Kwanini Spika hakumtetea Ester Matiko kuwa alimtuma Burundi

Mtakuja kuniambia utetezi wake.. Kuwa hakutaka kuingilia muhimili mwingine wa serikali.
Hapa sio suala la kuingilia mhimili mwingine bali inashuhudia jinsi tulikaliwa na viongozi mazwazwa, wewe spika anajua kwamba alimtuma Esther Matiko kwenda burundi kwa shughuli za kibunge halafu anashindwa kusema hayo mbele ya hakimu ?, tunahitaji kudai ukombozi wa nchi hii ili watu wote wawe na haki sawa mbele ya sheria
 
"akatumia kipindi chake cha mapumziko cha matibabu kwenda Belgium ambapo si kosa Kisheria". Wale mapopoma na mavuvuzela ya Lumumba wakiongozwa na Bashite,Ndugai na Kalamaganda mliokuwa mnapiga kelele kuwa Lissu anazurura Marekani na Ulaya wakati ni mgonjwa mmeipata hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu nilikuwa sijaiona hiyo point, kwa hukumu hii Lissu anaweza kuitumia endapo Spika atajaribu kusitisha mshahara wake.
 
Akisoma uamuzi huo, Jaji Sam Rumanyika amesema ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonesha Mbowe na Matiko hawakuruka masharti ya dhamana kama ilivyoelezwa na upande wa Jamhuri.

Mahakama kuu imejiridhisha kwa nyaraka kuwa Mbowe alikwenda Afrika kusini kwa matibabu na akatumia kipindi chake cha mapumziko ya matibabu kwenda Ubelgiji jambo ambalo si kosa kisheria.

Pia Ester Matiko hakufika mahakamani siku ya kesi yake kwa sababu alitumwa na Spika kwenda Burundi kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya mabunge ya Afrika mashariki. Ester aliwasilisha mahakamani barua ya Spika lakini ilikataliwa na kufutiwa dhamana.
Ilishaamliwa kuwa wapelekwe jela. Refer issue ya Mo, baada ya jiwe juz kuikumbushia as if hajui kitu, ndio wiki ijayo utaona hekaheka za watu kupelekwa kisutu. This is a state under one man.
 
Kama lilikuwa agizo, spika hana ubavu wa kumtetea. Hii ilikuwa mission iliyopangwa. Ndiyo maana CAG alisema Bunge ni dahaifu

Kama Matiko alikuwa anajua masharti ya dhamana yake.....
Alipaswa kukataa kazi aliyopewa na Spika, na hata kama Spika angeamua kumchukulia hatua lakini isingekuwa kubwa kama ya hii ya Mahakama....

Vilevile, Matiko alikuwa na uwezo wa kumuandikia barua Spika kuwa awezi kutekeleza wito wake kutokana na masharti ya dhamana aliyonayo, hivyo spika kama alitaka kuendelea na nia ya kumtuma angemjibu kwa barua kumruhusu kuendelea na wito huko akipeleka nakala mahakamani.....

Hivyo iyo barua ya Spika ndiyo ingetumika kama ushahidi na siyo kumwita spika mahakamani......
 
What a shame!Halafu huyo Mashauri ndio kala shavu baada ya kuwasweka rumande kwa miezi 3 na ushee!
Awamu hii ukitaka kupata mafanikio kwa haraka basi wewe wafanyie ubaya wapinzani,hapo utamgusa JIWE na atakuona mtendaji imara na zawadi ya cheo juu!
Halafu nasikia anastaafu kapata ujaji ili astaafu katika level ya judge
 
Akisoma uamuzi huo, Jaji Sam Rumanyika amesema ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonesha Mbowe na Matiko hawakuruka masharti ya dhamana kama ilivyoelezwa na upande wa Jamhuri.

Mahakama kuu imejiridhisha kwa nyaraka kuwa Mbowe alikwenda Afrika kusini kwa matibabu na akatumia kipindi chake cha mapumziko ya matibabu kwenda Ubelgiji jambo ambalo si kosa kisheria.

Pia Ester Matiko hakufika mahakamani siku ya kesi yake kwa sababu alitumwa na Spika kwenda Burundi kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya mabunge ya Afrika mashariki. Ester aliwasilisha mahakamani barua ya Spika lakini ilikataliwa na kufutiwa dhamana.
Hawa walikuwa wafungwa wa kisiasa , full stop !
 
"akatumia kipindi chake cha mapumziko cha matibabu kwenda Belgium ambapo si kosa Kisheria". Wale mapopoma na mavuvuzela ya Lumumba wakiongozwa na Bashite,Ndugai na Kalamaganda mliokuwa mnapiga kelele kuwa Lissu anazurura Marekani na Ulaya wakati ni mgonjwa mmeipata hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app

wacha Mungu huwa hawapepesi jambo.muda wote waogope sana wanafiki na hakika watu hao wasipotuba hawatauona ufalme wa Mungu.Spika wetu kwa kweli hana viwango pia hawezi kuutawala mdomo wake.habakizi maneno ya kuzungumza.wengi mnaona anvyodhalilisha wabunge wenzake na watu wengine pale mjengoni lkn kila jambo lina ukomo wake.wakati ni ukuta na yy muda wake uliisha naye atadhalilishwa.mtenda dhambi hakika atahukumiwa kwa matendo yake endapo hatatubu.
 
Kama Matiko alikuwa anajua masharti ya dhamana yake.....
Alipaswa kukataa kazi aliyopewa na Spika, na hata kama Spika angeamua kumchukulia hatua lakini isingekuwa kubwa kama ya hii ya Mahakama....

Vilevile, Matiko alikuwa na uwezo wa kumuandikia barua Spika kuwa awezi kutekeleza wito wake kutokana na masharti ya dhamana aliyonayo, hivyo spika kama alitaka kuendelea na nia ya kumtuma angemjibu kwa barua kumruhusu kuendelea na wito huko akipeleka nakala mahakamani.....

Hivyo iyo barua ya Spika ndiyo ingetumika kama ushahidi na siyo kumwita spika mahakamani......
Hayo unayoeleza unafikiri Jaji hayajui,

kama umeruka dhamana kinachotakiwa ni kwenda na evidence kitu ambacho Ester alifanya, kosa lililofanywa na hakimu Mashauri ni kukataa kupokea evidence, kwa hiyo Mashauri hakupata muda wa kumuuliza matiko kujua kama ombi lake kwa spika kutoenda Burundi lilikataliwa ama la.

Kilichotakiwa ni mahakama kupokea ushahidi then ndipo hayo maelezo mengine ya kuomba ruhusa au kwa nini hukuomba kubadilishwa yangefuata, halafu hiyo inategemea pia na umuhimu wa kazi uliyotumwa.
 
What a shame!Halafu huyo Mashauri ndio kala shavu baada ya kuwasweka rumande kwa miezi 3 na ushee!
Awamu hii ukitaka kupata mafanikio kwa haraka basi wewe wafanyie ubaya wapinzani,hapo utamgusa JIWE na atakuona mtendaji imara na zawadi ya cheo juu!
Hivi huwa anaenda kanisani kufanya nini?Kuangalia altars ilivyopambwa?
 
Bunge na mahakama wapi na wapi.Kwani bunge ndio lililompa dhamana na masharti yake?
 
kosa lililofanywa na hakimu Mashauri ni kukataa kupokea evidence, kwa hiyo Mashauri hakupata muda wa kumuuliza matiko kujua kama ombi lake kwa spika kutoenda Burundi lilikataliwa ama la.

..Kosa la Makusudi.....
 
Back
Top Bottom