Bujibuji, kasema nani suti ni lazima kwenye harusi za Kikristo?. Kwenye za Kiislamu, jee kanzu na baraghashia ni lazima?.
Ukweli ni kwamba kati yale matukio 3 makuu ya binadamu, kuzaliwa, kuoa na kufa, ni harusi tuu ndio mhusika ana mamlaka nayo, hivyo wengi huamua kuvaa vizuri, kwa Wakristo wanawake shela na wanaume suti ila ni uamuzi binafsi sio lazima.
Kwa taarifa, Nigeria ndio nchi inayoongoza kwa Wakristu wengi barani Afrika, kwenye harusi nyingi huko Nigeria, huvaa mavazi yao ya kiasili na sio suti wala shela!.