Kwanini suti ni lazima kwa harusi ya Kikristo?

So lazima wala muhimu. Unaweza 'ukala' T-Sirt na jeans na ukatinga kwa padre kufunga ndoa halali kabisa
 
Sio lazima... Watu wanavaa kwa mazoea, unaeza kuamua kuvaa tofauti na ukatoka bomba vile vile..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sio lazima maana haijaandikwa popote kuwa uvae vipi siku ya harusi yako
Ni uamuzi wa mtu kuvaa vyovyote siku yake ya harusi ila kwa ajili ya kumfanya Bwana Harusi apendeze ndo maana anachagua suti
Ni uamuzi maana unaweza kuvaa kitamaduni na harusi yako ikafungwa
Wanachoangalia zaidi ni vazi ambalo halitaacha maungo yoyote nje au wazi
So ukivaa lubega ya kimasai kwa uamuzi kuw ando unaenda kufungia ndoa wafungishaji hawawezi kukurudisha wakuambie nenda kavae suti
 
Bujibuji, kasema nani suti ni lazima kwenye harusi za Kikristo?. Kwenye za Kiislamu, jee kanzu na baraghashia ni lazima?.

Ukweli ni kwamba kati yale matukio 3 makuu ya binadamu, kuzaliwa, kuoa na kufa, ni harusi tuu ndio mhusika ana mamlaka nayo, hivyo wengi huamua kuvaa vizuri, kwa Wakristo wanawake shela na wanaume suti ila ni uamuzi binafsi sio lazima.

Kwa taarifa, Nigeria ndio nchi inayoongoza kwa Wakristu wengi barani Afrika, kwenye harusi nyingi huko Nigeria, huvaa mavazi yao ya kiasili na sio suti wala shela!.
 
Kama kuna mwana JF ambaye siku ya harusi yake hakuvaa suti, naomba atutumie picha, nataka niige style, nimechoshwa na mambo ya suti
 
Mkuu Bujibuji ndo maana tukasema ni uamuzi na hakuna mahali popote imeandikwa kuwa ni lazima wanaooana wavae suti
Vazi lolote linaruhusiwa mradi tuu haliachi maungo nje ya wanaharusi
 
mbona kila nimuoaye anavaa suti? Tena wakikosa uwezo wa kununua, wanaenda kuzima?
Ni mkumbo tu bt sio lazima.. Hebu wewe jaribu kutoka kivingine kwenye harusi yako uone kama hawatakuiga... Daaah ila kuazima suti ya harusi ni noma!.. Jikune unapofikia, sio lazima kufanana na fulani...
 
Kama kuna mwana JF ambaye siku ya harusi yake hakuvaa suti, naomba atutumie picha, nataka niige style, nimechoshwa na mambo ya suti

buji huwa hazikukai vizuri nini ..sasa harusi ndo hiyo halafu unatafuta optional
si lazima kama waweza piga hata t -shirt na jeans
 
Siyo lazima ni utamaduni tu ulioigwa kama kuvaa kanzu na lemba alafu ujione wewe ndoo mstaarabu, hivyo basi kuvaa suti siyo lazima sana unaweza vaa vyovyote vile ikawa fresh......... fatilia harusi zinazofungwa pale mwenge kwa Bishop Kakobe hamna suti wala nini bado mtu anaondoka na wake. Asikudanganye mtu mkubwa Bujibuji usiazime suti za watu bana vaa ulivyozoea tu itafana.
 
bujibuji, sio lazima kuvaa suti, ila tu ni mazoea. Wengi huchukulia kuwa suti ni vazi la kiheshima zaidi(#japokuwa mimi sipendi suti na sijawahi kununua na sitegemei kununua)
 
bujibuji, sio lazima kuvaa suti, ila tu ni mazoea. Wengi huchukulia kuwa suti ni vazi la kiheshima zaidi(#japokuwa mimi sipendi suti na sijawahi kununua na sitegemei kununua)

kununua utanunua na utavaa, ni utoto ukikua utajua
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom