Kwanini tairi za gari ni nyeusi?

Kwanini tairi za gari ni nyeusi?

Kuna nchi moja ya uajami huko nimeona mashndano ya magari ya formula one g prix, matairi ni damu ya mzee, je huko wanafanyaje kuhusu mambo ya joto? Au wametumia unga wa carbon red?
Naomba elimu plz
Hakuna “carbon red”
Tairi za Formula One (zikiwemo kwenye Azerbaijan Grand Prix au mbio za Mashariki ya Kati kama Abu Dhabi Grand Prix) bado hutengenezwa kwa carbon black, si “carbon red"

Kampuni ya Pirelli huweka mistari ya rangi kwenye ukingo wa tairi (sidewall) tu.

Hivyo tairi inaonekana nyekundu kwa mbali, lakini sehemu inayogusa barabara bado ni nyeusi.
 
Ni kweli rangi nyeusi ina absorb heat haraka na kwa intensity kubwa kuliko rangi nyingine. Ila matairi haya-absorb heat toka kwenye jua au external bodies, yenyewe yanatengeneza joto lake yenyewe kwa mzunguko wa tairi, molecules zina-collide hadi joto la ndani kuongezeka. Sasa rangi nyeusi ipo vizuri kwenye dissipation-kuondoa joto la tairi kuliko rangi nyingine.

Nimeongelea absorption tuliyosoma ya rangi nyeusi na jua vs dissipation ya joto linalotengenezwa na rangi nyeusi/tairi.
 
Malighafi (carbon black) inayotumika kuifanya tairi kuwa imara ndio inayogeuza rangi za matairi kuwa nyeusi. Bila hiyo malighafi, tairi haitakuwa nyeusi.​
 
Kutokana na msuguano wa lami tairi ikiwa nyeupe itakua ngumu sana kupoteza joto, hivyo kupelekea kupasuka kwa haraka.

Wakati tairi nyeusi inapopata joto kutokana na msuguano ndo rahisi kwalo kulitoa nje hivyo hakuna heat rise katika tairi
Zipo za baiskeli nyekundu , blue etc unasemaje?
 
nyeusi ngumu hard to the core
Yeye hajajiuliza kwanini wakoloni walifunga safar wakavuka mabara na mabara kuja kuwafata watumwa weusi huku africa !? Anakaa kujiuliza uliza maswali mepesi tu.
 
Wanajamvi hivi hakuna uwezekano wa viwanda kuunda tairi za rangi tofautitofauti? Au kuna somo hapa?plz!​
Tairi hutengenezwa kwa mpira unaozalisha rangi nyeupe, inayofanana na ile ya maziwa. Hapo mwanzo, masizi yaliongezwa kwenye mchanganyiko wa mpira ili kusaidia kuimarisha mchanganyiko huo wa kikemia, kwani yaliongozwa na kaboni ambayo ilifanya tairi kuwa nyeusi. Hata hivyo, kadiri muda ulivyopita, matumizi ya masizi yalibadilishwa na badala yake kukatumiwa "carbon black," kwani ina sifa zinazoongeza nguvu na uimara wa tairi.

Kwa Nini Tairi za Magari ni Nyeusi?

Ingawa mpira unaotumika kutengeneza tairi una asili ya rangi nyeupe kama maziwa, tairi zote duniani ni nyeusi. Sababu kuu ya mabadiliko haya ni kuongezwa kwa dutu iitwayo Carbon Black wakati wa matengenezo.

Zifuatazo ni sababu tano (5) kuu za kutumia rangi hiyo:

Kuongeza Uimara na Uhai: Carbon Black huimarisha muundo wa tairi na kuifanya iwe ngumu kuharibika (abrasion), jambo linalofanya tairi idumu kwa muda mrefu zaidi ikilinganishwa na tairi nyeupe za zamani.

Ulinzi dhidi ya Mionzi ya Jua (UV): Dutu hii hufanya kazi kama kinga dhidi ya mionzi ya jua inayoweza kuunguza na kuharibu mpira wa tairi mapema.

Kupunguza Joto: Rangi nyeusi husaidia kutoa joto kwa ufanisi zaidi tairi inapokuwa kwenye mwendo, jambo linalozuia tairi kupata joto kali (overheating).

Kuficha Uchafu: Rangi nyeusi husaidia kuficha vumbi, grisi, na uchafu wa barabarani, hivyo kuifanya gari ionekane nadhifu bila kuhitaji kuoshwa kila saa.

Usalama: Ni rahisi kuona vitu vilivyochomeka kwenye tairi nyeusi (kama misumari, vioo, au mawe) kuliko kwenye tairi za rangi nyingine, jambo linalosaidia kuzuia pancha.​
 
Back
Top Bottom