme na wako na mpango wa kuweka umeme ,kwa hiyo hiyo dhana uanze kuisahau

Wekeni channel ya kilimo na ufugaji tuone tikiti inalimwaje tuone ngombe anafwanywaje Hadi atoe Lita 40 kwa siku

Inahamasisha Sana kufuga na kulima kuliko hivi tumebaki mabubu ili Hali sua inafyetua wataamu na hatujui wanaenda wapi
Mkuu achana na TANESCO hili shirika lina laana ni waongo kupindukia, vijijini umeme bado ni changamoto kubwa sana, watu wengi vijijini bado hawana umeme, nahis kuna haja ya kuchunguza hili shirika, umeme wa REA wanaweka tu kwenye senta za vijiji au sehemu muhimu tu wanasepa huku raia zaidi ya 90% wengine kwenye kijiji husika wanabaki gizani
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,555
2,000
Hongera kwa majukumu popote ulipo!

Uchumi wa Tz kwa kiasi kikubwa unategemea au umefungamana na kilimo.

Kwa kumbukumbu zangu, niwie radhi kama nakosea, hakuna chaneli ya TV inayorusha matangazo /makala kuhusu kilimo pekee.

Je, ni kwa nini hakuna chaneli ihusuyo kilimo tu kwa lugha ya Kiswahili?

Nimekuwa nikifuatilia masuala ya kilimo kupita TV za nje.

Kwa maoni yangu, hii ni fursa kwa wadau wa media.

Na kazi njema iendelee!
Bado kilimo hakijapewa kipaumbele kinachostahili
Hakuna apps za kilimo
Hakuna majukwaa ya kilimo
Hakuna mashindano ya kilimo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom