Akisoma uamuzi huo, Jaji Sam Rumanyika amesema ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonesha Mbowe na Matiko hawakuruka masharti ya dhamana kama ilivyoelezwa na upande wa Jamhuri.
Mahakama kuu imejiridhisha kwa nyaraka kuwa Mbowe alikwenda Afrika kusini kwa matibabu na akatumia kipindi chake cha mapumziko ya matibabu kwenda Ubelgiji jambo ambalo si kosa kisheria.
Pia Ester Matiko hakufika mahakamani siku ya kesi yake kwa sababu alitumwa na Spika kwenda Burundi kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya mabunge ya Afrika mashariki. Ester aliwasilisha mahakamani barua ya Spika lakini ilikataliwa na kufutiwa dhamana.