Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 579
Kunakuwa na unga wa kaboni (carbon powder) ambao huengezwa katika mpira (rubber) utumikao kutengeneza matairi. Unga wa kaboni ni mweusi, kwa kawaida. Wakati matairi yatengenezwapo kwa kutumia mpira uliowekwa unga wa kaboni, huimarisha nyuzi zake na yanakwa imara sana na si rahisi kupasuka. Matairi ya rangi nyeupe yaliwahi kutumika sana kipindi cha nyuma, hadi miaka ya 1930 hivi ila kutokana na kuwa hayakuwa na unga wa kaboni yalipasuka haraka sana na kuleta usumbufu kwa watumiaji.
Vilevile, watu wengi walipenda kutumia matairi ya rangi nyingne kwa ajili tu ya urembo au mapambo. Ila kutokana na uchafu wa barabarani, rangi hizo huishia bado kuwa nyeusi na hili likafanya pia swala la rangi kwa ajili ya mapambo lisiwe la msingi sana. Aidha, matairi mengi uyaonayo yakiwa katika rangi tofautitofauti leo (kama mmoja alivyoweka picha hapo juu), si rangi zao mpaka ndani ila yamepakwa hizo rangi tu kwa juu. Matairi hayo yakikwanguliwa rangi, bado yanabaki kuwa meusi. Nadhani hili jibu litakupatia ufumbuzi kidogo